Text

Amebarikiwa Mtu Yule Astahimiliye Majaribu

1 views 1 day ago

Yakobo 1:12

Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Neno hili likutie moyo wewe ambaye UNAPITIA MOTO (MAJARIBU)

-- Una heri (Umebarikiwa) ukistahimili

-- Ukistahimili utakubalika, kisha Utapokea taji kwa kustahimili kwako

-- Walioandaliwa taji ni WAMPENDAO MUNGU, na kustahimili ni moja ya ishara ya KUMPEMDA MUNGU. 

-- Kustahimili ni jambo gumu ndio maana inahitaji KUSTAHIMILI

--Kustahimili ni pamoja na kuendelea KUAMINI WEMA WA MUNGU KATIKATI YA CHANGAMOTO

Warumi 8:28Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

--Kustahimili ni pamoja na KUAMINI NA KUENDELEA KUUONA UPENDO WA MUNGU katikati ya CHANGAMOTO

Warumi 8:28,37-39Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

-- Hata upoteze vyote, usikubali MACHO YAKO YAKAWA KIPOFU KUUONA UPENDO WA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO. 

Waefeso 3:18-19ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo,upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.

-- Mungu afungue macho yako UONE UPANA, UREFU, KIMO NA KINA CHA UPENDO MKUU WA MUNGU ambao umejaa tele hata saa unayopita kwenye MOTO. 

--Kustahimili ni pamoja na KUENDELEA KUMPENDA MUNGU na kutomuwazia mabaya katikati ya MOTO

Ayubu 1:22Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.

--Kustahimili ni KUENDELEA KUMUABUDU MUNGU hata kama bado hajakujibu au hajakutoa kwenye CHANGAMOTO 

Matendo ya Mitume 16:25Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.

--Kustahimili ni pamoja na KUENDELEA KUWA MUOMBAJI hata kama bado ombi hilo halijajibiwa na bado unapita kwenye moto.

Luka 18:1Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.

--Kustahimili ni pamoja na KUENDELEA KUMTUMIKIA MUNGU kwa uaminifu hata katikati ya huo MOTO

--Kustahimili ni KUENDELEA KUWA NA MOYO WA SHUKRANI KWA MUNGU katikati ya MAJARIBU 

Wakolosai 3:15Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.

--Kustahimili ni KUACHA KABISA KUMLALAMIKIA NA KUMNUNG'UNIKIA MUNGU KWA SABABU YA HAYO MAJARIBU 

--Kustahimili ni kuacha kabisa KUWALAUMU WANADAMU SABABU YA HALI UNAYOPITIA

Ni kweli UNAPITIA MOTO, LAKINI Kwa hakika hutateketea

Isaya 43:2Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza

Zaburi 46:1-3Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.

Hakuna jaribu lisilo na mwisho japo saa ya kujaribiwa ni kama unakuwa huoni mwisho. 

ANA HERI MTU YULE ASTAHIMILIYE MAJARIBU, AKIISHA KUKUBALIWA, ATAIPOKEA TAJI YA UZIMA MUNGU ALIYOWAANDALIA WAMPENDAO.

Mimi nimechagua KUSTAHIMILI, nimechagua KUTOKATA TAMAA, nimechagua KUWA UPANDE WA WASHINDI... wewe je?

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

#Umebarikiwa

~Na Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!