Imani Ishindayo (Nguvu ya Imani Inayoendesha Maisha)
Waebrania 10: 37 – 39
“Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana,Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.”
Roho Mtakatifu ameweka Neno hilo ndani yangu ninaamini litatuvusha mahali hasa kipindi hiki tulichonacho.
Ni wazi kabisa Yeye ajaye (Yesu) yu karibu kurudi kulichukua kanisa, ninaamini hili sio mjadala tena kwa dalili nyingi tunazoziona zikitokea duniani kwa ujumla.
Ni muhimu sana kufahamu katika siku hizi za mwisho, kitu kikubwa sana Shetani anakitafuta kwa mtu wa Mungu ni imani.
Ndio maana Yesu akauliza
Luka 18:8 "...walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?"
Na hii ndio sababu, kwenye mistari niliyonukuu ya Waebrania 10:37 anazungumzia kurudi kwa Yesu na msitari unaofuata 38 anazungumzia imani.... Anasema "mwenye haki wangu ataishi kwa IMANI"
Kwa hiyo kuna muunganiko wa siku za mwisho na imani... Kurudi kwa Yesu na imani ya watakatifu (kanisa)...
Kwa hiyo IMANI ndio itamuwezesha mwenye haki kuishi hasa zama hizi tulizo nazo.
Tunapaswa kufahamu kwamba, mambo mengi yanayoendelea humu duniani, ambayo tunaweza kudhani ni mambo ya kawaida ya dunia na kisayansi, yanaitafuta imani ya mtu wa Mungu kwa sababu IMANI ndio itaamua huyu mwenye haki aishi au la.
Nataka nieleze maana ya baadhi ya maneno toka kwenye andiko ili tuelewe vizuri:-
Waebrania 10:38 "mwenye haki wangu ATAISHI KWA IMANI"
--KUISHI:
-- Kuishi inayoongelewa hapa ni kuwa hai, kuwa na uzima lakini pia ni kuwa na afya.
-- Kuishi ni nguvu ndani ya mtu inayomfanya au kitu kuwa hai.
Maneno mengine yanayoelezea hilo neno "kuishi" ni "to live" yaani "kuwa hai" lakini pia ni "to quicken" yaani "kufanya hai au kutia uhai au uzima"
--KWA IMANI:
Hilo neno "KWA" Sio kiunganishi cha kawaida bali linamaana "ikiwa ni matokeo ya" au "zao la" au "tunda la" kingereza "product of" au "as a result of"
Neno hilo "kwa" halina tofauti na hili lililotumika kwenye Mathayo 1:5 "Salmoni akamzaa Boazi KWA Rahabu; Boazi akamzaa Obedi KWA Ruthu;..."
-- Yaani, Boazi ni matokeo ya (zao la) Salmoni na Rahabu, na Obedi ni matokeo (zao la/product of) Boazi na Ruthu...
Lengo langu ni kukuelewesha maana ya hilo neno "KWA IMANI"
--KUISHI KWA IMANI:
Kwa kuzingatia tafsiri nilizotoa hapo juu, utagundua kwamba:-
-- MAISHA ni matokeo ya KUWA NA IMANI...
-- Maisha ni zao la imani...
-- Imani ndio nguvu inayozalisha maisha au kuishi kwa mwenye haki...
-- Kuwa hai, kuwa na uzima ni matokeo ya imani...
-- Ukiondoa imani umeondoa maisha
Sasa tuingie ngani kidogo
--Nini maana ya Neno hili "Mwenye haki wangu ataishi kwa imani"?
1 - Pasipo imani hawezi kuishi (Atakufa)
-- Imani ndio uhai unaomuwezesha mwenye haki kuishi, kama hakuna imani huyu mtu amekufa hata kama anaishi.
-- Ukishakuwa mwenye haki, chochote ambacho unakiondolea imani unakiondolea kuishi. Kwa sababu kinachoamua mwenye haki aishi ni imani.
You start living when you have faith. Because faith is the substance for making life.
Hii ndio sababu Neno linasema katika Warumi 14:23 "...Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi."
-- Uzima wa mwenye haki hauwezi kuwa halisi mpaka awe na imani kuhusu uzima.
