Text

Badiliko la Kweli ni Leo/Sasa

1 views 1 day ago

2 Wakorintho 6:2b

"...tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa."

Kuna watu wengi husema, ipo siku nitabadilika tu na kujifariji kwamba hiyo siku isiyojulikana itafika ambayo ATABADILIKA. 

Mtumishi wa Mungu mmoja, rafiki yangu, alisema, Mwanadamu ana siku tatu tu za kuishi, nazo ni JANA, LEO na KESHO.

Kisha akasema, Jana imeshapita na hatunayo tena, kwa hiyo tumebakiza siku mbili, ambazo ni LEO na KESHO. Lakini pia, KESHO hatuna uhakika nayo sababu haiko mikononi mwetu, na hatuwezi kujihakikishia sana, kwa hiyo SIKU PEKEE TULIYONAYO NI LEO.

Kwa hiyo, kimsingi, Siku pekee Mungu aliyokukabidhi ni LEO. Jana imepita si yako na hakuna lolote unaloweza kufanya kuhusu jana yako, KESHO pia hauna uhakika nayo, inaweza kuwa yako au isiwe yako, lakini LEO una uhakika nayo na ndio iko mikononi mwako.

Neno la Mungu nililonukuu hapo juu linasema ...tazama, uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.”

Neno hilo kimsingi linaingia ndani zaidi, halisemi tu kuhusu LEO, linasema SASAWakati uliokubalika mbele za Mungu sio JANA, sio KESHO, ni LEO na kimsingi sio tu leo bali ni SASA. Maana yake ni kwamba uko msaada wa Mungu kwa BADILIKO lako SASA ikiwa utafanya maamuzi ya kubadilika SASA.

Jambo lolote ambalo umeshawishika ni sahihi kulifanya au unapaswa kulifanya, wakati sahihi kulifanya ni SASA.

Badiliko lolote la kweli la maisha ni lile ambalo UTAAMUA KULIFANYA/ KULIANZA SASA.

Kumbukumbu la Torati 30:19 Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;

UZIMA NA MAUTI, BARAKA NA LAANA viko mbele yako LEO, SIO KESHO na Neno la Mungu linatupa jibu sahihi kwamba LEO TUCHAGUE UZIMA/ BARAKA. 

Kesho sio siku ya kufanya uchaguzi, kesho ni siku ya kuona matokeo ya uchaguzi wa leo. Leo ndio SIKU YA KUCHAGUA UZIMA AU MAUTI, KESHO NI SIKU YA KUISHI UZIMA AU MAUTI. Leo ndio siku ya kuchagua BARAKA AU LAANA, kesho ni siku ya kuishi katika Baraka au Laana.

Bahati mbaya ni kwamba, hata tusipochagua leo tutajikuta tunatembea kwenye matokeo tusiyoyachagua kwa hiyo ni bora kuchagua.

Usipochagua UZIMA leo, bila kupenda (by default) umechagua MAUTI. Kwa kutomchagua YESU/ WOKOVU leo, UMECHAGUA MAUTI/ JEHANAM. 

Yoshua 24:15 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi LEO mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.

Joshua anasisitiza tena "Chagueni hivi LEO mtakayemtumikia". Usipochagua kumtumikia Mungu leo, umechagua kutumikia miungu, hakunaga kuwa katikati (neutral). 

Usipochagua KUBADILIKA leo, maana yake umechagua KUTOKUBADILIKA.

Usiniambie utabadilika kesho, usiniambie utaokoka kesho, usiniambie utaanza tabia ya maombi kesho, usiseme kuanzia Kesho utaanza kuwa msomaji mzuri wa Neno, usiseme utaanza kuishi maisha matakatifu na ya ucha Mungu kesho.

BADILIKO LA KWELI LINAANZA LEO, NA KIMSINGI SI LEO BALI NI SASA, AMUA SASA. CHAGUA SASA. Wakati uliokubalika ni SASA. Unao msaada wote wa Mungu nyuma ya maamuzi ya kubadilika ukiamua SASA.

Jiulize tangu lini umekuwa ukihairisha hayo maamuzi ya kubadilika? 

Kila siku unasema nitaacha tabia hii mbaya.

Kila siku unasema NITAACHA MAHUSIANO HAYA AMBAYO YANANISABABISHA NIMKOSEE MUNGU KILA SIKU.

Wakati sahihi wa KUVUNJA HAYO MAHUSIANO SIO WIKI IJAYO WALA KESHO, WAKATI SAHIHI NA ULIOKUBALIKA NI SASA. Usiendelee kujihurumia UTAJIANGAMIZA. Unavyoendelea kuchelewa, unachagua MAUTI, unakataa UZIMA.

Mungu amekuwa akikupa nafasi kila SIKU lakini wewe ni shahidi namna ambavyo umekuwa ukimuangusha KILA SIKU (you let Him down everyday) KWA KISINGIZIO CHA KWAMBA UTABADILIKA KESHO. UTAOKOKA KESHO, UTAANZA KESHO.

If you are already convinced and convicted in your heart that you have to CHANGE, it is better you change NOW!!! Tomorrow might be too late, tomorrow might not be yours.

Kama umeshashawishika ndani ya moyo wako kwamba UNAPASWA KUBADILIKA, ni vizuri UBADILIKE SASA, ya kesho huyajui, KESHO UNAWEZA UKAWA UMESHACHELEWA, KESHO INAWEZA ISIWE YAKO.

2 Wakorintho 6:2b “...tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa."

 

*#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

*#Umebarikiwa

~ Na. Mwl. Francis M. Langula

+255754711247

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!