Je, Unajitambua Wewe ni Nani? Unatoa Sauti Gani?
Yohana 1:19 – 23
“Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawikutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.”
Mst.19 “Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?”
Wayahudi (Jamii aliyoishi au iliyomzunguka Yohana) walikuwa wakichanganyikiwa na kutojua Yohana ni Nani.
Baada ya kufuatilia anachofanya wakagundua Eneo lake (yaani anachofanya Yohana kinaangukia eneo gani).
Wakagundua, sio cha Kisiasa, hakihusiani na Kiserikali, sio cha Kibiashara.
Wakagundua kinahusiana na mambo ya Kiibada, mambo ya Kikuhani na Walawi.
Wakaamua kuchagua kundi la Watu sahihi kuwatuma kwa YOHANA kufuatilia.
Wakawatuma makuhani na walawi (They considered Experts kwenye Eneo la anachofanyaYohana).
Makuhani na Walawi ni watu walikuwa wakitumika moja kwa moja katika HEKALU.
Walikiwa ni Experts kwenye eneo alilotumika Yohana.
Mst. 20 “Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo.”
Inaonekana wazi Makuhani na walawi walikuwa wakifahamu fika ule ulikuwa ni MSIMU GANI (SEASON FOR THE COMING OF MESSIAH - CHRIST).
Kwa hiyo, kwa utendaji wa Yohana wakahisi anaweza kuwa ndiye Kristo. Lakini YOHANA ALIKUWA ANAJITAMBUA WAZI YEYE SIO KRISTO, hivyo akawajibu wazi kwamba Yeye sio Kristo.
Hii ni hatua ya kwanza muhimu sana, KUJITAMBUA WEWE SI NANI.
Kabla hujajitambua wewe NI NANI, ni muhimu sana kujitambua WEWE SI NANI.
Hii itakusaidia kutojihusisha na watu ambao hupaswi kujihusisha nao na kutochukua nafasi isiyo yako.
Yohana alijua wazi yeye sio Kristo.
Mtu Kutojua yeye si nani, kunaweza kumchanganya na kumfikisha mahali pa KUFANYA KILA KITU KIZURI AMBACHO MTU MWINGINE ANAKIFANYA NA KUJIKUTA KATIKA JANGA LA MASHINDANO BADALA YA KUISHI.
Ishara ya kutojua wewe si nani ni MAISHA YA KUIGA NA KUSHINDANA.
KAMA MIMI SI NABII, HATA KAMA HUDUMA YA NABII INAFANYA VIZURI NA KULETA MATOKEO MAKUBWA, SITAHANGAIKA KUPAMBANA NA NABII ILI NIWE KAMA YEYE KWA SABABU UKWELI NI KWAMBA MIMI SI KAMA YEYE NA WALA SI YEYE.
Hatuwezi kufanya kila kitu, tunapaswa kufanya kile ambacho tunapaswa kufanya.
Neno la Mungu linasema "SISI SIO WA DUNIA HII" japo wengi tunapambana kuwa kama wa dunia hii. Shida kubwa hatujui SISI SIO NANI.
Neno linasema katika Warumi 12:2 "WALA MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII.." lakini watu wa Mungu wengi tuko busy TUNAFUATISHA NAMNA YA DUNIA.
Yohana alikiri YEYE SIO KRISTO, YEYE NI MTU MWINGINE.
Mst. 21 “Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.”
Japo Yohana alijitambua YEYE SIO NANI, na aliwaambia Makuhani na Walawi mimi sio KRISTO, lakini hawakuridhika bado na JIBU LA YEYE SI NANI.
Wakaendelea kujaribu kubashiri yeye ni nani kwa namna ya maisha yake.Wakaendelea kujaribu kumu associate na watu wengine ambao sio yeye.
Yohana sio tu kwamba ALIJUA YEYE SI NANI BALI ALIKUWA ANAJUA KWA UNDANI YEYE SI NANI. Alikuwa na details za identity yake.
Dunia itaendelea kukupa shinikizo (pressure) kujaribu kukulazimishia KUWA KAMA WATU FULANI, wakati mwingine mazingira yatakulazimisha UJIUNGANISHE na KUJIFANANISHA NA WATU FULANI FULANI ambao wanachofanya si kibaya lakini SIO CHA KWAKO, NA WEWE SI WAO.
Wakati mwingine inaweza kusababisha uonekane mbaya na unajitenga.
