Maneno yamebeba Roho Nyuma yake
Ayubu 32:18
“Kwa kuwa nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza."
MAMBO YA KUJIFUNZA:
- Unataka Roho Mtakatifu ndani yako kukuhimiza? Au kukusukuma kufanya mambo ya Mungu? Jaza Neno la Mungu ndani yako!
- Maneno ya Mungu, yana uvuvio wa Roho wa Mungu nyuma yake, ndio maana yakimjaa mtu Roho wa Mungu humuhimiza
“Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” Yohana 6:63
- Kwa maneno hayo aliyosema Yesu, inadhihirisha kuwa kuna Roho nyuma ya maneno.
-Sasa kama Roho wa Mungu yupo kuya support maneno ya Mungu, tuwe na uhakika kwamba, hata nyuma ya maneno yasiyo ya Mungu kuna nguvu ya roho isiyo ya Mungu kuyavuvia!
- Tuwe waangalifu tunasikiliza nini, maana haiishii kwenye kusikiliza, inaathiri na nguvu za roho zetu pia!
- Kilichommaliza Samson ni kuruhusu kuendelea kusikiliza maneno ya ubembelezi toka kwa Delila ilihali akijua kwa hakika Delila alikusudia kumuua; yaani anajua kabisa huyu mtu amebeba mauti yangu lakini anaendelea kuwa karibu naye na kusikiliza maneno yake muda mwingi!
“Ikawa, kwa vile [Delila] alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa." Waamuzi 16:16
- Kilichofanya roho ya Samson idhikike kiasi cha kufa ni maneno ya ubembelezi ya Delila.
- Huwezi kuniambia yale maneno yalikuwa maneno matupu, lazima yalikuwa na nguvu nyuma yake iliyodhuru roho ya Samson kiasi cha kudhikika hata kufa na mwisho wake Samson alitoa siri iliyosababisha madhara na mauti kwake.
“Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu;" Mithali 5:3-5
--Kwa kadiri unavyoendelea kusikiliza maneno hayo ya ubembelezi (yanayoonekana kama asali) toka kwa huyo mkaka au mdada ambaye sio mume wako wala mke wako (hata kwenu hawamjui, unajua hana hata mpango wa kukuoa au huma mpango wa kumuoa), unaruhusu roho ya uzinzi iliyo nyuma ya maneno hayo kuidhoofisha roho yako(hata kama kwa wakati huo sio kusudi lako) na ikifika point ya roho yako kudhikika kiasi cha kufa [kama Samson] ndio unashangaa mkaka au mdada na ulokole wake wote ameanguka chali tena mahali hata yeye anajishangaa.
--Kama kweli unampenda Mungu na unamsimamo, usiendelee kusikiliza hayo maneno yasiyofaa.... Kata hiyo connection maana NI CONNECTION NA MAUTI; Usidhani ni maneno matupu tu, yana roho nyuma yake na yanaweza kukuangamiza kabisa.
--Kama haufahamu, hiyo ndio barabara ya mauti na kuzimu, na hicho unachoruhusu ndio umeshaanza kupiga hatua kuelekea shimoni sawa na Neno tulilonukuhu hapo juu “Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu;” Mithali 5:5
Turudie andiko letu la msingi:
“Kwa kuwa nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.” Ayubu 32:18
Unataka Roho wa Mungu ndani yako kukuhimiza katika mambo ya Ki-Mungu, basi jaza maneno ya Mungu ndani yako kwa kusoma Neno, kusoma na kusikiliza mafundisho sahihi.
Unataka roho iliyo ndani yako kukuhimiza kutenda dhambi au kukiishi unachokisikia, basi endelea kujaza hayo maneno ya tamthilia na movie za mapenzi masaa yote, endelea kujaza hizo nyimbo za mapenzi asubuhi mpaka jioni, endelelea kusikiliza maneno ya ubembelezi yanhuyo mkaka/madada; Na siku ukijikuta chali na ulokole wako usitafute mchawi; umejiroga mwenyewe kwa yale maneno ambayo unayaruhusu kuyasikiliza masaa yote!
Neno la Mungu linasema, UZIMA NA MAUTI VIMO KATIKA UWEZO WA ULIMI.
Uwe mwangalifu na MANENO UNAYORUHUSU KUYASIKILIZA!
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author