Text

Huwezi Kutoa Ambacho Hauna Sehemu ya II

1 views 1 day ago

Matendo ya Mitume3:6

"Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende."

Kitendo cha kusema "Mimi sina fedha wala dhahabu" Kinadhihirisha wazi kwamba Petro alikuwa anafahamu kwa hakika yeye ni nani na kile anacho katika Kristo!

He had enough knowledge of his identity and his ability in Christ!

Watu tulioookoka na kujazwa Roho Mtakatifu, mara nyingi tunachopungukiwa sio nguvu bali tunapungukiwa:- 

1) Ufahamu juu ya nguvu za Mungu na nini zinaweza kufanya toka ndani yetu

- Hatujui utendaji wa nguvu za Mungu, hatujui nini nguvu za Mungu zinaweza kufanya! Na mbaya zaidi, duinia ya sasa inajua zaidi kuhusu uchawi, nguvu za giza na mapepo kuliko nguvu za Mungu

- Kwa kiwango ambacho unaongeza ufahamu (kwa kusoma Neno, Vitabu na kusikiliza mafundisho) kwa nguvu za Mungu na utendaji wake; unajitengenezea mazingira sahihi ya kuanza kutembea katika nguvu za Mungu na kuziachilia kwa wengine.

2) Kutambua uwepo wa nguvu hizo za Mungu ndani yetu!

- Roho Mtakatifu (ambaye ndiye mtoa nguvu) anafanya kazi mahali ambapo anatambuliwa tu, Kama hatambuliwi atatulia tu bila kufanya chochote!

- Tukianza kuutambua uwepo wake kwenye maisha yetu tutatengeneza mazingira mazuri kuanza kufurahia nguvu zake maishani mwetu!

3) Jinsi ya kuziachilia nguvu hizo kutenda kazi kutuponya sisi na wale tunaowahudumia!

- Eneo lingine muhimu ni jinsi gani ya kuachilia nguvu hiyo ambayo iko ndani yetu na tunaitambua!

Ukiangalia alichoeleza Petro wakati anawaelezea watu kuhusu uponyaji wa kiwete, aliweka wazi kilichotokea hata kiwete huyo kutembea!

“Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.” Matendo ya Mitume 3:16 SUV

IMANI KATIKA JINA LA YESU...

Kwa hiyo, TULICHONACHO TUNAKIACHILIA KWA IMANI...

IMANI HII NI WAKATI WA MAOMBI AU WAKATI WA MATAMKO YA KILE TUNACHOTAKA KITOKEE!

"Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, *ila aamini kwamba hayo asemayo* yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu." Marko 11:23-24 SUV

KWA MAANDIKO HAYO NILIYONUKUU, tunaweza kuachilia nguvu ya Mungu ya kuhamisha milima kwa KWA IMANI KWA KUUAMBIA MLIMA, AU KWA KUSALI/KUOMBA KWA IMANI!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!