-- Kama huna imani wewe sio mzima hata kama hauumwi, kwa sababu Mwenye haki ANAISHI (ANAKUWA NA UZIMA) KWA IMANI. Kwa hiyo, Hata kama hauumwi, wewe sio mzima mpaka uwe na imani ya uzima.
-- Kama huna imani wewe ni mgonjwa tayari hata kama huumwi, sababu huna cha kukufanya kuwa mzima (kizalisha uzima). You don't have life (health) provider.
Faith is the substance to make a person live.
-- Lakini vile vile ugonjwa hauwezi kuishi (kuwa halishi) mpaka umeupatia nguvu ya kuishi kwa kupitia imani.
Namaanisha kwamba, wewe sio mgonjwa mpaka pale utakapoamini kuwa ni mgonjwa au unao ugonjwa, yaani unapoamini ndipo ugonjwa unaanza kuishi.
Namaanisha kwamba, IMANI yako kuhusu afya na uzima ndio itaamua UGONJWA usababishe madhara au la. Kwa sababu kinachoamua uzima wa mwenye haki sio kuwepo au kutokuwepo kwa ugonjwa bali ni IMANI.
Muda unapoamini kwamba ugonjwa fulani una nguvu kukukuzidi na utakuua muda huo huo ndipo unaupa huo ugonjwa nguvu ya kukumaliza na hata kukuua, kabla ya hapo hauna nguvu ya kukuua kwa sababu MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI YAKE.
-- Mtu yeyote anayekushawishi UDHARAU IMANI YAKO KWA MUNGU KUHUSU UZIMA NA AFYA, HUYO MTU ANATAKA UFE. Sababu mwenye haki ataishi kwa imani. No faith no life.
2. Imani ndio inavifanya vitu vya mwenye haki vianze kuishi.
-- Imani ndio UHAI wa mwenye haki, ndio inamfanya yeye aishi lakini pia ndio inaamua UHAI WA KILA ALICHO NACHO.
-- Kama wewe ni mwenye haki, ukiondoa imani kwenye chochote unachokifanya, umemuondoa Mungu au kwa lugha rahisi umeondoa maisha ya hicho unachofanya.
-- Afya ya mwenye haki ni kwa imani, biashara ni kwa imani, kazi ni kwa imani.
3. Imani ndio inakufanya uendelee kuwa mwenye haki
-- Dakika unapoacha imani kwa Mungu kupitia Yesu Kristo, ndio dakika hiyo unakuwa si mwenye haki tena sababu mwenye haki ataishi kwa imani.
-- The moment you cease believing in God through Jesus Christ, you end your righteousness in Christ
4. Imani Ndio inakufanya uendelee kuwa na haki ya Mungu juu ya jambo.
-- Kwenye kila jambo (Uzima, Afya, ulinzi, magonjwa, majanga ya dunia nk) kuna haki zako kama mwana wa Mungu. Kuna ahadi ya Mungu kwa ajili ya mwenye haki.
Namaanisha kwamba, kama mwana wa Mungu, unayo haki ya kuwa na AFYA KAMILIFU, KULINDWA NA MUNGU, KUEPUSHWA NA MAJANGA, KUPONYWA nk lakini haki hiyo utaifurahia KWA IMANI, kwa hiyo unapokosa imani juu ya haki yako automatically UNAIPOTEZA HAKI YAKO.
Namaanisha, As long as unaamini kuhusu afya, una haki ya kuishi afya, na utaishi afya nk.
5. Imani ndio inamtoa mwenye haki miongoni mwa wanaopatwa na UHARIBIFU na kumuingiza kwenye kundi la walioandikiwa KUISHI (WANAOOKOLEWA)
Waebrania 10:38 – 39 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani... Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na KUPOTEA[KUPATA UHARIBIFU], bali tumo miongoni mwa hao walio na IMANI YA KUTUOKOA roho zetu.”
Zaburi 91:7 “Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako.
Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume!
Hata hivyo hautakukaribia wewe.”
