Bwana Atakuondolea Ugonjwa Wote
Kumbukumbu la Torati 7:15 SUV
“Na BWANA atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yoyote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao.”
Ni kusudi la Mungu kukuondolea UGONJWA WOTE!
Yaani kuondoa ugonjwa, chanzo chake na dalili zake zote!
Yaani kuondoa ugonjwa na madhara yote yaliyosababishwa na ugonjwa.
Yaani kuondoa ugonjwa halafu ukabaki kama hujawahi kuumwa kabisa!
Linapokuja swala la uponyaji, USIKUBALI KUPATA NAFUU TU, ING'ANG'ANIE AHADI YA MUNGU KWA UKAMILIFU WAKE!
Do not be settled for releaf, God promised wholeness, complete healing!
Naamani, yule aliyekuwa ana ukoma, alipoponywa Neno la Mungu linasema, ngozi yake ilikuwa kama ya mtoto mchanga, yaani hata ukimchunguza, huwezi kabisa kuona dalili kama aliwahi kuwa na ukoma!
Ukoma ulibaki ushuhuda tu!
Kwanini Mungu yuko tayari au anataka kutuondolea UGONJWA WOTE?
1. Kwa sababu Yesu alishughulika na CHANZO CHA MAGONJWA pamoja na MAGONJWA YENYEWE
"Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote," Zaburi 103:3 SUV
Kabla ya dhambi hakukuwa na ugonjwa wowote, magonjwa yote yanaonekana baada ya anguko la adamu, kwa hiyo CHANZO HALISI CHA MAGONJWA DUNIANI NI DHAMBI!
YESU ALIKUJA KUSHUGHULIKA NA DHAMBI ambacho ni chanzo, KWA HIYO ALISHUGHULIKA NA MAGONJWA PIA.
Swala la AFYA NA UPONYAJI NI "DONE DEAL" MBELE ZA MUNGU, KAMA ILIVYO SWALA LA MSAMAHA WA DHAMBI!
2. Kwa sababu, tunapokea uponyaji kwa njia ya IMANI, na imani ikiachiliwa haishughuliki na dalili tu bali na chanzo.
“Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini. Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia. Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.” Marko 11:13-14, 22-23 SUV
IMANI katika kuukemea mtini haikukausha majani tu bali ilianza na chanzo (mizizi) pamoja na matokeo (matawi). Vivyo hivyo imani inapaswa kufanya kwa MAGONJWA. IMANI ikiachiliwa huweza kuondoa UGONJWA WOTE!
3. Kwa sababu ameahidi katika Neno lake, kwa hiyo yuko commited kutimiza alichoahidi.
“ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma”. Isaya 55:11 SUV
Kila alichoahidi Mungu, maana yake ameji commit kukitimiza, ameahidi kutuondolea UGONJWA WOTE, maana yake yuko tayari kufanya hivyo!
4. Kwa sababu anataka kututofautisha na dunia.
Mungu anapenda sana kututofautisha katika kila eneo na dunia inayotuzunguka! Alilithibitisha hili kwa Wana wa Israel pia. ALIWATOFAUTISHA KABISA NA WAMISRI WAKATI WA YALE MAPIGO KUMI
Sisi tunapaswa KUTOA MAJIBU KWA DUNIA HATA KATIKA ENEO LA AFYA NA UPONYAJI, MASWALA YALIYOSHINDIKANA HOSPITAL YANAPASWA KULETWA KANISANI NA KWA WATU WALIOOKOKA; Kama mambo hayako hivyo maana yake sisi kama kanisa na watumishi wa Mungu tunawajibika, kuna mambo hayako sawa!
“Kisha BWANA atawatenga wanyama wa Israeli na wanyama wa Misri; wala hakitakufa kitu cho chote cha wana wa Israeli.” Kutoka 9:4 SUV
“Basi Musa akaunyosha mkono wake kuelekea mbinguni; kukawa na giza nene katika nchi yote ya Misri muda wa siku tatu; hawakupata kuonana mtu na mwenziwe, wala hakuondoka mtu mahali alipokuwa muda wa siku tatu; lakini wana wa Israeli wote walikuwa na mwanga makaoni mwao.” Kutoka 10:22-23 SUV
5. Kwa sababu Yeye ni BWANA atuponyaye - Jehova Rafa.
Mungu mponyaji (Jehova Rafa) ni JINA la Mungu ambalo lipo kwa sababu ya KAZI YAKE YA KUPONYA!
Kama nimeacha kufundisha, sina sababu ya kuitwa MWALIMU, kama SITIBU sina sababu ya kuitwa DAKTARI.
Udaktari sio jina la sifa tu, bali ni jina la kazi anayofanya mtu.
Yehova Rafa, ni jina analojitambulisha nalo Mungu kwa kazi anazozifanya za KUPONYA hata yale magonjwa ya KUFISHA!
“akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye”. Kutoka 15:26 SUV
KIMSINGI, HAKUNAGA UGONJWA WA KUFISHA KWENYE MWILI! KILA UGONJWA UNAWEZA KUPONA.
6. Kwa sababu sisi ni wenyeji wa UFALME WA MUNGU ambao magonjwa si sehemu ya ufalme.
“Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.” Isaya 33:24 SUV
NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHI YETU UGONJWA KUFANYA MAKAO NDANI YA MIILI YETU.
MAADAMU UMESAMEHEWA MAOVU YAKO, HURUHUSIWI KUWA MGONJWA
USIKUBALI UONEVU WA ADUI TENA! UTAIFA WAKO HAUKURUHUSU KUENDELEA KUWA MGONJWA. ING'ANG'ANIE HAKI YAKO KAMA MWANA WA MUNGU!
TUNA SABABU ZOTE ZA KUWA WAZIMA KIKAMILIFU
AHADI HIZI HAZIJALISHI NI AINA GANI YA UGONJWA UNAUMWA! UKIZIONA NI ZAKO, ZITAFANYA KAZI.
MUNGU YUKO TAYARI KUKUONDOLEA UGOJWA WOTE, KAMA UKITHUBUTU KUAMINI!
Ukipenda unaweza ukanishirikisha tukaamini pamoja ili Mungu AONDOE UGONJWA WOTE MAISHANI MWAKO NA WALE UWAPENDAO!
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author