Adui Ndiye Aliyetenda Hivi
Mathayo. 13:28
“Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?”
Yesu alitoa mfano ambao unapatikana katika Mathayo 13:24-30
Kwamba kuna mtu alipanda mbegu na alipolala ADUI akaja akapana MAGUGU! Wale watumishi wa shamba lake wakamuuliza ULIPANDA MBEGU NJEMA, YAMETOKA WAPI MAGUGU?
Yesu akawajibu "NI ADUI NDIYE ALIYETENDA HIVI"
Nina uhakika wengi tuna maswali ya aina hii kwenye maisha yetu! Tumepanda mbegu njema lakini pasipokujua tunaona magugu na hatujui ni nani anawajibika na hayo magugu!
UMETENDA WEMA KWA NIA NJEMA KABISA LAKINI UMEJIKUTA UMEINGIA KATIKA LAWAMA NA UNABAKI UNAMUULIZA MUNGU, KWELI HAYA NDIO MALIPO YA WEMA WANGU? Wengine tumeenda mbali zaidi mpaka kufikia uamuzi wa kusema kama ndio hivi BASI SISAIDII MTU TENA au SITENDI WEMA WA AINA HII TENA
Yesu anatujibu leo "NI ADUI NDIYE ALIYETENDA HAYO"
Umeongea jambo kwa nia njema lakini ukatafsiriwa vibaya na ikakusababishia madhara makubwa na kushutumiwa, na unabaki na maswali, kweli Mungu nilistahili mavuno haya kwa mbegu hizi nilizopanda?
Yesu anakujibu leo "NI ADUI NDIYE ALIYETENDA HAYO"
Umemsaidia mtu au watu au umetoa sadaka ya muda wako lakini ukaeleweka vibaya na unabaki ukijiuliza maswali mengi..
Yesu anakujibu leo "NI ADUI NDIYE ALIYETENDA HAYO"
Umetenga muda wa kutosha kuomba na ku ongeza mahusiano yako na Mungu ukitegemea mambo yawe mazuri lakini badala yake nikama unapokea mabaya badala ya mema, mambo yako ndio kwanza yanakuwa mabaya, na unabaki unamuuliza Mungu je hii ni sawa baada ya kuamua kukutafuta ndio haya yanatokea?
Yesu anakujibu leo "NI ADUI NDIYE ALIYETENDA HAYO"
Umeamua kuacha dhambi na tabia fulani kwenye maisha yako na UMEAMUA KUBADILIKA KWA KUMAANISHA LAKINI NDIO KWANZA WANAKUSHUTUMU KWA TABIA HIZO ULIZOAMUA TOKA MOYONI MWAKO KUZIACHA, na unabaki unajiuliza maswali, KWELI MUNGU UNAJUA NIMEAMUA KUBADILIKA LAKINI MBONA BADO WANANIITA MBAYA NA KUNISHUTUMU? Na kwa sababu hiyo unafikiria bora tu uachane na bidii yako maana ni kama haina matunda, wanaendelea kukuita majina mabaya wakati umeshabadilika!
YESU anakupa jibu leo kwamba NI ADUI NDIYE ALIYETENDA HILO!
Umemueleza mtu shida yako kwa nia njema na kwa nia ya kutafuta msaada lakini ukajikuta umeingia kwenye matatizo na unabaki unajiuliza kwa nini Mungu unanifanyia hivi?
Yesu anakujibu leo "NI ADUI NDIYE ALIYETENDA HAYO"
USIENDELEE KUFIKIRIA KUWA HUYO MTU au HAO WATU NDIO CHANZO AU SABABU YA HAYO YOTE, NI ADUI ! Sio watu au mtu!! Acha kuwaangalia watu!!! Acha kutafuta mchawi, NI ADUI NDIYE ALIYETENDA HAYO!
YESU ALIWAAMBIA WATUMISHI WAKE, Viacheni vikue pamoja MAGUGU NA NGANO! Kwa sababu mkijaribu kung'oa MAGUGU mnaweza mkajikuta mmeng'oa na NGANO!
Najua unapenda sana ungeweza kujieleza mpaka ukaeleweka nia yako, lakini WAKATI MWINGINE UNAPOJARIBU KUREKEBISHA NDIO UNAWEZA KUJIKUTA UNAHARIBU KABISA, UNAWEZA KUJIKUTA UNANG'OA MAGUGU PAMOJA NA NGANO!
Wakati mwingine kujitetea hakusaidii!
Kuna msemo unasema "TIME HEALS"!
Kuna vitu vingine dawa yake ni kuvipa muda tu!
Yesu alisema, YAPENI TU MUDA MAGUGU, muda ndio utaamua UKWELI NI UPI NA UONGO NI UPI!
KAMA HAWAKUELEWI, USIENDELEE KUTUMIA NGUVU NYINGI, ACHA KANUNI YA MUDA IAMUE!
Usiendelee kuumia na kujiuliza maswali, AMUA KUACHILIA NA USONGE MBELE!!
“Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.”
GAL. 6:7, 9-10 SUV
Maandiko hayo yanasema wazi, TUNACHOPANDA LAZIMA TUTAVUNA, lakini ikiwa tu HATUTACHOKA AU KUACHA NA PIA WAKATI UKIFIKA!
Kwa hiyo, KITENDO CHA KUONA MAGUGU WAKATI ULIPANDA MBEGU NJEMA NI ISHARA KWAMBA WAKATI WA MAVUNO BADO!
Palilia na umwagilie mbegu zako kwa UVUMILIVU, NA KUTOCHOKA NA KUZIPA MUDA LAZIMA UTAVUNA!
Usifikirie kwamba MUNGU HAKUONA ULICHOPANDA, WAKATI TU NDIO BADO!!
USICHOKE ETI TU KWA SABABU YA ANACHOFANYA ADUI, ZIPE MBEGU ZAKO MUDA MPAKA ZIIVE NA HAKUTAKUWA NA ATAKAYEPINGA MAVUNO YAKO!
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author