Kwenye Uwepo wa Mungu - Mahali Pa Mabadiliko ya Kudumu.
Luka 9:28-29
“Baada ya maneno hayo yapata siku nane, aliwatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba. Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta.”
1 Samweli. 10:6
“na roho ya BWANA itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine.”
Yesu alipopanda Mlimani KUSALI kuna vitu vilitokea ambavyo kila aliyekuwa naye aliona kwa wazi kabisa.
Jambo la kwanza ni, SURA YA USO wake iligeuka, na la pili MAVAZI YAKE yakawa meupe yakimeta meta.
Sauli alipojiliwa na Roho wa Bwana kwenye maisha yake, aligeuzwa na kuwa MTU MWINGINE!
- Kwenye uwepo wa Mungu ni MAHALI PA MABADILIKO YA KUDUMU!
- HAIWEZEKANI UWE NA TABIA YA KUKAA KWENYE UWEPO WA MUNGU HALAFU UBAKI VILE VILE!
- Uwepo wa Mungu unakubadilisha kwanza wewe kabla ya mtu mwingine yeyote!
- Kusudi kuu la Mungu kututaka katika uwepo wake (Sala, Maombi na Neno), n i kutubadilisha sisi kabla ya k ujibu maombi yetu.
- Uwepo wa Mungu utakusaidia kukuonyesha wapi unapaswa kurekebisha!
- Uwepo wa Mungu utakusaidia kugundua hata makosa na mdhaifu ambayo siku zote hukuwa unayafahamu!
- Unataka kuwa mkamilifu, Mungu ametupa nafasi kukaa uweponi mwake ili kutukamilisha!
- Kwa kadiri unavyendelea kukaa uweponi mwa Mungu, utaendelea kukamilishwa!
KILA UNAPOINGIA KWENYE MAOMBI NA KUSALI, UNAINGIA UWEPONI MWA MUNGU na KILA UNAPOSOMA NA KUJIFUNZA NA KUTAFAKARI MANENO YA MUNGU, UNAKAA UWEPONI MWA MUNGU!
1. SURA YA USO wake ikageuka.
- Kibali kiko usoni mwa mtu, unahitaji kibali maishani mwako, kaa kwenye uwepo wa Mungu, ghafla utashangaa unaanza kupata kibali hata kwa wale ambao hukuwategemea!
- Mara nyingi watu binafsi au taasisi au wateja nk hutukubali au kutukataa mara ya kwanza tu baada ya kutuona au kuona bidhaa zetu... Kibali cha Mungu kitaanza kufanya watu wakukubali au waikubali bidhaa yako mara tu baada ya kuiona bila hata kukufahamu au kuifahamu sana.
- Kibali kitasababisha mioyo ya WATU AMBAO MUNGU AMEWAKUSUDIA MAISHANI MWAKO iambatane na moyo wako au kazi yako au biashara yako MARA TU BAADA YA KUKUONA.
- Tatizo ni kwamba wengi hatujafanya MAAMUZI YA DHATI KUDUMU KATIKA UWEPO WA MUNGU MAISHA YETU YOTE, tunaingia na kutoka!
“Neno Moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.”
ZAB. 27:4
- Fanya maamuzi leo, kuhakikisha hauachi kwenda mbele za uwepo wa Mungu kila siku na utaanza kuona UWEPO WA MUNGU UKIKUBADILISHA KUWA MTU MWINGINE NA KUFUNGUA KIBALI CHAKO MAENEO MBALIMBALI YA MAISHA.
2. MAVAZI YAKE YAKAWA MEUPE
- JE UNA VIJITABIA AMBAVYO UMEJARIBU KUVIACHA VIM EKUSHINDA? YAANI UMEJARIBU KUACHA VINAJIRUDIA? AMUA LEO UVIPELEKE KWENYE UWEPO WA MUNGU, UTAANZA KUONA MABADILIKO!
- VAZI tunaweza kulitafsiri kama TABIA, ukikaa uweponi mwa Mungu muda wa kutosha, lazima TABIA ZAKO ZIANZE KUBADILIKA!
- UNATAKA BADILIKO LA KUDUMU LA KITABIA? Jiwekee utaratibu wa KUDUMU WA KUKAA KWENYE UWEPO WA MUNGU!
- Unapokaa mbali na uwepo wa Mungu ni sawa na Pannel za solar kukaa mbali na jua, taratibu zitapoteza uthamani wake!
- HAKIKISHA KILA SIKU UNATENGA MUDA MZURI WA UTULIVU WA KUKAA KATIKA UWEPO WA MUNGU KWA NJIA YA MAOMBI, KUSOMA NENO NA KULITAFAKARI NA KWA KADIRI UNAVYOFANYA HIVYO UTAANZA KUONA MABADILIKO YA MAISHA YAKO!
Ninaposema maombi simaanishi tu kwenda kumwambia Mungu nataka hiki na kile, namaanisha kuwa na uhusiano na Mungu. Kuwa na utaratibu wa k wenda mbele za Mungu hata kama huna mahitaji ya kumwambia, kwenda mbele zake kuongea naye, kumsifu, kumuabudu, kumwambia unavyompenda na kusikiliza anataka nini kwako.
Ukijijengea tabia hii, NAKUHAKIKISHIA HAUTABAKI ULIVYO... BADILIKO LA KUDUMU NI LAZIMA.
NAOMBA KUSISITIZA MABADILIKO HAYA HAYATOKEI KWA WATU WA MATUKIO, YAANI KWENDA MBELE ZA MUNGU KWA SABABU YA MATUKIO FULANI FULANI MAISHANI, MABADILIKO HAYA YA KUDUMU NI KWA WALE WANAOFANYA MAAMUZI YA KUDUMU YA KUCHAGUA MAISHA YA AINA HII YA KUKAA KWENYE UWEPO WA MUNGU SAWASAWA NA ZABURI 27:4
“Neno Moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.”
FANYA MAAMUZI LEO, CHAGUA KUKAA UWEPONI MWA MUNGU
At God's presence, is the place for transformation!
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
Mwl. Francis Langula
Author