Kristo Ndani yangu, Tumaini la Utukufu
Wakolosai 1:27
“ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu”
Katika tafakari ya leo, ningependa tuangalie Siri ambayo imefunuliwa katika andiko hilo nililonukuhu, nayo ni "KRISTO NDANI YENU, TUMAINI LA UTUKUFU"
Neno hili Mungu aliliweka ndani yangu wakati kijana wangu mdogo anaumwa, na ninaamini ndio lilikuwa limebeba uponyaji au uzima wake.
Nitakachokifundisha hapa ndicho nilikiamini na kushawishika masaa mengi kabla sijamuwekea mikono.
Tafsiri ya kingereza ya neno hilo inasema "Christ in you, the hope of Glory"
Neno la Mungu linasema hii ni siri kubwa sana iliyofunuliwa kwetu, yaani, KIRISTO AKIWA NDANI YETU, LIPO TUMAINI LA UTUKUFU.
Hii ikiwa na maana kwamba, KRISTO AKIWA NDANI YETU, TUNAUTAZAMIA (EXPECTATION) UTUKUFU (UZIMA WA KRISTO) NDANI YETU, au TUNAO UZIMA WA MUNGU NDANI YETU.
Zingatia haya maneno Neno "KRISTO NDANI YENU" na "TUMAINI LA UTUKUFU"
Ili tuelewe vizuri maneno hayo, tuangalie maana mojawapo ya Neno utukufu.
Utukufu ni uwepo wa Mungu uliodhihirika wazi.
Mfano mzuri wa utukufu wa Mungu ni Wakati Yesu anaenda kumfufua Lazaro! Alipokutana na Martha alimwambia "UKIAMINI UTAUONA UTUKUFU WA BWANA" na aliposema "UTUKUFU WA BWANA" alimaanisha UFUFUO WA LAZARO, ALIMAANISHA UZIMA WA LAZARO.
Yohana 11:40 “Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”
Kwa hiyo, KRISTO NDANI YETU, TUMAINI LA UTUKUFU maana yake ni kwama KRISTO AKIWA NDANI YETU, TUNALO TUMAINI (TARAJIO) LA UZIMA, TUNALO TARAJIO LA UFUFUO AU UTUKUFU WA KRISTO.
KRISTO AKIWA NDANI YETU, TUNAO UZIMA NDANI YETU, TUNAO UFUFUO NDANI YETU, UPONYAJI NDANI YETU.
Anaposema KRISTO NDANI YETU hamaanishi Kristo ndani ya roho zetu pekee, anamaanisha KRISTO NDANI YA ROHO, NAFSI NA MIILI YETU.
KRITO NDANI YANGU MAANA YAKE KRISTO ANAWEZA KUKAA KILA ENEO LA MWILI WANGU.
Na kwa sababu KRISTO NDANI YANGU, NI TUMAINI LA UTUKUFU (UZIMA, UPONYAJI, AFYA, UFUFUO) MAANA YAKE KILA ANAPOKAA KUNA UZIMA, UPONYAJI, UFUFUO, AFYA NK.
Kristo kwenye MOYO WANGU, UZIMA KWENYE MOYO WANGU...
Kristo kwenye MAPAFU YANGU, UZIMA KWENYE MAPAFU YANGU...
Kristo kwenye MIGUU YANGU, UZIMA KWENYE MIGUU YANGU...
Kristo kwenye MACHO YANGU, UZIMA KWENYE MACHO YANGU...
KWA LUGHA RAHISI NI KWAMBA, KUWEPO KWA YESU NDANI YETU NI KUWEPO KWA UZIMA NDANI YETU.
Kama unaumwa eneo lolote la Mwili, ufahamu huu unaweza KUACHILIA UZIMA KWENYE ENEO HUSIKA UKIAMINI NA KUSHAWISHIKA.
LAKINI PIA UZIMA HUU, UNAOSABABISHWA NA KRISTO NDANI YETU, UNAHAMISHIKA (TRANSFERABLE) KUTOKA KWETU KWENDA KWA WENGINE, NA MAANDIKO YANATHIBITISHA HILO NA YANAWEKA WAZI NAMNA YA KUHAMISHA UZIMA NDANI YETU KUWAGAWIA WENGINE.
Tunahamisha uzima kwa kuwekea mikono lakini pia kwa matamko yetu na njia zingine pia...
Andiko lingine Roho Mtakatifu aliliiweka ndani yangu linalohusiana moja kwa moja na nililonukuu ni;
Wagalatia 2:20 “Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.”
Katika andiko hilo, kitu ambacho Roho Mtakatifu anataka tuone ni "bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu"
Anaongelea tena kitu kile kile, KRISTO YU HAI NDANI YANGU, kisha anasema kitu muhimu sana kwamba UHAI KATIKA MWILI WANGU, UNATOKANA NA UHAI WA KRISTO NDANI YANGU, AU UNATOKANA NA IMANI YANGU KUHUSU UHAI WA KRISTO (MWANA WA MUNGU ALIYE NDANI YANGU).
Hapa anaongelea wazi UHAI KATIKA MWILI, Yaani UHAI au UZIMA katika MIGUU, MIKONO, MOYO, MAPAFU na KILA SEHEMU YA MWILI UNAYOWEZA KUITAJA.
Paulo anaiita hii NI SIRI KUU. YAANI KRISTO KUWA NDANI YETU NI SIRI KUU YA UFALME WA MUNGU AU WOKOVU.
Neno la Mungu limejaa Siri/mafumbo (Mysteries) ambayo usipoyafumbua au zisipowekwa wazi (clear) ndani yako na Roho Mtakatifu hutaweza kuzifurahia.
Na hii ni mojawapo ya SIRI KUU ZA UFALME ILI KUFURAHIA AFYA NA KUWEZA KUWAHUDUMIA WENGINE UPONYAJI.
Ninaamini siri hii IMESABABISHA UZIMA MKAMILIFU KWA KIJANA WANGU, LAKINI PIA SIRI HII IMEMFUNGUA/IMEMPONYA (PAPO HAPO) MAMA MJAMZITO ALIYEKUWA AMEZIMIA KWA MUDA MREFU NA MARA BAADA YA MAOMBI YENYE UFUNUO HUU NDANI YAKE, AKAZINDUKA NA SASA NI MZIMIA.
Natamani KILA MTU AELEWE HII, KRISTO NDANI YETU NI UZIMA, AFYA, UFUFUO, UHAI NDANI YETU...
-- Kristo NDANI YANGU UZIMA KWENYE DAMU YANGU
-- Kristo NDANI YANGU UZIMA KWENYE MAPAFU YANGU
-- Kristo NDANI YANGU UZIMA KWENYE MOYO WANGU
--Kristo NDANI YANGU UZIMA KWENYE MIGUU, MIKONO, KIFUA, KICHWA, TUMBO, NA MWILI WANGU MZIMA.
KRISTO NDANI YANGU UZIMA KWA KILA NITAKAYEMUWEKEA MIKONO KUMUHAMISHIA UZIMA AU KUMTAMKIA ILI KUMUHAMISHIA UZIMA...
Wakolosai 3:3 “Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.”
-- UKWELI NI KWAMBA, UHAI NA UZIMA WETU UMEFICHWA PAMOJA NA KRISTO KATIKA MUNGU. KWELI HII IKIZAMA KABISA NDANI YETU, ITASABABISHA KUSIWE NA NGUVU ZOZOTE ZA GIZA ZINAZOWEZA KUUONA WALA KUUGUSA UZIMA WETU.
Mungu awabariki sana
KRISTO NDANI YAKO, TUMAINI LA UTUKUFU
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author