Jinsi ya Kuiachilia Nguvu Iliyopo Katika Jina la Yesu
Matendo ya Mitume 3:16 SUV
“Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.”
MAMBO YA KUJIFUNZA:
Na kwa imani katika jina lake [Yesu], jina lake [Yesu] limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua;
Kilichomponya yule kiwete, sio kina Petro kutaja jina la Yesu tu, bali ni kitendo cha Petro kutaja jina la Yesu huku akiwa na IMANI katika Jina la Yesu!
Ndio maana Petro alianza kueleza kuwa "kwa IMANI KATIKA JINA LA YESU"
Kwa hiyo, kabla ya kulitaja jina la Yesu, walikuwa na IMANI KATIKA JINA LA YESU!
Neno la Mungu linasema, IMANI ni kuwa na UHAKIKA.
UHAKIKA ni matokeo ya KUJUA PASIPO SHAKA au KUELEWA PASIPO SHAKA!
Kwa hiyo, PETRO kabla ya kulitamka Jina la Yesu, alikuwa anajua pasipo shaka uwezo ulioko kwenye jina la Yesu!
Na kwa kuwa IMANI NI KITU HALISI, WALITAMBUA KABISA KWA HAKIKA WANAYO IMANI KATIKA JINA LA YESU ndio maana Neno linasema "Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho." Matendo ya Mitume 3:6a
- Petro hakuwa anabahatisha, bali, kama vile alivyokuwa na uhakika kwamba hana FEDHA wala DHAHABU mfukoni mwake, NDIVYO ALIKUWA NA UHAKIKA NDANI YAKE JUU YA UWEZO WA JINA LA YESU; ndio maana akasema
"Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende." Matendo ya Mitume 3:6
IMANI ndio ilimmilikisha Petro uwezo katika jina la Yesu na kwa IMANI WAKATI WA KULITAMKA ndio ilisababisha Jina la Yesu limsimamishe YULE KIWETE na kuwa mzima!
Kwa hiyo kinachosababisha uponyaji sio kutaja tu Jina la Yesu, bali ni pale yule anayetaja jina la Yesu ANAJUA UWEZO WA JINA LA YESU NA ANA IMANI JUU YA JINA HILO LAKINI PIA WAKATI ANALITAJA ANALITAJA KWA IMANI au akiamini litazalisha matokeo sahihi!
“Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.” Matendo ya Mitume 19:13-16 SUV
Hawa wana wa Skewa, sio kwamba walimtaja Yesu asiye wa kweli, maana walifanya reference sahihi kabisa ya Yesu, kwamba "kwa Yesu anayehubiriwa na Paulo" lakini haikuwaletea matokeo!
Sababu kubwa ni kwamba, walijaribu kutoa kitu hawana, kwa hiyo lilitoka jina Yesu midomoni mwao, lakini kwa sababu HAWAKUMJUA YESU, WALA NGUVU ILIYO KATIKA JINA LA YESU, KWA HIYO HAIKUWA KATIKA IMANI, KWA HIYO HAIKUWA NA NGUVU NA HAIKUWATISHA PEPO KABISA!
Watu wengi hatuoni matokeo tunapolitumia Jina la Yesu KWA SABABU hatujui uwezo uliopo kwenye jina kwa hiyo hatulitamki kwa IMANI!
Kabla ya kulitamka JINA LA YESU, TAFUTA KUFAHAMU KWA UNDANI UWEZO ULIOKO KATIKA JINA LA YESU, UTAFAKARI WEWE MWENYEWE UWEZO HUO mpaka uwe halisi ndani yako, yaani uwe na uhakika [IMANI] ndani yako juu ya JINA HILO, halafu sasa NDIPO ULITAMKE KWA IMANI KAMA PETRO, lazima utaanza kuona matokeo yake!
Kuna watu tunatumia jina la Yesu kama KIUNGANISHI TU CHA MAOMBI YETU AU KIBWAGIZO WAKATI TUNAOMBA NA TUNATEGEMEA KUONA MATOKEO!
Kuna watu tunatumia JINA LA YESU KAMA MSHANGAO TU AU KIASHIRIO CHA MSHITUKO NA TUNATAZAMIA KUONA JINA LIKIFANYA KAZI!
UKWELI NI KWAMBA, JINA LA YESU LINA NGUVU SANA ZAIDI YA KITU CHOCHOTE MBINGUNI, DUNIANI NA HATA CHINI YA NCHI
“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.” Wafilipi 2:9-11 SUV
Kama kungekuwa na HESHIMA NYINGINE KUBWA ZAIDI, MUNGU ANGEMPATIA YESU! Lakini MUNGU AKAONA HESHIMA KUBWA YA YESU AIWEKE KWENYE JINA LAKE, HALAFU AKATUPATIA SISI HILO JINA!
Hili JINA LA YESU, ni kuu kuliko chochote chenye jina MBINGUNI, chochote chenye jina DUNIANI na chochote chenye jina CHINI YA NCHI yaani mpaka kuzimu; vyote vinapaswa kupiga goti kwa jina la Yesu!
Ili Kufanyia kazi hiki tulichojifunza, Kama unaumwa au una mgonjwa, tafakari ujumbe huu kwa makini mpaka uelewe kikamilifu nguvu ya JINA LA YESU; halafu JIOMBEE AU MUOMBEE MGONJWA HUKU UKITAMKA JINA LA YESU KWA IMANI NA UFAHAMU HUU JUU YA NGUVU ILIYOPO KWENYE JINA LA YESU! Utanipigia kunipa USHUHUDA!
Najisikia niko full charged kwa kutafakari ujumbe huu, kama una mgonjwa niunganishe naye, JINA LA YESU BADO LINA NGUVU ILEILE ILIYOMUINUA KIWETE MLANGONI PALE, hata sasa linaweza kuponya!
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author