Text

Huwezi Kuwa na Imani Zaidi ya Unavyowaza

1 views 1 day ago

Warumi 14:1 -2
Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake. Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.
Kuna mambo muhimu sana nimeyaona katika andiko hili kuhusu IMANI na MAWAZO, ambayo napenda tushirikiane kujifunza. 
Neno hili linaongelea UDHAIFU WA IMANI ya mtu ambao unapelekea huyo mtu KUCHAGUA VYAKULA. 
Sasa, lengo langu si kuzungumzia kuhusu vyakula bali IMANI na MAWAZO. 
Anasema, DHAIFU WA IMANI asikuhukumiwe MAWAZO YAKE. 
Kwa kusema hivyo ni wazi kabisa kwamba IMANI INA MUUNGANIKO WA MOJA KWA MOJA NA MAWAZO.
Kwa hiyo, ukiyachunguza mawazo ya mtu ambaye ni dhaifu wa imani, utagundua mawazo yake pia ni dhaifu.
Huwezi kuwa na (kuishi) imani zaidi ya unavyowaza. 
Mtu ambaye hali nyama kwa sababu za kiimani, basi mawazo yake ndio yalianza kumwambia nyama ni mbaya kiimani ndipo yakasababisha imani yake juu ya nyama ikawa dhaifu na akaacha kula nyama.
Mtu AMBAYE IMANI YAKE KUHUSU AFYA NA UPONYAJI NI DHAIFU, MAWAZO YAKE PIA HAYAJAKAA SAWA, ANAWAZA UDHAIFU.
Naweza kusema kwamba, ULIMWENGU WA MAWAZO NI UPANDE MMOJA WAPO WA ULIMWENGU WA KIROHO 
Ninaamini hii ndio sababu Neno la Mungu linasema
2 Wakorintho 10:3 – 5 “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
Usipolishughulikia wazo linalopingana na Neno la Mungu, litatoa imani yako katika msingi sahihi ambao ni Neno la Mungu.
Marko 7:20 -23 “Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.
Usipoyashughulikia mawazo mabaya, yatakuangusha katika imani yako.
Ukitaka kushinda ulimwengu wa roho, hakikisha unashinda ULIMWENGU WA MAWAZO. 
Mathayo 16:23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Marko 8:33 Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Wakolosai 3: 1 – 3 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
WAZA (THINK) unachotaka kitokee --> AMINI (BELIEVE) unachotaka kitokee --> OMBA (PRAY) unachotaka kitokee --> TAMKA (CONFESS) unachotaka kitokee --> TENDA(ACT) unachotaka kitokee 

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

#Umebarikwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

+255754711247

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!