Amua Kusamehe
Mathayo 6:14-15
“Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.”
Tunawajibika kusamehe, na Mungu ameuweka msamaha mahali pagumu sana.
Anasema, tusiposamehe na yeye hatatusamehe. Yaani kama kuna mtu sijamsamehe basi hata nisijihangaishe kwenda mbele za Mungu kuomba msamaha.
Kwa hiyo, nikienda mbele za Mungu kuomba anisamehe, anaangalia kama kuna mtu yeyote sijamsamehe, Mungu azuia msamaha wangu.
Kimsingi sio Mungu anazuia msamaha bali ni mimi mwenyewe ninajizuilia msamaha wangu.
MSAMAHA wa Mungu siku zote upo kwa ajili yetu lakini sisi ndio tunao ufunguo wa kufungua kuuchukua au kuufungia ndani tusiufurahie.
Kinachoogopesha kwenye hilo andiko ni andiko hilo kutotaja aina ya makosa, yaani KOSA LOLOTE NILAKOSHINDWA KUSAMEHE LINANIZUIA KUSAMEHEWA.
KILA KOSA, BILA KUJALI NI KUBWA AU NI DOGO, LINA UWEZO WA KUNIZUILIA KUSAMEHEWA NA MUNGU.
Kwa hiyo salama yangu ni KUSAMEHE KILA KOSA NITAKALOKOSEWA, liwe kubwa au dogo.
Jambo hili sio rahisi lakini kwa Neema na Pendo la Mungu ndani yetu, tunao uwezo wa KUSAMEHE KILA KOSA.
Tunao uwezo, na tunalazimika kuwasamehe wanaotukosea MAKOSA AINA ZOTE, NDIO MAKOSA AINA ZOTE, HATA HILO AMBALO WAKATI UNASOMA UJUMBE HUU UNALIFIKIRIA KWAMBA NI KUBWA SANA HALISAMEHEKI.
Tunapaswa kuwasamehe, wenzi wetu, wazazi wetu, ndugu zetu, marafiki zetu, jamaa zetu na watu wote tunaohusiana nao, MAKOSA AINA YOTE AMBAYO WAMEWAHI KUTUSAMEHE NA AMBAYO WATAKUJAKUTOKOSEA.
HII NI KWA USALAMA WETU NA HATMA ZETU.
Ni bora kujiandaa kabisa, kisaikolojia na kiufahamu na kiroho, KUSAMEHE KILA AINA YA KOSA, kwa sababu ukweli ni kwamba MAADAMU TUNAHUSIANA NA WATU LAZIMA WATATUKOSEA, na inawezekana kabisa SIKU MOJA WAKATUKOSEA MAKOSA AMBAYO TUMEYAORODHESHA KAMA MAKOSA MAKUBWA YASIYOSAMEHEKA.
JIANDAE KUSAMEHE, KWA SABABU KWA HAKIKA UTAKOSEWA.
Kitu kingine kigumu kwenye maandiko hayo ni kwamba, HILO ANDIKO ALISEMI HIVI:
Kwa maana mkiwasamehe watu (WANAOWAOMBA MSAMAHA) makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu (WANAOWAOMBA MSAMAHA) makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Yaani hicho kipengere cha KUOMBWA MSAMAHA hakipo kwenye maandiko hayo.
Binafsi yangu NATAMANI ANDIKO HILO LINGEBORESHWA NA KUONGEZEWA KIPENGERE HICHO, LAKINI KWA BAHATI NZURI JAMBO HILO HALIWEZEKANI, YALIYOANDIKWA YAMEANDIKWA.
Kwa hiyo salama yetu, NI KUJIANDAA KUSAMEHE TU BILA HATA KUOMBWA MSAMAHA.
Salama yetu ni KUAMUA KUTEMBEA NA MISAMAHA MIFUKONI MWETU ILI TUKIKOSEA TUNAKUWA RAHISI KUSAMEHE.
Salama yetu ni KUAMUA KUTANGAZA MSAMAHA BURE KWA KILA ALIYETUKOSEA NA ATAKAYETUKOSEA.
Kuna kitu nimekigundua kwa uzoefu wangu, HAKUNAGA KOSA KUBWA MBELE YA MSAMAHA.
KOSA HUWA LINAONEKANA KUBWA KABLA TU MTU HAJAFANYA MAAMUZI YA KUSAMEHE, NA WAKATI MTU AKILITAFAKARI KOSA NA UBAYA WAKE, LAKINI AKIAMUA KUFIKIRIA NAMNA YA KUFANYA ILI KUSAMEHE KWA GHARAMA YOYOTE, BASI ULE MSAMAHA GHAFLA UNAANZA KUONDOA UKUBWA WA KOSA.
MSAMAHA NI MKUBWA KULIKO KOSA LA AINA YOYOTE, NA HAKUNA KOSA LINALOSHINDWA KUSAMEHEKA KAMA MTU AKIAMUA KWA DHATI.
Msamaha ni kwa faida yetu, kusamehe ni kwa faida yetu zaidi kuliko hata wale waliotukosea, na maandiko yanathibitisha hilo.
Nikisamehe ni kwa faida yangu, ukisamehe ni kwa faida yako, usiposamehe ni kwa hasara yako.
--KUSAMEHE WOTE WALIOKUKOSEA, AMUA KUSAMEHE WOTE WATAKAOKUKOSEA.
--TEMBEA NA MISAMAHA MFUKONI UKISUBIRI KUIGAWA UKIKOSEWA.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author