Kwenye Uwepo wa Mungu ni Mahali Pa Kupata Burudiko (Kuwa Refreshed)
Mathayo. 11:28-29
“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;”
Mdo 3:19
“Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;”
Je unajihisi umechoka nafsini mwako? Unahisi kulemewa hivi?
Inaweza kuwa kwa sababu ya dhambi fulani fulani ambazo ni kama zimegoma kuondoka kwako, umejaribu sana kuacha lakini imeshindikana; yaani imekuwa ni dhambi ikuzingayo kwa upesi!
Au inawezekana ni sababu ya maisha fulani ya mahangaiko, umekuwa ukijaribu kuamini juu ya mambo fulani lakini mara zote umekuwa unakutana na vitu vya kukukatisha tamaa!
Au kwa sababu yoyote ile, umejikuta una hali ya kuchoka na kulemewa! Haujisikii kuendelea tena, haujisikii kufanya chochote, hujisikii tena kuomba wala kufunga wala kusoma neno!
KUNA WITO KWA AJILI YAKO USOGEE KWENYE UWEPO WA MUNGU
SIO LAZIMA IWE KWENDA KUOMBA, BALI KWENDA KUBURUDISHWA, KUWA REFRESHED, KUREJESHEWA UBICHI NA UNYEVU, KUREJESHEWA NGUVU!
Ukiangalia mistari yote miwili ya tafakari hii, KUNA WAJIBU MKUBWA SANA KWA MUHUSIKA ALIYELEMEWA!
Wa kwanza unasema "Njooni kwangu" ikiwa na maana muhusika ndio anayefanya maamuzi ya kwenda kupata PUMZIKO AU BURUDIKO!
Wa pili unasema "TUBUNI MREJEE" ikiwa na maana kwamba, GEUZA UFAHAMU WAKO NA KUSUDI LAKO, NA NJIA ZAKO UMUELEKEE MUNGU
Kwenye maandiko hayo yote mawili, chini kabisa yanaongelea, kwa kufanya hivyo, UTAPATA BURUDIKO LA NAFSI KATIKA UWEPO WA MUNGU UTAKAOUENDEA
Kwa hiyo, tunaweza kufanya uamuzi kwa kwenda uweponi mwa Mungu kwa lengo la kupata burudiko (kuwa refreshed) ikiwa na maana ya kuongezewa nguvu hata kama tunahisi kuchoka na kulemewa au sababu ya mapito au hata dhambi!
Tatizo letu ni kwamba tukihisi kuchoka, kulemewa au kushindwa, TUNAKAA MBALI NA UWEPO WA MUNGU BADALA YA KUKAA KATIKA UWEPO WA MUNGU.
Wakati ambapo hujisikii kuomba, kufunga au kusoma Neno; Ni vizuri sana kukimbilia kwenye uwepo wa MUNGU!
Unaweza ukaamua kwa kumaanisha ukatenga muda wa kutulia mwenyewe na KUMWAMBIA ROHO MTAKATIFU NIMEKUJA UWEPONI MWAKO NAOMBA UNIHUDUMIE NA KUNIHUISHA TENA; halafu ukatulia hata kama ni kimya kwa muda wa kutosha utaanza kuona NGUVU ZAKO ZINAHUISHWA NDANI YAKO!
Neno la Mungu linasema, "Wamngojeao Bwana, watapata nguvu mpya..."
Unaweza ukaamua kutenga MUDA NA KUANZA KUTAFAKARI NENO LA MUNGU(KUUWAZA MSITARI FULANI KWENYE BIBLIA HUKU UKIUONGEA KWA SAUTI UNAYOWEZA KUJISIKIA) KWA MUDA WA KUTOSHA UTAJIKUTA UNAKUWA REFRESHED!
Unaweza ukaamua kutulia na kumuabudu Mungu kwa nyimbo za kuabudu au kwa maneno yako, baada ya muda utajiona unakuwa refreshed!
Unaweza ukaamua kusikiliza mafundisho au mahubiri hasa kuhusu Roho Mtakatifu na baada ya muda utajikuta umekuwa refreshed!
Hata kama umefanya dhambi, ni vizuri kukumbilia kwa MUNGU NA KUTUBU NA SIO KUUKIMBIA UWEPO WA MUNGU!
Daudi alichagua uwepo wa Mungu hata baada ya kukosea
“Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.”
2 SAM. 24:14 SUV
KATIKA HALI YOYOTE, CHAGUA KUK IMBILIA KWENYE UWEPO WA MUNGU, HUKO NI SALAMA ZAIDI KULIKO SEHEMU NYINGINE YOYOTE!
At God's presence is the PLACE FOR REFRESHMENT!
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
Mwl. Francis Langula
Author