Text

Kwenye Uwepo wa Mungu ni Mahali Pa Maelekezo, Nenda Ukiwa Umejiandaa

1 views 1 day ago

Kumb. 10:1-2, 4

Wakati ule BWANA akaniambia, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, kisha uje kwangu huku mlimani, ukajifanyie na sanduku la mti. Nami nitaandika juu ya hizo mbao maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, ulizozivunja, nawe uzitie ndani ya hilo sanduku.

Naye akaandika juu ya mbao mfano wa maandiko ya kwanza, zile amri kumi, alizowaambia BWANA huko mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano; BWANA akanipa.

MAMBO YA KUJIFUNZA:

Kila unapoenda kwenye uwepo wa Mungu hakikisha una mbao mbili ili MUNGU akitoa maagizo pawepo mahali pa kuyaandika!

Watu wengi tunaenda mbele za Mungu bila kujiandaa kupokea maagizo au maelekezo na matokeo yake tumekuwa tunapeleka mahitaji yetu na tunatoka bila hata kujua maelekezo yoyote ya Mungu kuhusiana na mahitaji tuliyompelekea!

TUNAENDA MBELE ZA MUNGU AU KWENYE UWEPO WA MUNGU KWA NJIA MBILI:

1) Kwa njia ya MAOMBI

KILA UNAPOENDA MBELE ZA MUNGU, KWA NJIA YA MAOMBI HAKIKISHA UMECHUKUA NOTEBOOK YAKO NA KALAMU TAYARI KWA KUANDIKA KILA MAELEKEZO ATAKAYOKUPATIA!

Maelekezo yanaweza kuja kama sauti ya Mungu au yanaweza kuja kama wazo ndani yako ukiwa katika uwepo wa Mungu!

Uwe mwangalifu sana na WAZO Mungu analodondosha ndani yako unapokuwa katika uwepo wa Mungu, liandike na ulifanyie kazi mara nyingi linakuwa limebeba JIBU!

Andika mawazo na maelekezo Mungu anayokupatia katika maombi

2) Kwa njia ya KUSOMA NENO LAKE

- Kila unaposoma Neno la Mungu, uko mbele za uwepo wa Mungu, kwa hiyo hakikisha una kalamu na notebook karibu, kwa sababu utakutana na maelekezo! Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuyahuisha maandiko na kuyafanya halisi kwenye maisha yetu na kutupatia maelekezo ya kututoa mahali na kutupeleka mbele, kwa hiyo unaposoma maandiko uwe na uhakika Roho Mtakatifu atakupa maelekezo, ni muhimu kukaa mkao wa kupokea maelekezo!

TATIZO KUBWA KWA NINI HATUPOKEI MAELEKEZO TUNAPOENDA KWENYE UWEPO WA MUNGU, NI KWA SABABU HATUENDI KWA IMANI TUKIYATARAJIA MAELEKEZO HAYO

KITENDO CHA KWENDA UKIWA UMECHONGA MBAO AMBAZO MUNGU ATAANDIKA (YAANI UKIWA NA NOTEBOOK NA KARAMU) NI KITENDO CHA IMANI NA MUNGU AKIONA HICHO ATAKUPA TU AMRI (MAELEKEZO)

Fanyia kazi hili kuanzia leo na utaanza kuona matokeo!

KWENYE UWEPO WA MUNGU PALIVYO MAHALI PA MAELEKEZO; KWA HIYO NENDA UKIWA UMEJIANDAA KUPOKEA MAELEKEZO

At God's presence, is the place for instructions!

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula

 

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!