Text

Kinga ya Mungu, na Uponyaji Kwa Magonjwa Yote Mabaya.

1 views 1 day ago

Kumbukumbu la Torati 7:15

“Na BWANA atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao.”

Kuna vitu viwili Roho Mtakatifu amenionyesha hapo kwenye hilo andiko nililonukuu naomba kukushirikisha.

1. BWANA atakuondolea ugonjwa wote

2.  Hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo.

Nitaanza na hili la pili, kisha nitamalizia la kwanza.

2. Hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo.

Zama hizi tunazoishi, kumekuwa na hofu nyingi sana imetanda kwa watu hata waliookoka kwa sababu ya mlipuko wa magonjwa mabaya yanayowapata watu bila kujali rika/umri na wakati mwingine bila hata kuwa na sababu ya msingi sana za kidaktari.

Baada ya kuliona Neno hili, nimeongezewa ujasiri na imani juu ya ulinzi wa Mungu kwa watu wake dhidi ya magonjwa ambayo yanaogopesha watu katika dunia ya sasa.

Neno la Mungu linasema, Mungu hatatia/hataruhusu MARADHI MABAYA YOYOTE UYAJUAYO YAKUPATE.

Baada ya kusoma andiko hilo, nikaona msisitizo ndani yangu wa "MARADHI MABAYA YOYOTE UYAJUAYO".

Nikaanza kuwaza ni maradhi/magonjwa mabaya mangapi ninayajua au nimewahi kuyasikia? KWA HIYO YOTE HAYO MUNGU HATARUHUSU YANIPATE.

NIKISHAUSIKIA TU UGONJWA MBAYA, KWA ANDIKO HILI HUO UGONJWA HAURUHUSIWI KUNIPATA.

Nikaanza kuyawaza magonjwa mabaya ninayojua au kuyasikia... Nikagundua, Cancer hairuhusiwi kunipata, UKIMWI hauruhusiwi, KIHARUSI, KISUKARI, PRESSURE, MAGONJWA YA FIGO, ULCERS, EBOL     A, KIPINDUPINDU, NA MENGINE MENGI.

Yani hata ukiibuka ugonjwa mpya, kama ni mbaya hauruhusiwi kunipata.

Hili NENO NIMELIONA, NA KWA KUWA NIMELIONA NI LANGU MIMI NA WATOTO WANGU.

Kila kilichofunuliwa kwetu ni mali yetu....

“Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele,” Kumbukumbu la Torati 29:29

Hili Roho Mtakatifu amelifunua basi ni la kwetu sisi na watoto wetu milele. Ulinzi huu dhidi ya magonjwa ya kutisha ni wetu sisi na watoto wetu milele.

Neno linasema "Maradhi mabaya niyajuayo"

Mungu hakutaja ugonjwa hapo kwenye andiko hili, ametuachia sisi kugundua ugonjwa mbaya na kuuweka kwenye list.

Kwa hiyo kila ugonjwa ambao mimi nitauona mbaya, au nitau categorize kama ugonjwa mbaya, basi hauruhusiwi kunipata.

Uzuri ni kwamba, kwangu mimi sioni ugonjwa mzuri, yote ni mabaya kwa hiyo hayaruhusiwi.

NINALIPENDA SANA NENO LA MUNGU, UKILIAMINI LINAFANYIKA HALISI.

Ukifikiria au kukumbuka ugonjwa wowote mbaya (na hakuna ugonjwa mzuri) basi huo ugonjwa hairuhusiwi kukupata wewe.

Sehemu hii ya pili ya andiko hilo, inatuhakikishia KINGA DHIDI YA MAGONJWA YOTE MABAYA.

Uzuri wa Neno la Mungu linakinga na pia LINAPONYA.

Sehemu ya kwanza ya andiko hili inadhihirisha utayari wa Mungu KUTUONDOLEA KILA AINA YA UGONJWA.

1. BWANA atakuondolea ugonjwa wote.

Kwa hiyo, kama wewe ni mgonjwa, MUNGU YUKO TAYARI KUKUONDOLEA UGONJWA WOTE.

Uzuri pia hata hapa hakutaja kabisa jina la ugonjwa, maana yake yuko tayari kukuondolea ugonjwa wowote.

Kwa hiyo, kama wewe hauumwi, Neno hili linakuhakikishia kinga, kama unaumwa Mungu yuko tayari kukuondolea ugonjwa wote.

Tukifika mahali tukaliamini Neno la Mungu kuliko taarifa ya Madaktari, tutaanza kuona matokeo. Tukaliamini Neno la Mungu KULIKO HATA HISIA ZETU ZA MAUMIVU, LAZIMA LITAZALISHA MATOKEO.

Tulichukue Neno kama linavyosema, bila kujali hali ya nje ikoje. NENO LA MUNGU LINA NGUVU NDANI YAKE YA KUGEUZA HALI YOYOTE ILE, UKILIAMINI HALIWEZI KUKUANGUSHA.

MIMI NINAAMINI NENO HILI KWENYE MAISHA YANGU, NAAMINI MARADHI YOYOTE MABAYA HAYATANIPATA.

TUUNGANE PAMOJA KUMWAMINI MUNGU, WAKATI DUNIA INAISHI KWA HOFU YA MAGONJWA MABAYA, TUISHI KWA IMANI KWA NENO NA AHADI ZA MUNGU KUTUKINGA NA MARADHI YOTE MABAYA.

YAORODHESHE MAGONJWA YOTE MABAYA UNAYOYAJUA, KWA NENO HILI, HAYARUHUSIWI KUKUPATA, NA KAMA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE MARADHI HAYO YAMEKUPATA, KWA NENO HILI HILI, MUNGU YUKO TAYARI KUYAONDOA

“Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.” Kutoka 23:25

Mungu akibariki chakula na maji maana yake, huwezi pata MAAMBUKIZI YOYOTE KUPITIA KULA WALA KUNYWA, LAKINI PIA AMESEMA ATAONDOA UGONJWA KAMA UNAO.

Ninalipenda sana Neno la Mungu, linanipa pa kushika, linanipa msimamo wa uhakika.

"MANENO HAYA NIMEYAONA NA NI HAKI YANGU MIMI NA WATOTO WANGU HATA MILELE."

NA KILA ALIYEELEWA NA KUAMINI ASEME HIVYO, NAYO YATAKUWA HALISI KWAKE KWA JINA KUU LA YESU.

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!