Imani yangu Katika Yesu Ndio Inaamua Kiwango Cha Afya ya Mwili Wangu
WAGALATIA 2:20
“Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.”
Nimeona kitu kwenye Neno hilo kwamba:-
"UHAI NILIONAO SASA KATIKA MWILI, NINAO KATIKA IMANI YA MWANA WA MUNGU..."
Kwa hiyo, "Uhai na Uzima wa Mwili wangu, ni matokeo ya Uhai na uzima wa IMANI YANGU KWA MWANA WA MUNGU"
Uhai wa IMANI YANGU KWA YESU, ndio UNAOTAKIWA KUAMUA UHAI NA UZIMA WA MWILI WANGU! VINGINEVYO ni kinyume na Neno la Mungu!
Kwa hiyo ninapoongeza UHAI WA IMANI YANGU KWA YESU, automatically nimeongeza UHAI NA UZIMA WA MWILI WANGU!
Uzima wa MWILI WANGU UNATEGEMEA NA UZIMA WA IMANI YANGU!
Kwa hiyo, UZIMA WA MWILI WANGU HAUTEGEMEI MAJIBU YA HOSPITALI HATA KIDOGO!
UZIMA WA MWILI WANGU HAUTEGEMEI MAJIBU YA VIPIMO NA DAKTARI YANASEMAJE!
UZIMA WA MWILI WANGU HAUTEGEMEI MAZINGIRA NINAYOISHI (sasa hii haimaanishi tuishi mazingira hatarishi kwa makusudi)
UZIMA NA UHAI WA MWILI WANGU HAUTEGEMEI HATA UFANYAJI KAZI BORA WA VIUNGO (MOYO, MAPAFU, FIGO, INI, KONGOSHO NK) MBALI MBALI VYA MWILI WANGU, BALI UNATEGEMEA UZIMA NA UHAI WA IMANI YANGU KATIKA KRISTO YESU!
Kwa hiyo, HATA KAMA VIUNGO VYA MWILI WANGU HAVIFANYI KAZI SAWA SAWA, KAMA NINAO UHAI KATIKA IMANI, ILE IMANI INA UWEZO WA KUVIHUISHA VIUNGO VYA MWILI VIKAWA SAWA!
Uzuri ni kwamba IMANI KATIKA KRISTO YESU, ina uwezo wa kuumba na kuhuisha hata vilivyokufa!
Neno la Mungu linasema “(Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)” 2 KOR. 5:7
Imani ndio inatakiwa kuamua afya yetu na uzima wa miili yetu na sio hali ya nje inayoonekana!
Ndio maana Neno la Mungu linasema:-
“Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu....”
Matendo ya Mitume 17:28
Kwa hiyo, KAMA IMANI YAKO KATIKA YESU KRISTO INA UZIMA NA UHAI, lakini AFYA YA MWILI WAKO HAIKO SAWA SAWA, UNAWEZA KUTUMIA NENO HILI NA UFAHAMU HUU KUAMURU UZIMA NA UZIMA WA IMANI YAKO UHAMIE KATIKA MWILI WAKO!
Maana yake ni kwamba, UNAWEZA UKASHUSHA (DOWNLOAD) UZIMA WA IMANI YAKO KUJA KWENYE MWILI!
You can synchronize YOUR BODY condition WITH YOUR FAITH IN CHRIST JESUS!
You can command your FAITH LIFE AND FITNESS to DUPLICATE TO YOUR BODY!
Lakini pia, KAMA UNAUMWA, UNAWEZA UKAAMUA KUTAFUTA MAHALI PA UTULIVU NA KULITAFAKARI NENO HILI NA KULIWAZA KWA UMAKINI HUKU UKILIONA NI LA KWAKO, HUKU UKIONA LINAKUPONYA, Na baada ya kulifikiri na kulitafakari kwa muda wa kutosha, jaribu kujicheki tena afya yako, utagundua umepona au umeanza kupata nafuu!
Amua kuliamini NENO LA MUNGU KULIKO KITU KINGINE CHOCHOTE, NA ULIKUBALI LIGEUZE AFYA YA MWILI WAKO!
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
Mwl. Francis Langula
Author