--HIYO IMANI NINAYOIONGELEA HAPA, YA KUMFANYA MWENYE HAKI KUISHI, NI NINI NA INAWEZA KUFANYA NINI?
Waebrania 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”
1 -- Imani hii ni uhakika ulio ndani ya moyo wa mtu unaozalishwa na NENO LA MUNGU.
-- Hii imani inayoendesha maisha ya mwenye haki si maneno matupu bali IMEJENGWA KWENYE NENO LA MUNGU.
-- Uhakika wa UZIMA na KUISHI unatokana na Neno la Mungu lililo imara linaloweza KUMJENGA MTU NA KUMRITHISHA UZIMA ANAOUAMINI.
Matendo ya Mitume 20:32 “Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa.”
Unatokana na Neno la Mungu linalodumu milele, lililo juu ya MAGONJWA YOTE, lililo juu ya wanadamu wote, lililo juu ya SAYANSI.
Mathayo 7: 24 – 25 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.”
2 --Imani hii ni uhakika unaozalishwa kwa KUMJUA MUNGU
Danieli 11:32b "...watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu."
Ayubu 22:21 “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.”
Warumi 8:28 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”
2 Timotheo 1:12 “...kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.”
3 --Imani hii ni Uhakika unaozalishwa na MAHUSIANO BINAFSI NA IMARA NA MUNGU
-- Ukosefu wa imani kwa Mungu ni ishara ya uhusiano dhaifu kwa mtu na Mungu.
Mtu ambaye mnahusiana naye vizuri utamuamini kwa kile anachosema.
Kuna vitu ambavyo baba yangu mzazi akiniambia wala siwezi kupata shida (ku-struggle) kumuamini, imani yangu itakuwa inatiririka (ina-flow) tu kwa kile amesema, hii ni kwa sababu ya mahusiano ambayo nimejenga naye yananifanya nisiwe na chembe ya shaka.
Kuna namna ukiwa na uhusiano mzuri na imara na Mungu, itakuzalishia IMANI KUBWA KWA MUNGU ambayo sio rahisi iyumbishwe na taarifa mbalimbali unazozisikia huku duniani.
Zaburi 91:14 “Kwa kuwa amekaza kuipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.”
Kwa kiwango ninachohusiana na Mungu kupitia Roho Mtakatifu anayekaa ndani yangu, kuna vitu siwezi kabisa kumtilia shaka (to doubt) Mungu.
Kwa kadiri unavyoimarisha mahusiano yako na Mungu kupitia Ushirika na Roho Mtakatifu, utashangaa kiwango cha imani yako kinapanda.
-- Dhamiria kuongeza maisha ya Maombi, mifungo, Neno, kusikiliza mafundisho, ibada nk utashangaa imani yako inaongezeka kiwango huwezi kumuonea Mungu shaka kwa kile amekuahidi.
--ONDOA IMANI YAKO KWENYE VITU VIFUATAVYO:-
1. ONDOA IMANI YAKO KWA MWANADAMU
Neno la Mungu linasema, Yeremia 17:5 "BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa KINGA yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA."
-- Mungu hataki Mwanadamu yeyote achukue nafasi ya Mungu kwenye maisha yako, ukimruhusu mwanadamu kufanya hivyo utashangaa Mungu mwenyewe anakupinga.
-- Kuwategemea wanadamu ni pamoja na kutegemea masuluhisho (solutions) ya wanadamu kuliko Mungu.
-- Kutumia suluhisho la kibinadamu sio tatizo lakini kutegemea suluhisho hilo kuwa ndio UZIMA WAKO, AFYA YAKO NA KINGA YAKO kiwango cha kumuweka Mungu pembeni au hata kama linaathiri IMANI YAKO KWA MUNGU NA NENO LAKE ni tatizo KUBWA sana.
Mithali 29:25 "Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama."
Kuwategemea wanadamu ni pamoja na kufanya maamuzi yenye msingi wa hofu na wasiwasi bila kujali NENO LA MUNGU LINASEMA NINI. BILA KUJALI ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO AMERIDHIA AU LA.
2. ONDOA IMANI YAKO KWENYE UJUZI NA AKILI ZAKO
-- Usijenge imani yako kwa akili zako, ujuzi wako, elimu na maarifa yako.
