Text

Maana ya Imani na Nguvu ya Imani

1 views 1 day ago

Waebrania 11:1 SUV

"Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana."

"NOW FAITH is the assurance (the confirmation, the title deed) of the things [we] hope for, being the proof of things [we] do not see and the conviction of their reality [faith perceiving as real fact what is not revealed to the senses]." Hebrews 11:1 AMPC

MAMBO YA KUJIFUNZA:

IMANI ni hali ya kuwa na uhakika ya kwamba kile unachokitarajia utakipata.

--Je unatarajia jambo na una uhakika bila shaka utapata unachotarajia? Hiyo ndio IMANI YENYEWE; Hakuna cha kukuzuia KUPOKEA

--Unatarajia uponyaji na una uhakika bila shaka utapokea? Hakuna cha ziada, tamka unachokiamini na POKEA UPONYAJI WAKO!

IMANI ni uwezo wa kuona kwa uhalisia wake jambo ambalo halijaonekana kwa macho ya nyama wala hujalihisi kwa milango ya fahamu.

--Je, una uwezo wa kujiona MZIMA ingawa bado hisia zako zinakuambia UNAUMWA? Huo ni uwezo tosha KUKUMILIKISHA AFYA YAKO; Shetani asikuwekee masharti mengine

--Je, una uwezo wa KULIONA HILO JAMBO ambalo kwa macho ya nyama halionekani?

IMANI ni HATI MILIKI (TITLE DEED) ya mambo unayoyatarajia!

- Hati Miliki ni waraka (document) wa kisheria unaoonyesha umiliki wa halali wa rasilimali (property).

- Kama unayo hati miliki haimaanishi wewe utakuja kuwa mmiliki wa rasilimali hiyo bali inamaanisha WEWE TAYARI NI MMILIKI HALALI WA RASILIMALI HIYO!

--Kwa hiyo KAMA UNAYO IMANI JUU YA UZIMA AU UPONYAJI AU AFYA basi wewe tayari ni MMILIKI HALALI WA AFYA AU UZIMA AU UPONYAJI.

--Kwa hiyo, IMANI SIO BAADAYE BALI NI SASA MAANA HATI MILIKI HAIONGELEI BAADAYE BALI NI SASA.

Ndio maana YESU ALISEMA:

“Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini [muda ule ule mnaosali] ya kwamba mnayapokea [wakati huo huo mnaosali] nayo yatakuwa yenu [yatadhihirishwa kwenye macho yenu ya nyama].” Marko 11:24

--Muda ule unaposali ukiamini, tayari umejimilikisha HATI MILIKI YA KILE UNACHOKIOMBEA.

--IMANI haina baadaye, imani ni sasa ingawa udhihirisho katika macho ya nyama unaweza kuchukua muda lakini UMILIKI (IMANI) ni muda ule ule wa kusali au kuomba au kutamka

--IMANI sio nguvu ya kimwili ndio maana haina MUDA [FAITH is the spiritual force or commodity that's why it has no time limitations].

--Ulimwengu wa roho haufungwi na muda, ndio maana Mungu akajitambulisha yeye ni NIKO AMBAYE NIKO; na IMANI haifungwi na muda kwa sababu IMANI ni bidhaa ya rohoni.

--Kwa hiyo KATIKA Ulimwengu wa roho IMANI INAMILIKI JIBU MUDA ULE ULE ILIPOACHILIWA; lakini kwa sababu ULIMWENGU WA MWILI UMEFUNGWA NA MUDA ndio maana udhihirisho katika ulimwengu wa mwili lazima utachukua muda (yaweza kuwa sekunde, dakika, siku, wiki nk)

Ndio maana katika mistari tuliyonukuhu MK 11:24 YESU akasema "nayo YATAKUWA yenu" akimaanisha huku duniani itachukua muda kuonekana kwa macho ya nyama.

- Hata miujiza ya papo kwa papo kuna sekunde kadhaa zinahesabika huku duniani.

--Habari njema ni kwamba, unapoachilia IMANI wakati unaomba au kutamka jambo, unayo mamlaka ya kutamka na muda wa udhihirisho pia [Kama vile Yoshua alivyosimamisha jua, Kama Eliya alivyoshusha moto nk].

--Kwa hiyo ukichanganya IMANI na kutambua mamlaka yako, unaweza uka control muda wa jambo au uponyaji kutokea!

IMANI ni UTHIBITISHO au UBAYANA au USHAHIDI wa MAMBO TUSIYOYAONA kwa macho ya nyama.

--Kwa hiyo kama unaamini juu ya jambo, mtu akikuuliza UTHIBITISHO au akikwambia nipatie USHAHIDI kwamba jambo hili litatokea mwambie IMANI YANGU NDIO UTHIBITISHO WENYEWE.

--Kwa mtu mwenye IMANI, imani inashikika, imani ndio ushahidi wenyewe... Haitaji ushahidi mwingine!

--Sihitaji USHAHIDI mwingine kwamba NINACHOKIAMINI KITAFANYIKA, YAANI HIYO IMANI NDIO USHAHIDI TOSHA, wala haihitaji kusaidiwa!!!

Kama unayo IMANI, una kila unachohitaji.

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Framcis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!