Itafika Wakati
Itafika wakati, sehemu pekee ambayo utakimbilia kupata msaada sio kule unapopapatia kipaumbele kikubwa na ambapo panakuchukulia muda mwingi/ wote. Sio kazi, biashara, sio marafiki, sio TV (filamu, soccer), sio simu (games, chatting, WhatsApp, TELEGRAM, Instagram, YouTube, Twitter nk)
Itafika wakati, Usingizi uliokuwa unafikiri ni muhimu sana kuliko kuamka kuomba na kumtafuta Mungu, hautakuwa na maana tena maana utalala mpaka hutatamani kuona kitanda.
Itafika wakati, hata watu ambao sasa unawafikiri ni wa muhimu sana kwako hutawaona, zile connection ulizofikiri zinakufaa sana hazitakuwa na maana, connection za madakatari Bingwa, za matajiri, watu maarufu, marafiki mlioshibana mnaokutana kila siku na kukaa wote. Kwa sababu wote wanaweza wasiwe na msaada kabisa.
Kuna wakati utafika, vitu unavyotumia pesa zako nyingi kwa hivyo, kiasi cha kuona huna pesa za kupeleka injili, sadaka za yatima na wahitaji, hata kuwakumbuka wazazi haiwezekani; utagundua havikuwa na maana kwa kiwango hicho.
Itafika wakati, mahusiano (boyfriend, girlfriend, mchumba, rafiki, mume, mke nk) uliyodhani ni ya muhimu sana KIASI UMEMUWEKA YESU PEMBENI (kiasi cha kuwa tayari kumuacha Yesu, au kumkosea Mungu) ili kumfurahisha huyo mtu, utagundua hayakuwa na muhimu KULIKO YESU WAKO.
Itafika wakati, watu ambao ulidhani hawana umuhimu sana na umekuwa hufikirii umuhimu wao kabisa kwenye maisha yako ndio watakuwa na muhimu kuliko kitu kingine chochote, wale ambao unawaona wa kawaida kabisa kiasi ambacho huna muda nao; ambao hata hujali sana wanachokifanya wala wanaishije, unawaona ni kama wanafanya hicho kwa sababu walikosa cha kufanya duniani, Watumishi wa Mungu ndio watakuwa na umuhimu mkubwa kwako, waombaji, watu wa kiroho ndio watakuwa muhimu kuliko wengine kwa sababu utagundua una changamoto/ tatizo ambalo hao tu ndio wanaweza kukusaidia.
Itafika wakati, vile vitu ambavyo ulikuwa huoni vya muhimu sana, wala huvipi kipaumbele eti sababu uko busy na kazi, biashara, huduma nk ndio vitakuwa vya muhimu sana. Umekuwa huyapi kipaumbele Maombi, Mifungo, kutenga muda kusoma Neno, Ibada, kukaa kwenye uwepo wa Mungu eti sababu uko busy sana. Unahisi kwamba hivyo vitu vinapaswa kuzingatiwa sana na watu ambao hawako busy sana katika kukimbizana na maisha.
Itafika wakati kinachokufanya busy hadi unamsahau Mungu na maelekezo yake hakitakuwa na maana tena. Kazi au bishara unayofanya imekukamata kuliko biashara kuu ya Yesu ya kuvuna nafsi.
Itafika wakati, Utagundua Maamuzi uliyofanya ukidhani ni ya maana sana kwa maisha, kumbe hayakuwa na maana kwa kiwango hicho. Na yale uliyoyapuuzia (kumpa Yesu maisha, kuishi maisha matakatifu na ya kujikana, kuzingatia maombi nk) ndio yalikuwa na maana kuliko yote na tulipaswa kuyapa kipaumbele.
Itafika wakati, UTAGUNDUA UAMUZI PEKEE WA MAANA KULIKO MAAMUZI YOTE ULIYOWAHI KUFANYA, ULIKUWA NI UAMUZI WA KUMPA YESU MAISHA NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU. Kwa sabau utagundua MAISHA YA DUNIANI YANAFIKA MWISHO, na mwisho wa kukimbizana kote na maisha, KUMPA YESU MAISHA NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU NDIO KUTAAMUA MAISHA YAKO YA MILELE WAKATI KILA KITU KIMEFIKIA MWISHO WAKE.
Wakati AFYA IMEFIKA MWISHO, UTAMUHITAJI YESU PEKEE. WAKATI PUMZI INAFIKA MWISHO UTAMUHITAJI YESU PEKEE. Yesu pekee ndiye atamaanisha maisha wakati huo. Kama ndiye atamaanisha maisha wakati huo, UWE NA UHAKIKA HATA SAAA NI YEYE PEKEE NDIYE ANAMAANISHA MAISHA. Yeye ni Alfa na Omega., Mwanzo wa vitu vyote ni yeye na mwisho kabisa wa mambo yote utamkuta Yeye.
KABLA YA WAKATI HUO KUFIKA, kaa chini jifikirie, jitathmini njia zako, fikiria upya vipaumbele vyako, zingatia moyoni mwako kama yule mwana mpotevu, fanya maamuzi sahihi.
Luka 15:17,20 “Alipozingatia moyoni mwake... Akaondoka, akaenda kwa babaye”
Zingatia moyoni na uondoke kurudi kwa Baba yako Mungu. AMUA KUREKEBISHA VIPAUMBELE VYAKO, usisubiri wakati mwingine. Saa ya wokovu (kuokoka, Marekebisho, matengenezo, kumrudia Mungu, kurudi kwenye maisha matakatifu, kurudi kwenye mahusiano mazuri, kurudi kwenye Neno, kurudia ibada nk) ni sasa.
Waebrania 3:15 “Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha”
Yohana 9:4 “Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.”
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
#Umebarikiwa
~Na Mwl. Francis M. Langula
+255754711247
Mwl. Francis Langula
Author