Haitoshi kujijua WEWE SI NANI, UNAPASWA KUWA NA DETAILS ZA WEWE SI NANI NA KUKATAA KILA AMBACHO WEWE SICHO.
Yohana anawaambia, MIMI SI KRISTO, MIMI SI ELIYA, WALA MIMI SI NABII YULE.
Mst. 22 “Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako?”
Baada ya kuwahakikishia Yeye sio hao waliowataja au kumuunganisha naye, wakaja na maswali mawili mwengine Muhimu.
a) Wewe U nani? - Tukawaambie waliotutuma
b) Wanenaje juu ya nafsi yako?
Kujua wewe si Nani haitoshi kukutambulisha kwenye ulimwengu wako.
LAZIMA UJUE WEWE NI NANI.
LAZIMA PIA NAFSI YAKO ISHUHUDIE WEWE U NANI.
Dunia inahitaji kujua WEWE NI NANI, lakini pia inahitaji kujua UNAJIONAJE KWENYE NAFSI YAKO.
Swali la kwanza linataka kujua UNATAMBUA WEWE NI NANI, UNATAKIWA KUFANYA NINI?
Swali la pili, UMEWEKEZA NINI NDANI YAKO ili KUJITAMBULISHA KWENYE ULIMWENGU WAKO?
Kuna watu wanajua ni watu wakuu, wanatakiwa kufanya nini, lakini sababu hawajawekeza kwa usahihi kwenye nafsi zao, basi NDANI YA NAFSI ZAO WANAJIONA DUNI.
Wakijibu swali la kwanza WATAJIELEZA VIZURI, LAKINI WAKISEMA KWELI JUU YA NAFSI ZAO WANAJIONA SI KITU, WANAJIONA MAPANZI.
Dunia inahitaji majibu yote mawili yawe sahihi.
Ujue wewe ni nani, na NDANI ya NAFSI YAKO KUWE NA PICHA SAHIHI YA WEWE ULIVYO.
Hiki cha Nafsi ndicho kiliwakwamisha Wapelelezi 10 wa Israel kati ya 12 waliotumwa kuipeleleza nchi.
[22] "Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako?"
Jibu la kwanza la maisha yako SIO PESA. NI KUJITAMBUA ULICHONACHO NA KUJIONA SAWA SAWA.
Kujitambua kwetu NDIO JIBU DUNIA INAHITAJI. DUNIA HAIHITAJI PESA KUPATA MAJIBU, INAHITAJI WALIOJITAMBUA.
Dunia haihitaji warembo, haihitaji rangi fulani, au kabila fulani au warefu au wafupi. DUNIA INAHITAJI WALIOJITAMBUA.
WANAOJUA WAMEMBEBA YESU WANAOJUA NDANI YAO YESU NI JIBU NA WAKO TAYARI KULIPA GHARAMA NA KUTOA MAJIBU KWA DUNIA.
Mst. 23 “Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.
YOHANA ANAFUNUA YEYE NI NANI KWA UNDANI WA HALI YA JUU SANA KWA KUJIBU MASWALI YAFUATAYO.
Yohana wewe ni nani au nini!
1) Mimi ni SAUTI
Ziko sauti nyingi (za wanyama, ndege, watu nk), wewe ni sauti ya nini au ya aina gani?
2) Mimi ni SAUTI YA MTU
Hiyo sauti inafanya nini? Inapiga kelele tu)
3) Mimi ni INAYOLIA
Inalilia eneo gani? Unalia kila sehemu? Ujumbe wako ni kwa kila mtu, kila rika, kila mkoa, kila eneo? Unafanya kila biashara? Kila huduma? Kila kazi?
4) Eneo langu ni NYIKANI
Huko nyikani una Ujumbe gani? Sauti yako ina maana gani? Unajua lengo au Kusudi la sauti hiyo au unachokifanya? Unataka nini kupitia unachokifanya? Sauti yako inatutaka tufanye nini?
5) INYOOSHENI NJIA YA BWANA
Nini misingi yako? Umeibukia wapi wewe? Nini kina ku backup?
6) NENO LA MUNGU NDIO LIKO NYUMA YA NINACHOKIFANYA (Kama vile alivyonena NABII ISAYA)
Swali langu kwako JE UNAJITAMBUA??? WEWE NI NINI AU NI NANI? ENEO LAKO NI LIPI?
Yona 1:8 “Ndipo wakamwambia [Yona], Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani?”
UNAMUHITAJI YESU.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
#Umebarikiwa
~Na Mwl. Francis Langula
+255754711247
Mwl. Francis Langula
Author