Text

Kosa Moja Haliadhibiwi Mara Mbili

1 views 1 day ago

Kisheria, kosa moja halitakiwi kuadhibiwa mara mbili, hata katika ulimwengu wa roho, kosa moja halipaswi kuadhibiwa mara mbili.

TAYARI YESU AMEKWISHA KUADHIBIWA KWA AJILI YA MAGONJWA YETU YOTE.

“Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” Isaya 53:5

Usikubali kuishi katika ugonjwa [adhabu] wakati Yesu tayari alikwisha kuadhibiwa kwa niaba yako; ndio maana Neno la Mungu linasema "Na kwa kupigwa [au kuadhibiwa] kwake sisi tumepona"

Kwa maneno hayo ni kwamba kila ugonjwa maishani mwako hauna uhalali wa kukaa. Kukaa kwake kwenye mwili wako ni kinyume cha sheria, maana tayari Yesu alikwisha kuadhibiwa kwa kosa hilo.

Kwa hiyo, kwa ufahamu huu wala huitaji kutumia nguvu nyingi, kwa imani unong'oneze hata kwa sauti ndogo huo ugonjwa uuambie kuwa "nimegundua haki yangu kwamba sitakiwi kuwa mgonjwa na hauna haki wala uhalali wa kuendelea kukaa ndani yangu kwa sababu KWA KUPIGWA KWAKE YESU NIMEPONA"

Ugojwa huo utasikia na leo utakuwa mwisho wake Kwa Jina la Yesu.

Kosa moja haliadhibiwi mara mbili

Ubarikiwe

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!