Text

Amini Bila Kuona

1 views 1 day ago

Yohana 20:29

“Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.”

Kila mtu angependa KUONA VITU VYA KIROHO KWA MACHO YA NYAMA halafu ndipo akaamini kirahisi, lakini Neno la Mungu halituhakikishii kwamba TUTAONA KWA MACHO YA NYAMA MAMBO YA ROHONI, lakini linatuhakikishia kuwa SISI TUNA HERI ZAIDI TUNAOAMINI PASIPO KUONA kuliko walioona wakaamini.

Kila mtu angependa KUMUONA YESU KWA MACHO YA NYAMA, lakini NENO LA MUNGU LINASEMA tuna heri TUNAOAMINI UWEPO WAKE KATIKATI YETU BILA KUMUONA.

“Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.” Ufunuo 3:20

Kila mtu angependa kuwaona malaika, lakini TUNA HERI TUNAOAMINI UWEPO WAO KUTULINDA PANDE ZOTE bila kuwaona sawa na NENO LA MUNGU katika

"Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote." Zaburi 91:11

Kila Mtu angependa kuiona Mbingu na Jehanam ndipo aamini, lakini tuna heri TUNAOAMINI uhalisia wa Mbingu na Jehanam sawa na Neno la Mungu.

Kinachozalisha matokeo KWENYE MAISHA YA MKRISTO SIO KUONA BALI NI IMANI.

Pamoja na kwamba Tomaso alimuona Yesu kwa macho, hatuoni akiwa na matokeo makubwa kama walioamua kumwamini bila kumuona kwa macho.

KUONA KATIKA MWILI HAKUZALISHI IMANI bali KUAMINI KUTAZALISHA KUONA KATIKA MWILI.

“Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?” Yohana 11:40

Hauanzi UTUKUFU, inaanza IMANI, ndio maana YESU akamwambia Martha, sikukuambia UKIAMINI UTAUONA UTUKUFU WA MUNGU?

Utukufu wa Mungu ni HESHIMA, AFYA, ULINZI, UZIMA nk.... Ukiamini UTAUONA UTUKUFU.

Imani inazalisha Utukufu wa Mungu....

Nikiamini ULINZI NITAZALISHA ULINZI HALISI, NIKIAMINI UPONYAJI hata kama siuhisi mwilini mwangu nitazalisha KUPONA. Nikiamini UZIMA nitazalisha AFYA mwilini.

Kwa kuwa INAANZA IMANI ndipo kunakuja KUONA, kwa hiyo SIHITAJI KUONA CHOCHOTE NDIPO NIAMINI.

Wakati sahihi wa kuamini, ni pale ambapo HUONI DALILI zozote za nje za kukufanya uamini.

IMANI na KUONA ni pande mbili tofauti kabisa. Ni sawa na GIZA NA NURU.

Mahali ambapo kuna NURU, GIZA haliwezi kuwepo, na mahali penye GIZA, NURU haipo.

UKISHAONA huitaji imani, na UKIAMINI kuona hakuna mchango wowote...

Yaani sihitaji KUONA CHOCHOTE ili NIAMINI...

Yaani kama SIONI chochote ndio wakati sahihi KUAMINI.

IMANI INA NGUVU ZAIDI PALE AMBAPO HAKUNA CHA KIMWILI CHA KUKUFANYA UAMINI. NA IMANI YA AINA HIYO NDIO YESU ALISEMA WANA HERI WALIO NAYO.

IMANI BILA KUONA NI HERI SABABU INA UWEZO WA KUZALISHA KUONA UNACHOTAKA KUKIONA.

SWALA LA KUONA SIO LA MUHIMU INAPOKUWEPO IMANI SABABU IMANI YENYEWE NDANI YAKE INAO UWEZO WA KUZALISHA KUONA (VYA KUONEKANA).

Yaani IMANI INAO UWEZO WA KU     FANYA VISIVYOONEKANA VIKAONEKANA, VISIVYOKUWEPO VIKAWEPO...

IMANI NI MUHIMU KWA SABABU NI SAWA NA UFUNGUO WA KUINGILIA KWENYE ULIMWENGU AMBAO UNA KILA KITU TUNACHOKIHITAJI HATA KAMA HATUKIONI KWA MACHO.

IMANI INATUWEZESHA KUNUNUA KILA TUNACHOKIHITAJI TOKA ULIMWENGU WA ROHO NA KUKIFANYA KIONEKANE KATIKA ULIMWENGU WA MWILI.

IMANI haitishwi na kutokuonekana kwa kitu kwa sababu NDANI YA IMANI upo uwezo wa KUKIFANYA KISICHOONEKANA KUONEKANA.

“Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.” Waebrania 11:3

“Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake;” Waebrania 11:11

Kuona hakuna nguvu kwa sababu kunakuwekea mipaka, yaani ukishaona, HUWEZI KUPATA ZAIDI NA UNACHOKIONA.

Ukiweza kukiona kwa macho, maana yake KITU HICHO KIPO TAYARI KATIKA ULIMWENGU WA MWILI ambao una mipaka ya MUDA, MAENEO, NA VITU.

IMANI haina mipaka (ya muda, fedha, maeneo, vitu nk), KILA UNACHOWEZA KUAMINI UNAWEZA KUKIONA... LAKINI KUONA KWA MACHO KUNA MIPAKA.

Ukiangalia JUU KWA MACHO YA NYAMA, UTAONA MWISHO KUNA BLUU     , SABABU MACHO YA NYAMA YANA MIPAKA LAKINI MACHO YA IMANI HAYANA MIPAKA, NA KILA UNACHOWEZA KUKIONA KWA MACHO YA IMANI, UNAWEZA KUKIMILIKI.

“BWANA akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi;” Mwanzo 13:14

Hayo ni macho ya IMANI...

“Jesus said to him, “Because you have seen Me, do you now believe? Blessed [happy, spiritually secure, and favored by God] are they who did not see [Me] and yet believed [in Me].” JOHN 20:29 AMP

TUMEBARIKIWA [TUNA FURAHA, TUKO SALAMA KIROHO, NA TUNA NEEMA NA KIBALI CHA MUNGU] TUNAOAMINI BILA KUONA.

UNGANA NASI, AMINI BILA KUONA, UFURAHIE ULIMWENGU USIO NA MIPAKA.

Kumbuka: Hatuanzii kwenye KUONA, tunaanzia kwenye IMANI.

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!