Text

Imekwisha, Msalabani ni Mahali Pa Mabadilishano (The Place For Exchange)- Adhabu na Msamaha

1 views 1 day ago

Yohana 19:30

"Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.”

Kama kuna jambo Wakristo tunapaswa kujivunia ni KAZI YA MSALABA ALIYOFANYA YESU!

Msalaba ndio ulimtia kiboko shetani ambacho hatakisahau!

Kila kilichompata Yesu msalabani ni kwa ajili yetu na ni ushindi kwetu!

Kwenye msalaba ndio mahali YALIFANYIKA MABADILISHANO (A PLACE FOR EXCHANGE)

Tulibadilishana na YESU, AKACHUKUA VYA KWETU NA KUTUPATIA VYA KWAKE!

Kwenye msalaba ndio mahali ULIFANYIKA MUAMALA (A PLACE FOR TRANSACTION), Yaani YESU ALITULIPIA KILE TULICHOKUWA TUNADAIWA!

Yesu ALIKUWA NA orodha YA VITU ambavyo alikuwa anavishughulikia ndio maana alipomaliza cha mwisho alisema IMEKWISHA, MAANA YAKE VYOTE NIMESHALIPIA HAKUNA DENI TENA!

Moja ya Vitu alilipia YESU na ambacho nataka tukiangalie leo KWENYE SEHEMU HII YA KWANZA ni, MSAMAHA WETU!

Unajua mtu anapokosea, kama hakuna MSAMAHA, BASI ITAKUWEPO ADHABU!

Kwa hiyo, SOTE TULISTAHILI ADHABU! Kwa sababu Neno linasema “kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;” Warumi 3:23 SUV

Kwa hiyo upande wetu KULIKUWA NA ADHABU, upande wa Yesu KULIKUWA NA MSAMAHA!

MSALABANI NDIO MAHALI PALIFANYIKA MABADILISHANO (EXCHANGE); YESU AKACHUKUA ADHABU YETU AKATUPATIA MSAMAHA WAKE!

MSALABANI NDIPO PALIFANYIKA MUAMALA (TRANSACTION); YAANI YESU ALIFANYA MALIPO YOTE YALIYOTAKIWA ILI SISI TUONDOLEWE ADHABU NA KUUPOKEA MSAMAHA!

Hakuna kitu Yesu alisaza kwa habari ya MSAMAHA WETU, kila kinachotakiwa kutolewa au kulipwa kililipwa na Yesu!

"kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.” Waebrania 9:28 SUV

"Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi." Waebrania10:12, 14, 18 SUV

️Hakuna tena toleo kwa ajili ya dhambi zetu, YESU ALISHALIPIA KILA KITU, kazi yetu NI KUAMINI NA KUPOKEA MSAMAHA!

Asije akakudanganya mtu, kwamba ILI USAMEHEWE DHAMBI HII, basi unapaswa kutoa sadaka fulani kufidia DHAMBI ULIYOFANYA; au ufanye malipizi fulani; YESU ALISHAJITOA SADAKA TAYARI!

ADHABU YA YESU ILINUNUA MSAMAHA WETU (JESUS' PUNISHMENT purchased our FORGIVENESS)

"Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote." Isaya 53:6 SUV

Maovu yetu yote yaliwekwa kwa Yesu! Kwa hiyo hatupaswi kubeba adhabu!

"akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;" Wakolosai 2:14 SUV

YESU ALISHAFUTA ILE HATI YA KUTUSHITAKI, HAIPO TENA, HATA UKIKOSEA LEO HATI ILISHAFUTWA, UNACHOPASWA NI KWENDA MBELE ZAKE KWA IMANI KUCHUKUA MSAMAHA!

ALICHOFANYA YESU KWA AJILI YA DHAMBI ZETU MSALABANI KINATUFANYA TUTAMANI KUISHI MAISHA MATAKATIFU, KWA SABABU GHARAMA ALIYOTOA KUTUPATIA MSAMAHA NA KUTUWEZESHA KUISHI MAISHA MATAKATIFU NI KUBWA MNO!

NDIO MAANA NENO LINASEMA: "Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu." Warumi 8:1 SUV

Ukweli ni kwamba, ukishaamua kuwa kwa Kristo, HAKUNA HUKUMU YA ADHABU JUU YAKO, YESU ALISHACHUKUA ADHABU KWA AJILI YAKO!

Kuamua kukaa na adhabu na hukumu moyoni baada ya kukosea, ni kutokujua alichofanya YESU MSALABANI!

Ingawa hii haitupatii tiketi ya kuishi maisha dhaifu na kucheza na dhambi, lakini kama umekosea au ulianguka, shetani asiendelee kukukandamiza hapo chini, INUKA, JIKUNG'UTE MAVUMBI YA HUKUMU NA KUJILAUMU, NENDA MBELE ZA MSALABA, MUACHIE YESU ADHABU YAKO NA HUKUMU, CHUKUA MSAMAHA WAKO, NA USITENDE DHAMBI TENA!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!