Je Moyo Wako Una Hali Gani? ni Kama Mwamba?
Mathayo. 13:20-21 SUV
“Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha; lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa.”
Yesu alitoa mfano wa mtu (mpanzi) aliyetoka kwenda kupanda mbegu, na akaeleza maeneo mnne (kwenye mwamba, kwenye miiba, kwenye njia, na kwenye udongo mzuri) ambayo mbegu zilianguka na matokeo ya kila eneo.
Ukifuatilia hayo maandiko kuanzia mstari wa kwanza wa Mathayo sura ya 13, utagundua huu ulikuwa upandaji wa kumwaga mbegu shambani, sasa wakati anazimwaga hizo mbegu, ndipo zikaangukia kwenye maeneo hayo manne niliyoyataja.
Leo, ndani yangu, Roho Mtakatifu ananiongoza tuangalie eneo moja kati ya hayo manne, ambalo ni MBEGU KWENYE MWAMBA au MIAMBA.
Nafikiri kundi kubwa la watoto wa Mungu mioyo yao iko kwenye kundi hili.
Kwa tafsiri ya moja kwa moja ya Yesu, Mbegu ni Neno la Mungu, na aina nne za udongo ni mioyo ya watu wa Mungu inayolipokea Neno.
Sasa tuangalie kwa undani kidogo MBEGU KWENYE MWAMBA.
Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha; lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa.
Mathayo 13:20-21
Andiko tulilonuku u linasema, mtu mwenye moyo wa aina hii,
1. ANALISIKIA NENO
2. ANALIPOKEA KWA FURAHA
3. HANA MIZIZI NDANI YAKE
4. NENO HUDUMU KWA MUDA MFUPI TU NDANI YAKE
5. CHANGAMOTO NA MAKWAZO HUUATHIRI MOYO WAKE (HUCHUKIZWA) HIVYO HULIZUIA LILE NENO LISIZAE
Hawa watu (wenye mioyo ya mwamba) ndio wale wanakuwa wanasisimka sana (very excited) kwa neno la Mungu likiwajia.
Kusikia kwao sio tatizo, hupenda ibada na mafundisho sana na sio kupenda tu bali WANAYAFURAHIA.
Baada ya Neno utasikia mtu anasema, Neno hili limeniponya, limenipa nguvu, limenivusha [sasa kusema hivi si tatizo, tatizo ni je kuna matokeo baada ya hapo?] na atatoka baada ya kusikiliza neno (kwenye ibada au mafundisho yoyote ya Neno la Mungu) AKIWA NA FURAHA SANA na anaweza hata kuidhihirisha furaha yake nje.
Ukweli ni kwamba hata watu wakimuangalia wanaona hata uso umechangamka baada ya ibada au mafundisho.
Lakini shida inakuja, KWA SABABU HANA MIZIZI YA NENO LA MUNGU NDANI YAKE, lile Neno linakosa mizizi ya kujishikiza ili kumletea matokeo.
Ili Neno la Mungu linalofundishwa au kuhubiriwa limzalie mtu matunda kirahisi, ni muhimu sana huyu mtu awe na MIZIZI KATIKA NENO LA MUNGU.
Watu wengi hawana mizizi kwenye Neno, yaani hulifahamu Neno kwa akili tu.
Neno la Mungu haliko mioyoni mwao.
Ninachomaanisha ni kwamba, ndani kabisa ya mioyo yao HAWAJASHAWISHIKA VYA KUTOSHA KUHUSU NGUVU YA NENO LA MUNGU KUBADILISHA HALI ZAO AU CHANGAMOTO ZAO.
Kwa mfano, watu wengi midomoni mwao husema, NAAMINI MUNGU ATANIVUSHA HAPA kwa sababu Neno lake linasema "Yote yawezekana kwake aaminiye", lakini ndani kabisa ya mioyo yao hawajashawishika kwa Neno hilo wanalolikiri (deep inside their hearts there is no conviction, beyond doubt, of what they confess).
Lile Neno halina mizizi, linatoka mdomoni tu. Na hii inasababishwa na kutokuwa na MUDA BINAFSI wa KULISOMA NENO NA KULITAFAKARI.
Kusoma Neno huifanya akili na ufahamu wa mtu kulishika au kulikariri andiko, unapoanza kulitafakari (kutulia na kulifikiria lile Neno kwa muda mrefu huku unamruhusu Roho Mtakatifu akufunulie siri lililobeba na kukuonyesha ukuu wake dhidi ya kila changamoto, huku pia ukitafuta agizo lililobebwa na hilo neno nk) ndipo lile andiko linaingia ndani yako, na likiwa ndani ya moyo sio andiko tena bali linakuwa ANDIKO LENYE PUMZI YA MUNGU (NENO), ndani ya moyo ndio linazalisha IMANI na ndiko LINAWEKA MIZIZI NDANI YAKO.
Kwa hiyo, mtu kabla hata ya kusikia Neno au mafundisho au mahubiri fulani, unakuta TAYARI NDANI YAKE ANAYO MIZIZI YA NENO LA MUNGU, NA IMANI IMESHAZALIWA.