-- Mungu anaturuhusu kutumia elimu zetu na akili zetu lakini sio kuzitegemea akili zetu na ujuzi wetu, sio kuzitumainia akili zetu.
Mithali 3:5 “Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;”
-- Tumaini letu ni Bwana sio akili zetu. Tumaini letu ni Bwana sio madaktari . Tumaini letu ni Bwana sio SAYANSI. Tumaini letu ni Bwana sio hospitali. sio kadi za bima.
-- Akili yako inaweza kufika Mwisho na kushindwa, madaktari wanaweza kufika mwisho na kushindwa, sayansi inaweza kufika mwisho na kushindwa lakini BWANA AMBAYE NI TUMAINI LETU HAWEZI KUSHINDWA. Yeye yu juu ya yote hayo.
3. ONDOA IMANI YAKO KWENYE ULIVYO NAVYO
-- Uzima wako hauko kwenye vingi wa vitu ulivyo navyo, uzima wako uko kwenye imani yako kwa Mungu mkuu... Kwa sababu mwenye haki ataishi kwa imani.
-- Ukihamisha imani yako kutoka kwa Mungu, vitu vyote ulivyo navyo havina maana, kuna aina ya changamoto au magonjwa huwa haijali una vitu kiasi gani.
Luka 12:15 "...maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo."
1 Timotheo 6:17 “Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.”
--USIKUBALI KUPOTEZA IMANI
-- Kwa gharama yoyote ile usikubali kupoteza imani yako kwa Mungu na Neno lake.
-- Usikubali kupoteza imani yako kwa kazi nzuri ya Yesu msalabani iliyosababisha wokovu na UPONYAJI/AFYA YA KWELI.
-- Usikubali kupoteza imani kwa damu ya Yesu inayoweza kutuokoa na kutulinda na kila aina ya uharibifu wa adui na mauti.
-- Usikubali kupoteza imani kwa uaminifu wa Mungu kwetu ambao ni ngao na kikao chetu.
-- Usikubali kupoteza imani kwa Upendo wa Mungu na wema wake kwa maisha yetu, sababu hakutuweka duniani kwa hasara yake bali tupate wokovu.
-- Usikubali kupoteza imani ULINZI MKAMILIFU WA MUNGU KINYUME NA KILA HILA ZA SHETANI NA KINYUME NA KILA AINA YA MAAMBUKIZI YA MAGONJWA YA KUFISHA.
Kwa sababu Neno la Mungu linasema "Mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu."
--WEWE NI WA TOFAUTI SABABU YA IMANI YAKO
Mimi simo miongoni mwao wasitao na kupata uharibifu unaoikumba dunia, bali nimo miongoni mwa waliona imani ya KUWAOKOA NA KILA AINA YA UHARIBIFU UNAOIKUMBA DUNIA.
1 Yohana 5:4 “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.”
Mimi nimezaliwa na Mungu ninaushinda ulimwengu.
Yohana 3:31 "Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote ... Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote."
Mimi ni wa juu niko juu ya yote. Imani yangu katika Mungu inanipa kuishi juu ya yote. Juu ya magonjwa, juu ya dhambi, juu ya maambukizi, juu ya hofu. Juu ya dunia nk
Kila ambacho hakiwezi kumpata Yesu hakiwezi kunipata kwa sababu 1 Yohana 4:17b"...kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu."
Tunaishi duniani lakini sisi si wa dunia hii. Asili yetu si ya dunia hii. Asili yetu ni mbinguni na Neno linasema "...na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni." 1 Wakorintho 15:48b
TUNAYO IMANI ISHINDAYO... SISI NI WASHINDI... IMANI YETU NDIO USHINDI WETU... IMANI YETU KWA MUNGU NDIO MAISHA YETU... IMANI YETU NDIO NGUVU INAYOENDESHA MAISHA YETU HAPA DUNIANI.
WE HAVE THE WINNING FAITH.....WE ARE THE WINNERS
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
#Umebarikiwa
~Na Mwl. Francis M. Langula
+255754711247
Mwl. Francis Langula
Author