Text

Kwa Neno Lako Nitazishusha Nyavu

1 views 1 day ago

Luka 5:5-6 SUV

“Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;”

Petro alikuwa ana haki ya kukataa kushusha nyavu kwa sababu zifuatazo:-

1) Alikuwa amechoka baada ya kufanya kazi usiku kucha bila kupata kitu

2) Alikuwa na uzoefu wa kutosha linapokuja swala la uvuvi, maana ndio kazi aliyoifanya miaka mingi!

3) Siku zote wamekuwa wakivua usiku na sio mchana, kwa hiyo mchana haukuwa wakati sahihi kuzishusha nyavu!

4) Hakuwa na uhakika na uzoefu wa anayemuambia zishushe nyavu

Lakini pamoja na hayo yote aliamua kulitii NENO LA YESU!

Petro akajibu "lakini kwa NENO LAKO nitazishusha nyavu"

Kitendo cha kuanza kwa kusema "LAKINI", anamaanisha kuwa pamoja na sababu zote nilizonazo za kutozishusha nyavu, hizo sababu zote naziona hazifai na ninaziachilia na ninaamua kufanya kile UMESEMA!

Mara nyingine ni rahisi sana mazingira yetu na uzoefu wetu kutufanya TUSILIANGALIE NENO LILILOACHILIWA LA YESU!

Ile kwamba HUO UGONJWA UME     HANGAIKA NAO KWA KILA MBINU UNAYOFAHAMU NA KWA KILA DAKTARI UNAYEMFAHAMU, haina maana YESU HAWEZI KUUPONYA!

Petro alikuwa amehangaika sana kupata samaki bila mafanikio, mazingira yenyewe yalikuwa hayaruhusu kupata samaki, uzoefu wake ulikuwa unamuhakikishia kwamba hawezi kupata samaki lakini KWA NENO LA YESU ALIPATA SAMAKI!

Kwa hiyo, kwenye hiyo CHANGAMOTO inayoonekana kushindikana, unachohitaji ni NENO LA YESU TU JUU YA HIYO CHANGAMOTO!

Uzuri ni kwamba NENO LA YESU LINA UWEZO HATA WA KUUMBA VISIVYOKUWEPO; kwa hiyo sio shida hata kama hicho kitu hakipo kabisa kinaweza kuumbwa na kikawa!

“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.” Yohana 1:1, 3 SUV

NENO HILO HILO LINA UZIMA NDANI YAKE, kwa hiyo KIFO WALA HAKILITISHI; hata kama hilo jambo limekufa au kuna vitu vimekufa au una ugonjwa wa kufisha; inawezekana kabisa Neno likafufua na kutia uzima!

“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.” Yohana 1:1, 4 SUV

NENO HILO LINA NURU NDANI YAKE; kwa hiyo giza wala halilitishi; hata kama unaona maishani mwako ni giza tupu au kwenye afya yako ni giza tupu yaani huoni mbele wala huoni dalili ya kutoka, ndani ya Neno iko nuru

“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.” Yohana 1:1, 4-5 SUV

Ifike mahali tuliamini NENO LA MUNGU KULIKO KITU KINGINE CHOCHOTE DUNIANI! Maana Neno la Mungu lina uwezo wa kukifanya kitu chochote kikawa!

SETTLE DOWN, YEYE (MUNGU) AKISEMA ATATIMIZA

YEYE ALIYEAHIDI NI MWAMINIFU; muda kupita haimaanishi hatatimiza!

“Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.” Waebrania 11:11 SUV

SIKU ZA SARA KUKOMA HAIKUGEUZA UAMINIFU WA MUNGU KWA NENO LAKE!

UZEE WA IBRAHIM HAU     KUGEUZA UAMINIFU WA MUNGU KWA NENO LAKE!

KUVUA USIKU KUCHA NA KUKOSA KWA PETRO HAIKUGEUZA UWEZO WA NENO LA MUNGU KUWAKUSANYA SAMAKI ILI AWAVUE!

KUVUA SAMAKI MCHANA [KINYUME NA UTARATIBU] SAWA NA NENO LA MUNGU HAIKUZIA NGUVU YA NENO KUSABABISHA SAMAKI!

TUACHE KULINGANISHA NENO LA MUNGU NA MATATIZO YETU, TUACHE KULINGANISHA NENO LA MUNGU NA TUNACHOITA KUCHELEWA KUPOKEA TUNACHOOMBA! NA BADALA YAKE TULIAMINI NENO LA MUNGU KAMA ALIVYOSEMA PETRO, "PAMOJA NA YOTE HAYO LAKINI KWA NENO LAKO NITACHUKUA HATUA" nikiamini na kujua kwamba LITATIMIZA KUSUDI LAKE!

Katika hali yoyote tafuta kujua NENO LA MUNGU JUU YA HALI HIYO; ukishalijua basi vingine vyote weka pembeni ZISHUSHE NYAVU (yaani chukua hatua) na uamini Mungu atatenda!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!