Akija kusikia Neno, mahubiri, mafundisho basi ATAYAPOKEA KWA FURAHA, NA YATAKUTA MIZIZI YA NENO NDANI YAKE, lile Neno litat hibitika ndani ya huyu mtu, HATA AKIKUTANA NA CHANGAMOTO NA MAKWAZO BADO NENO NDANI YAKE LITAKUWA IMARA MPAKA LINAMZALIA MATUNDA.
“Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.” Waebrania 4:2
Mizizi ya Neno ndani ya mtu ndio huzalisha IMANI na hiyo imani, IKICHANGANYIKANA NA NENO (MAHUBIRI/MAFUNDISHO) ANALOSIKIA MTU NDIPO YALE MAHUBIRI YANAWEZA KUMFAA, KUMTOA MAHALI, KAMA NI YA BARAKA BASI KUSABABISHA BARAKA NK.
Na mchakato wa Imani, ni kama nilivyoeleza hapo juu. IMANI ni matokeo ya mchakato wa kukaa na Neno la Mungu na kulitafakari.
Nilirudi nyuma kidogo, Neno la Mungu linasema, "ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa"
Huyu mtu asiye na mizizi ndani, ni kwamba akimaliza kusikiliza NENO AU MAFUNDISHO, ANAKUWA NA FURAHA SANA (VERY EXCITED) lakini sasa baada ya muda, akikutana na dhiki au udhia (vinavyotumika pia kulijaribu lile neno ndani yake), anachukizwa na kupo teza Neno.
Yaani unakuta mtu anatoka kanisani au kusikiliza Neno ana furaha, akifika nyumbani (yaani yale mazingira aliyoyazoea) anakutana na dhiki (Changamoto alizoziacha kabla ya ku sikia Neno) au udhia (adui anamtengenezea mazingira ya makwazo) basi anashindwa kujizuia, changamoto zinamletea tena mawazo yasiyo na majibu na mazingira ya makwazo yanamkwaza anajikuta amekwazika, furaha ya Neno imepotea, amekasirika, au anakuwa depressed and stressed tena, na baada ya muda HALI YA KUKATA TAMAA IMEMRUDIA, NI KAMA HAJASIKIA YALE MAFUNDISHO (NENO), Neno limepotea. DHIKI NA UDHIA ZIMESHALIONDOA NENO AMBALO LINGEMVUSHA.
Na hii ndio imekuwa duara (circle) ambayo watu wengi wa Mungu wanazunguka.
Leo amekata tamaa kabisa, hajui cha kufanya, kesho Mungu anamtumia NENO LA KUMTOA HAPO, KWELI ANALIPOKEA KWA FURAHA KABISA na hata HUZUNI NA KUKATA TAMAA HUONDOKA NDANI YAKE, lakini tatizo HANA MIZIZI, kesho kutwa AMELIPOTEZA LILE NENO na amerudia hali yake ya mwanzo, siku inayofuata anapokea mafundsho kwa furaha tena na mzunguko unaendelea.
Na hiki ndicho kilikuwa k inawatokea wana wa Israeli Jangwani na kikawafanya watumie muda mrefu sana Jangwani. Walikuwa wanafurahia sana kile anachowatendea Mungu lakini baada ya muda WANAANZA TENA MANG'UNIKO KWA HUYO HUYO MUNGU ali yewatendea.
Mwisho Mungu akawaambia, "BWANA akanena, akaniambia, Mlivyouzunguka mlima huu vyatosha; geukeni upande wa kaskazini." Kumbukumbu la Torati 2:2-3
Ninaamini kwa ujumbe huu, Mungu anaona inatosha sasa kwa watu wake kuzunguka kwenye mlima, TUNAPASWA KUCHUKUA HATUA (KUGEUKA) KUZALISHA MIZIZI NDANI YETU NA KULIAMINI NENO LA MUNGU, BILA KUJALI CHANGAMOTO NA MAKWAZO, MPAKA LITUZALISHIE MATUNDA YALIYOKUSUDIWA.
Neno la Mungu ni Mbegu, KILA MBEGU HUWA IMEBEBA UKUU. Ndani ya mbegu ya ubuyu NDIO KUNA MTI MKUBWA WA MBUYU, ukiona mbegu ya mbuyu, huwezi kuamini kama MBUYU MKUBWA UKO NDANI YAKE, lakini ukiitengenezea mazingira ya kukua na kuweka mizizi chini vizuri, utashangaa kitakachotokea.
Mara nyingi Neno la Mungu halituzalishii matokeo kwa sababu ya MAZINGIRA YA MIOYO YETU KAMA NILIVYOELEZA.
KUANZIA LEO, ANZA KULIPA NENO THAMANI YAKE NA NAFASI YAKE, ANZA KULIPATIA MUDA MAKUSUDI KABISA, NAKUHAKIKISHIA, UTAONA MATOKEO.
Mungu halitumi Neno kutufurahisha tu, ANALITUMA KUGEUZA MAISHA YETU.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author