Jenga Imani yako Katika Neno la Yesu, Ikuzalishie Matokeo Haraka
Mathayo 8:5-8, 13 SUV
“Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye. Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile.”
MAMBO YA KUJIFUNZA:
Huyu akida alipeleka ombi lake kwa Yesu, na Yesu alikuwa tayari kumtendea na akasema "Nitakuja, nimponye".
Kwa hiyo ni hakika kabisa Yesu alikuwa yuko tayari kumponya yule mtumishi wa yule akida; lakini inaonekana Yesu alikuwa ana safari anaelekea kwa hiyo akapanga akimaliza huko anakoenda ataenda kwa huyu akida pia!
Ukisoma maandiko utagundua kuwa Yesu alikuwa anaelekea kwa mama mkwe wake na Petro!
Sasa huyu Akida alipopeleka ombi lake kwa Yesu alipewa jibu zuri na sahihi kabisa kwamba "Nitakuja nimponye"! Kwetu wengi hili ni jibu zuri sana toka kwa Mungu!
Jibu la nitakuja nimponye LINADHIHIRISHA WAZI MAPENZI YA YESU KUMPONYA YULE MTUMISHI WA AKIDA!
Lakini kinachoshangaza ni kwamba Akida hakuridhika na jibu zuri namna hii!
Yesu alipokuwa duniani alikuwa ndani ya mwili kwa hiyo haikuwa inawezekana awepo sehemu mbili kwa wakati mmoja; kwa hiyo ilikuwa ni sahihi kabisa kwa Akida kusubiri Yesu amalize kumponya mama mkwe wa Petro (Mathayo 8:14-15) ndipo aende kumponya mtumishi wa Akida!
Inaonekana akida alikuwa amemfuatilia Yesu na kugundua kuwa Yesu alikuwa na mamlaka kwenye maneno yake maana ukisoma sura moja kabla ya hii utakutana na maneno yafuatayo:
“kwa maana [YESU] alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.” Mathayo 7:29 SUV
Kwa hiyo Akida alijua maneno ya Yesu yana amri ma mamlaka; akaunganisha na uzoefu wa kazi yake akagundua SINA HAJA YA KUSUBIRI MUDA WOTE HUO; nimuombe tu huyu Bwana ATAMKE NENO MOJA TU; na ndipo akamwambia Yesu:
"sema neno tu, na mtumishi wangu atapona."
Na ikawa vile vile kama Akida alivyoamini!
IMANI YA AKIDA KWA NENO LA YESU ILIFUPISHA MUDA WA KUPOKEA MAJIBU YAKE!
JIBU LA YESU LILIONYESHA MAPENZI YA YESU KUMPONYA MTUMISHI WA AKIDA, lakini IMANI YA AKIDA NDIO ILIAMUA MTUMISHI WAKE APONE MUDA GANI!
Imani katika Neno la Mungu inaweza ikaamua jambo ambalo ni mapenzi ya Mungu lifanyike muda gani!
Alichohitaji akida ni NENO LA YESU TU kuhusiana na ombi lake!
Kuna watu tumekuwa tunasema laiti Yesu angekuwepo hapa angeweza kufanya hiki na kile; tunasahau NENO LA YESU LILIFANYA KAZI HARAKA KULIKO HATA YESU MWENYEWE KWENDA KWA MGONJWA!
Ukiamua kuliamini NENO LA MUNGU kama huyu Akida lazima litakuzalishia matokeo yale yale!
Sisi tayari tunalo neno la MUNGU maishani mwetu, tunachohitaji kwa sasa ni Roho Mtakatifu kukukumbusha tu Neno sahihi kuhusiana na hali tunayoipitia, BASI.
Ukishalipata hilo, changanya na imani yako LIAMINI LIKUZALIE MATUNDA!
Usifikiri kwamba huyu Akida HAKUWA NA REPORT NYINGINE KUHUSIANA NA UGONJWA WA MTUMISHI WAKE!
Inawezekana kabisa alishaambiwa huyu kijana wako anakufa muda wowote, na inawezekana aliona kabisa nikingoja mpaka Yesu amalize shughuli zake ndio aje anaweza kuja sio kuponya bali kufufua!
Pamoja na Yote ALIAMUA KULIAMINI NENO LA YESU KWELI KWELI!
Yesu alipanga kumponya baadaye lakini IMANI YA AKIDA ALIYOIACHILIA KATIKA NENO LA YESU NDIO ILISABISHA MTUMISHI WAKE APONE MUDA ULE ULE!
HAKUNA ANAYEWEZA KULIAMINI NENO LA MUNGU KWA KIASI HICHO ASIONE MATOKEO!
“Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.” 2 Petro 1:19 SUV
IMANI KATIKA NENO LA MUNGU HUZALISHA MATOKEO HARAKA!
Kiasi cha IMANI ya muhusika katika NENO LA MUNGU ndio kitaamua muda wa MATOKEO KWA KILE ANACHOKIAMINI!
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author