Maisha na Maamuzi
Kumbukumbu la Torati 30:19
"Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;"
Maisha tunayoishi duniani yamejaa maamuzi, na kwenye kila maamuzi kuna mambo mawili tu, UZIMA NA MAUTI.
Maamuzi tunayofanya ndani yake yanaweza kuwa yamebeba UZIMA au MAUTI, FAIDA au HASARA, UZURI au UBAYA nk.
Lakini pia maisha tunayoishi leo ni matokeo ya maamuzi ambayo tuliwahi kufanya au tumekuwa tukifanya.
Maisha ni matokeo ya maamuzi madogo madogo ambayo tunayafanya kila siku.
Ni matokeo ya maamuzi ya kila Sekunde, dakika, saa, siku, wiki, mwezi, na mwaka ambao MUNGU ANATUPATIA.
Maisha yangu ya mwaka mzima huu tangu umeanza ni matokeo ya maamuzi madogo madogo ninayoyafanya kila sekunde na kila saa Mungu anayonipatia.
Maisha yangu ya kifedha niliyonayo ni matokeo ya maamuzi ninayofanya au niliyofanya kwa KILA PESA Mungu anayoruhusu ipite mikononi mwangu.
Maisha yangu na Mahusiano na watu ni matokeo ya maamuzi ninayofanya KWA KILA MTU AMBAYE MUNGU ANANIKUTANISHA NAYE au kwa kila mtu ninayepata fursa ya kukutana au kufahamiana naye.
Kwa ufupi, maisha yangu ni matokeo ya maamuzi ninayofanya kuhusu:-
- Muda Mungu anaonipatia
- Pesa inayopita mikononi mwangu
- Watu ninaokutana nao
- Yale ninayosikia na kujifunza
- Vitabu ninavyosoma
Na vingine vingi...
Kwa mujibu wa maandiko niliyonukuhu, kwenye kila tunachokutana nacho, tuna machaguo mawili tunaweza kufanya, UZIMA au MAUTI, BARAKA au LAANA, FAIDA au HASARA.
"Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;" Kumbukumbu la Torati 30:19
Hata kama nimewahi kufanya maamuzi mabaya maishanji mwangu au ninaishi matokeo ya maamuzi mabovu niliyoyafanya, NENO LA MUNGU LINANIPA NAFASI NYINGINE YA KUCHAGUA.
Ukigundua umefanya au ulifanya maamuzi mabaya, usikwamie hapo, FANYA MAAMUZI MENGINE. Tubia maamuzi mabaya, samehe waliokukosea, ujisamehe kwa kukosea, waombe msamaha uliowakosea kwa maamuzi yako, HALAFU FANYA MAAUZI MAZURI KWA KUMAANISHA, NA UENDELEE NA MAISHA.
Kukosea maamuzi sio mwisho wa maisha. Usikae hapo, fanya maamuzi ya kuinuka na kuendelea.
Mwenye haki huanguka mara saba lakini kila akianguka ANAFANYA MAAMUZI YA KUINUKA TENA.
Basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako...
KUNA MAAMUZI UNAWEZA KUFANYA LEO UKAWA HAI (YENYE FAIDA) SI WEWE TU BALI NA UZAO WAKO.
Kuna maamuzi unaweza kufanya YAKAKUATHIRI SI MAISHA YAKO YA SASA TU BALI NA MAISHA YAKO BAADA YA KUFA.
Maamuzi ya KUMPOKEA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO BINAFSI NDIO MAAMUZI MUHIMU KULIKO YOTE MWANADAMU ANAWEZA KUFANYA MAANA HAYAISHII DUNIANI TU BALI NDIO MAAMUZI PEKEE YANAYOWEZA KUMPATIA MTU UZIMA WA MILELE MBINGUNI.
Kama kuna eneo Mungu analiheshimu kwa mwanadamu, NI ENEO LA MAAMUZI BINAFSI YA MTU. Mungu na uungu wake wote, HAINGILII MAAMUZI YA MTU, atamshauri tu kama alivyofanya kwenye andiko hilo tulilosoma.
Mungu AMEKUWEKEA LEO UZIMA na MAUTI, chagua UZIMA, CHAGUA WOKOVU, MCHAGUE YESU, FANYA MAAMUZI SAHIHI LEO.
Chagua kuacha uovu, Chagua KUSAMEHE, Chagua TOBA... CHAGUA CHAGUO SAHIHI... CHAGUA KUINUKA TENA, CHAGUA KUREKEBISHA... CHAGUA KUMRUDIA MUNGU... CHAGUA KUANZA TENA MAISHA YA KUMPENDEZA MUNGU... CHAGUA KUANZA TENA KUMTAFUTA MUNGU... CHAGUA KURUDIA MAISHA YA MIFUNGO NA MAOMBI ULIYOYAACHA... CHAGUA KUTOKATA TAMAA NA KUSONGA MBELE...
MAAMUZI UNAYO WEWE NA SI MWINGINE
"Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA." Yoshua 24:15
Chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako. Chagua kumtumikia Mungu... Chagua wokovu...
UAMUZI NI WAKO
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author