Text

Mahali Penye Upinzani ni Mahali Pa Kumiliki

1 views 1 day ago

Kumbukumbu la Torati 2:30, 33

“Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, alimfanya mgumu roho yake, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate mtia mkononi mwako kama alivyo hivi leo. BWANA, Mungu wetu, akamtoa mbele yetu, tukampiga yeye na wanawe, na watu wake wote.”

Kuna kitu nimekiona kwenye maandiko haya, nikaona nishirikiane nawe kwa ufupi kabisa.

Ukisoma kuanzia mstari wa 26 wa Kumbukumbu ya torati sura ya 2, utaona, Musa na wana wa Israel, baada ya kukaribia nchi ya Heshboni, kama kawaida yao, walituma wajumbe kwa mfalme wa nchi hiyo na kumuomba awaruhusu wakatize kwenye nchi yake wakiwa wanaelekea kwenye nchi yao ya ahadi, Kanaani. Mfalme wa Heshboni akawakatalia kukatiza kwenye nchi yake.

Mistari niliyonukuu hapo juu inaeleza kitu ambacho kinashangaza kidogo kwa kile ambacho kimetokea.

Neno linasema, "Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, alimfanya mgumu roho yake, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate mtia mkononi mwako".

Kwa hiyo, Mfalme hakuwaruhusu wapite kwa sababu, MUNGU ALIMFANYA MGUMU ROHO YAKE KWA KUSUDI LA KUMTIA MIKONONI MWA ISRAELI.

Najaribu kuwaza, wakati Musa na Israel wanaona kama WANAZUILIWA KUPITA KUELEKEA KANAANI kwenye ahadi ya Mungu, KUMBE MUNGU ANATAKA KUWAMILIKISHA HIYO NCHI      INAYOONEKANA KUWAPINGA NA KUWAZUIA.

Kuwazuia na kuwapinga ILIKUWA NI ISHARA YA NJE inayoonyesha kwamba ile nchi inapaswa kumilikiwa na Israel.

Kuwazuia na kuwapinga ilikuwa NI LUGHA YA ISHARA KWAMBA SISI NI MALI YAKO TUMILIKI.

Kumbe SIO KILA KIZUIZI KINAMAANA YA KUKUZUIA USIPITE, VIZUIZI VINGINE NI ISHARA YA UMILIKI.

Sio kila ugumu ni KIZUIZI, UGUMU MWINGINE UNAMAANISHA UMILIKI. UGUMU MWINGINE UNAMAANISHA, MUNGU AMELITIA JAMBO HILO MIKONONI MWAKO.

Mara nyingi tumezichukulia changamoto kama vizuizi na zimetukatisha tamaa, lakini kumbe tulipaswa kuziona kwa macho mengine na KUPAMBANA KUMILIKI.

Ukifuatilia maandiko kuanzia sura ya kwanza ya kumbukumbu, utaona Israel walipita nchi kadhaa ambazo waliwaruhusu bila kikwazo chochote mpaka nchi hii ya Heshboni ndio walikutana na upinzani.

Pale ambapo unaona kuna upinzani, UJUE KUNA VITU MUNGU ANATAKA AKUMILIKISHE KABLA YA KUPAVUKA, USIUANGALIE UPINZANI KWA KUKATA TAMAA BALI UANGALIE KAMA FURSA YA KUMILIKI, fanya jambo sahihi na MUNGU ATAKUMILIKISHA.

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!