Text

Huwapa Nguvu Wazimiao

1 views 1 day ago

Isaya 40: 28 – 31
Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
Mbona umezimia moyo? 
Mbona umechoka? 
Mbona umekataa tamaa? Mbona umeacha kuomba? Mbona umeacha mifungo? Mbona umeacha kukesha? Mbona umeacha ibada?
Mbona umeacha kumtafuta Mungu? 
Je! Wewe hukujua?
Je! Hukusikia?
[Kwamba] Yeye Mungu [ni] wa milele, [Yeye ni] BWANA, [Ndiye] Muumba miisho ya dunia, [Yeye] hazimii, wala hachoki; [Na] akili zake hazichunguziki.
Anaweza kuwapa nguvu wazimiao, anaweza kukuongezea nguvu usiye na uwezo... 
Anawapa nguvu waliochoka na kukata tamaa, huwaondolewa uchovu na kuwafanya upya tena... Anaweza kukufanya upya tena
Isaya 40: 30 – 31 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Katika hali yoyote uliyo nayo, ukiamua kumngojea BWANA, utashangaa unapata nguvu mpya.
Utakwenda juu kama tai, tai huenda juu sana wakati wa dhoruba ambazo zinawakwamisha ndege wengine.
Ukijifunza KUMNGOJA BWANA, Wakati wengine wanachoka wewe hutachoka, utatiwa nguvu mpya. Hutachoka kuomba, kufunga, ibada, kumtafuta Mungu nk
Hutachoka kungojea majibu yako wakati ukiendelea Kumtumikia Mungu.
A -- Kumngojea Bwana ni kumtazamia Bwana. Ni kutarajia kwa shauku kutoka kwa Bwana.
Zaburi 42:2 "Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai..."
Ni kuwa na Shauku na Mungu na nguvu zake.
Unapoenda mbele za Mungu ukiwa na shauku na kiu ndani yako kutoka kwa Bwana, lazima atakuongezea nguvu, lazima utatiwa nguvu.
Nakukumbusha tena sifa za unayemwendea;
--Yeye ni Mungu wa milele, yaani habadiliki wala hana mipaka ya muda, maeneo wala vitu
--Yeye ni BWANA, ni mmiliki wa vyote
--Yeye ni Muumba miisho ya dunia
--Yeye hazimii, wala hachoki;
--Yeye, Mungu, akili zake hazichunguziki.
--Yeye Huwapa nguvu wazimiao
--Yeye humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
B -- Kumngojea BWANA ni kuamua KUAMBATANA NA BWANA
--Ukiamua kwa dhati kuambatana na BWANA, hata kama uko kwenye hali mbaya kiasi gani, lazima utatiwa nguvu, utaongezewa nguvu.
--Usiambatane na changamoto yako, chagua kuambatana na Bwana.
Chagua kuambatana na KILE NENO LAKE LINASEMA KUHUSU CHANGAMOTO YAKO.
Usiambatane na manung'uniko kinyume na Mungu, usikae upande wa kumlaumu Mungu, kaa upande wa Mungu.
Kaa upande wa kuuona wema wa Mungu katikati ya changamoto.
Zaburi 27:13 "Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA
Katika nchi ya walio hai."

Hata kama huelewi kinachoendelea, CHAGUA KUAMBATANA NA BWANA.
Elekeza jicho lako kwenye wema wa Mungu.
Tafuta cha kumshukuru Mungu na sio cha kumlaumu.
UKIFANYA HIVYO UTATIWA NGUVU.
Warumi 8:28 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Kumbuka:-
Unaye ambatana naye ni Mungu wa milele, Ni Bwana, Hachoki, hazimii, akili zake hazichunguziki, Huwapa nguvu wazimiao.
HATA na wewe atakutia nguvu.
Na Anasema Hivi;
Isaya 43:2 "Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza."
Zaburi 40:1 – 2 “Nalimngoja BWANA kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu. Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.”


#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
#Umebarikiwa
~Na Mwl. Francis M. Langula

+255754711247

 

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!