Text

Kiashirio Cha Kiroho Kutusaidia Katika Mahusiano (Spiritual Alert To Help Us In Relationships)

1 views 1 day ago

Waebrania 10:38

"Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye."

Kuna kitu kikubwa sana Roho Mtakatifu ananifundisha hapa kuhusu MAHUSIANO (KATI YETU NA MUNGU NA KATI YETU NA WATU) na ninaamini kitatusaidia sote.

Kuna maneno matatu ya msingi nitayafafanua kisha nitaleta kile ambacho nakiona kuhusu MAHUSIANO.

Maneno hayo matatu tutayaangalia kwa mtazamo wa MAHUSIANO.

Waebrania 10:38 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.”

1) KUISHI KWA IMANI (FAITH)

Imani iliyozunguziwa hapa ni ushawishi wa ndani anaokuwa nao mtu kuhusiana na Mungu na uwezo alionao (inner conviction about God and His ability), hii ikihusisha kumuamini Mungu kwa hali ya juu ya kimauhusiano (TRUST) kwamba yeye ndiye mpaji (provider) na ni mwaminifu ambaye tunaweza kumtegemea.

2) KUSITA-SITA (DRAW BACK)

Ni kuanza kuwa au kuwa na mashaka na Mungu, kuacha kumuamini kama Yeye, kwa kiwango mnachohusiana naye kwa Imani na kwa uwezo alio nao, anaweza kukupatia au kukufanyia unachohitaji.

Ni kuanza kutilia shaka MAHUSIANO yako na Mungu, au kiwango chenu cha kushibana katika hayo mahusiano.

Kusitasita kimsingi, sio mashaka juu ya uwezo alionao Mungu, bali ni mashaka kama kweli kiwango cha uhusiano wako na Mungu kinaweza kukuhakikishia kupata msaada unaohitaji kutoka kwake.

Kusitasita huku kunasababishwa hasa na vitu vikubwa viwili, moja ni mazingira ya changamoto inayomkabili mtu na mbili ni kiwango cha kumjua Mungu (na Neno lake) na uaminifu wake, linapokuja swala la utatuzi wa changamoto za aina hiyo.

Lakini, Kimsingi, tatizo mama hasa la kusitasita sio mazingira bali ni KIWANGO CHA KUMJUA MUNGU NA UAMINIFU WAKE.

Kumjua Mungu na Neno lake ndio kunazalisha UHUSIANO IMARA NA MUNGU AMBAO UNAMUHAKIKISHIA MTU NDANI YAKE KUHUSU UAMINIFU WA MUNGU KATIKA KUSHUGHULIKA NA CHANGAMOTO ZAKE, NA MATOKEO YAKE HALI YA KUSITASITA INAKUFA YENYEWE.

Labda nieleze zaidi hapa, kimsingi mtu anapokuwa kwenye changamoto, kuna nguvu mbili zinashindana (two forces at work), NGUVU YA NJE (External Force) inayomuonyesha mtu tatizo na kulikuza na NGUVU YA NDANI (internal Force) inayomuonyesha mtu ukuu na UAMINIFU wa Mungu katika kushughulika na changamoto.  KUMJUA MUNGU NA NENO LAKE itasababisha NGUVU YA NDANI kuwa imara na kuweza kuimudu nguvu ya nje. Yaani muhusika ATAKUWA NA UFAHAMU ZAIDI KUHUSU UWEZO NA UAMINIFU WA MUNGU (AWARENESS OF GOD'S ABILITY AND FAITHFULNESS) KATIKA KULISHUGHULIKIA HILO NA HII AUTOMATICALLY ITAUA HALI YA KUSITASITA NA KUZALISHA UTULIVU.

Neno la Mungu linaweka wazi (katika kitabu cha Waebrania) kwamba, IMANI SIKU ZOTE HUAMBATANA NA UTULIVU WA NDANI, kwa lugha nyingine imeitwa RAHA (kingereza ni REST), kwa hiyo ukiona hauna utulivu wa ndani (ambao mwisho wake utasababisha kusitasita) ni ishara ya wazi kwamba IMANI INAPATA SHIDA.

“Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile;” Waebrania 4:3a SUV

For we who believe [that is, we who personally trust and confidently rely on God] enter that rest [so we have His inner peace now because we are confident in our salvation, and assured of His power] HEBREWS 4:3a AMP

Kwa hiyo, IMANI, ambayo kwenye maandiko hayo ya Waebrania imetajwa kama kiwango cha juu cha kuamini na kuwa na ujasiri kwa Mungu, inatuingiza kwenye CHUMBA CHA UTULIVU AU RAHA (Amani ya Mungu ndani yetu inayosababishwa na ujasiri tulionao kwa nguvu za Mungu na uhusiano mzuri tulionao na Yeye).

3) Roho yangu (ya Mungu) haina furaha.

Eneo la tatu kwenye andiko hilo ambalo nataka tuliangalie ni NAMNA ROHO YA MUNGU anavyoitikia KUHUSIANA NA HALI YA KUSITASITA TUNAYOKUWA NAYO.

Katika eneo hili, Sehemu ya kwanza tutaangalia UHUSIANO WA MTU NA MUNGU na sehemu ya Pili ni UHUSIANO WA MTU NA MTU au WATU.

Neno la Mungu linasema, tunaposita sita Roho ya Mungu inakosa furaha nasi. Yaani Roho ya Mungu au Roho Mtakatifu anahuzunika.

