Heshima Yetu Iko Katika Kuwaleta Watu Kwa Yesu
Mathayo 28:19 SUV
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;”
“Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.” Danieli 12:3 SUV
MAMBO YA KUJIFUNZA:
Vitu vya muhimu sana hutamkwa mwishoni ili visisahaulike!
Ninaamini Yesu alikuwa na mengi sana ya kuwaambia wanafunzi wake lakini hakuwa na muda wa kuwaambia yote; kwa hiyo ilimlazimu achague cha muhimu kuwaambia ambacho asingependa kisahaulike na ndipo anasema maneno hayo niliyonukuu, kwamba "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;"
Nimekuja kugundua, heshima yetu itapanda kwa kasi kama tukiwaleta watu kwa Yesu!
Heshima inapanda kwa kasi ukiongoza watu katika kutenda mema au kutenda haki!
“Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.” Danieli 12:3 SUV
Sasa wale tunaopenda mambo ya nyota hapa ndio mahali pake!
Ukiwaongoza watu kutenda haki au ukiwaleta watu kwa Yesu, lazima utang'aa kama nyota!
Safisha nyota yako kwa kuwaongoza watu katika haki; achana na habari ya kung'ang'ania kila siku uombewe na kuwekewa mikono ili nyota yako ing'ae
KUWALETA WATU KWA YESU NDIO AGIZO LETU
Kama kweli una Yesu ndani yako, huyo Yesu kwa kweli hawezi kukaa kimya kwa wenye dhambi kwa sababu Yesu alisema "Sikutumwa ila kwa ajili ya wenye dhambi"
Neno la Mungu linasema:-
"Nawezaje kutulia ikiwa Bwana amenipa agizo"
Kila anayetulia na injili bila kuwashuhudia watu, ukimfuatilia utagundua hana agizo la Bwana Ndani yake!
Napenda kauli mbiu ya kanisa moja kubwa duniani inasema hivi, "Every Winner is a soul Winner"
Unajiitaje MSHINDI na wakati hauleti watu kwa Yesu?
Hatujaokoka ili twende Mbinguni mara baada ya kuokoka, mbinguni ni nyumbani kwetu kwa hiyo huko ni destination yetu! Tumeokoka ili kuujenga UFALME WA MUNGU HAPA DUNIANI, na njia moja wapo ni kuhakikisha TUNAWATOA WATU WENGI IWEKEZENAVYO KWENYE UFALME WA GIZA WA SHETANI!
“Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu.” Mithali 11:30 SUV
“The fruit of the righteous is a tree of life; and he that winneth souls is wise.” Proverbs 11:30 KJV
Nimegundua kizazi hiki Mungu anatafuta watu ambao kwa kila wanachokifanya wanafikiria kumnyanganya shetani watu na kuwaleta kwa Yesu! Yaani OFISINI unawaza ninawaletaje watu kwa Yesu, Eneo la Biashara unawaza hilo, UNAPOPATA PESA UNAWAZA NATUMIA KIASI GANI KWA AJILI KUUJENGA UFALME; yaani kwenye kila unalofanya unauwaza ufalme wa Mungu kwanza ikiwa ni pamoja na AGIZO KUU LA KUWALETA WATU KWA YESU! MUNGU AKIMPATA MTU WA AINA HII LAZIMA AMBARIKI HATA KIFEDHA PIA MAANA ANA UAHIKIKA NI KWA AJILI YA UFALME WAKE!
Hawa ndio wanaitwa KINGDOM MINDED PEOPLE; na HUKO NDIKO MUNGU AMESHAAMUA KUUELEKEZEA UCHUMI USHIKWE NA WATU WA AINA HIYO!
“Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Mathayo 6:33 SUV
Mungu yuko tayari kuwazidishia watu ambao wameamua KUUFIKIRIA NA KUUTUMIKIA UFALME KWENYE KILA ENEO LA MAISHA YAO!
Tuhakikishe Shetani ananyang'anywa watu kila iitwapo leo na UFALME wa Mungu unajaa watu!
Hizi siku za mwisho watu wanatakiwa waujie ufalme wa MUNGU kwa makundi makundi!
Atakayeifanya hiyo kazi NI MIMI NA WEWE WALA SIO MTU MWINGINE!
Neno la Mungu linasema “Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.” Yoshua 1:6 SUV
Tusimfikirie mtu mwingine, ni mimi na wewe tunatakiwa KUWARITHISHA UFALME WA MUNGU WATU WA MUNGU AMBAO WAKO KATIKA HIMAYA YA SHETANI!
Ukiifanya hii kazi kubwa kwa UAMINIFU katika eneo lako, MUNGU LAZIMA AKUHESHIMISHE!
LAZIMA UTANG'AA KAMA NYOTA HATA KAMA HUJAFANYIWA MAOMBI WANAYOITAGA YA "kusafisha nyota"
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author