Hii inaonyesha wazi kwamba KUNA UHUSIANO WA MOJA KWA MOJA KATI YA IMANI ZETU NA ROHO YA MUNGU (AU NA MUNGU MWENYEWE).

Yaani, tukisita sita, Mungu anakosa furaha, tukiwa na IMANI, Mungu anafurahi.

Kuna namna MAHUSIANO YETU NA MUNGU YANAATHIRIKA TUNAPOSITASITA.

Neno la Mungu linasema, "Furaha ya Bwana ndio nguvu zetu" Nehemia 8:10b

kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.

Sisi tukiwa katika IMANI, Mungu anafurahi, Mungu akifurahi, TUNAONGEZEWA NGUVU, yaani ANAWEKEZA ZAIDI KWETU (HE INVESTS MORE IN US).

Tunapokuwa na IMANI, inatufanya kufuzu MUNGU KUWEKEZA ZAIDI NGUVU ZAKE KATIKA MAISHA YETU.

Tukisitasita, Roho ya Mungu haina furaha nasi, Mungu asipofurahi, TUNAKUWA DHAIFU. MUNGU ANASITISHA AU ANAPUNGUZA KUWEKEZA KATIKA MAISHA YETU.

Tunapositasita, mtiririko (flow) wa Nguvu za Mungu kutujia unakata, na tunakuwa dhaifu kiroho (na hata kimwili), kwa hiyo tunakuwa katika hatari ya kushindwa na changamoto zinazotukabili.

Mtazamo wa pili ambao Roho Mtakatifu alikuwa akinitazamisha kwenye sehemu ya andiko hilo isemayo "Roho yangu haina furaha naye", unahusiana na MAHUSIANO KATI YETU NA WATU, na mahususi ni Kuzitambua roho (discernment of the spirits) linapokuja swala la kuhusiana na watu ili kutusaidia kufanya maamuzi mbalimbali.

Unajua, uhusiano wetu na watu, mara nyingi (kama si mara zote) unahusisha roho zetu na nafsi zetu pia. Na tukiwa makini kufuatilia nini kinaendelea kwenye NAFSI NA ROHO zetu, tunaweza kujua hali (status) ya mahusiano yetu na watu.

Kwenye maandiko hayo tunaona Mungu kwa upande mmoja na Mwanadamu kwa upande wa pili, ambao wanahusiana (huu ni uhusiano wa kiroho), pia tunaona jambo fulani (kusitasita) linatokea upande wa mwanadamu (ambaye ni roho anayeishi katika mwili) ambalo, taarifa inaenda moja kwa moja kwenye Roho ya Mungu na KUZALISHA HALI YA KUKOSA FURAHA na huyo mwanadamu.

Kwa hiyo Mungu akiona hana furaha na Mtu, ni ishara ya wazi ndani yake kwamba IMANI na huyo mtu (trust between the two) imepata shida.

Tukumbuke sisi ni VIUMBE WA KIROHO (na tumeubwa kwa mfano na sura ya Mungu katika roho zetu), japo tunaishi ndani ya miili. Kwa hiyo, tukiwa makini, roho zetu zinaweza kabisa kutupatia viashirio ambavyo vitatusaidia kujua HALI (STATUS) YA MAHUSIANO YETU NA WATU MBALI MBALI HATA KABLA HALI YA NJE HAIJAONYESHA.

Ninachomaanisha ni kwamba, unapohusiana na mtu au watu, SIKILIZA HALI YA ROHO YAKO IKOJE. Ukiona Roho yako haina furaha na mtu, ujue hiyo ni ishara kwamba inawezekana kuna kitu fulani upande wa pili kinachohusiana na IMANI AU UAMINIFU (TRUST) katika uhusiano huo, hakiko sawa.

Uwezo huu wa kutambua hali ya mahusiano unaweza KUTUSAIDIA SANA KUTOINGIA AU KUTUTOA KWENYE MAHUSIANO YASIYO SAHIHI.

Lakini pia hii itatusaidia KUWA MAKINI ZAIDI TUNAVYOHUSIANA.

KIMSINGI, TUKIFUATILIA KWA MAKINI KIASHIRIA HIKI, KINAWEZA KUTUSAIDIA KUTUEPUSHA HATA NA HASARA MBALI MBALI ZINAZOTOKANA NA KUSHIRIKIANA KIBIASHARA NA WATU WASIO SAHIHI.

Kwenye sehemu ya kwanza ya uhusiano wa Mungu na sisi tumeona, Roho ya Mungu ikikosa furaha, Mungu anakata au anapunguza mtiririko (flow) wa nguvu zake kuelekea kwa mtu husika. Hii inatufundisha kwamba, KUNA JAMBO TUNAPASWA KUFANYA PIA MARA TUNAPOONA KIASHIRIA HIKI NDANI YETU.

Unapoona unapata shida hii, uwe makini na KIWANGO CHA NGUVU UNACHOWEKEZA (INVESTMENT) KWA MTU HUYO AU BIASHARA HIYO.

USIWEKEZE NGUVU NYINGI (AU USIWEKEZE KABISA) KWENYE BIASHARA AMBAYO ROHO YAKO HAINA FURAHA NAYO.

Kuwa makini na Mahusiano (ya kawaida au ya kibiashara) na mtu au watu ambao ROHO YAKO HAINA FURAHA NAO.

Ukiona Roho yako Haina furaha na Mtu mnayetaka kushirikiana naye jambo fulani, USIPUUZIE, FUATILIA KWA MAKINI HAYO NILIYOELEZEA NA UCHUKUE HATUA SAHIHI.

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!