Msamaha na Heshima
Zaburi 130:4
“Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe.”
“Lakini kwako twapata msamaha, ili sisi tukuheshimu.” Zaburi 130:4 BHND
But there is forgiveness with You, That You may be feared and worshiped [with submissive wonder]. PSALMS 130:4 AMP
But with you there is forgiveness, so that we can, with reverence, serve you. Psalm 130:4 NIV
Mungu ameweka Neno hili ndani yangu kwa mda kidogo na nimeona tulitafakari kwa pamoja.
Mwandishi anamwambia Mungu, KWAKO KUNA MSAMAHA, ILI WEWE UOGOPWE.
Hilo Neno "UOGOPWE", Ukifuatilia tafsiri mbalimbali na baadhi nilizoziweka hapo juu, linamaana UPATE HESHIMA, AU UHESHIMIWE KWA KIWANGO CHA JUU.
Nikagundua kwamba, hii ni moja ya sababu MUNGU HUHESHIMIWA, HII NDIO MOJA YA SIRI YA HESHIMA YA MUNGU.
Jaribu kufikiria MUNGU ASINGEKUWA NI WA REHEMA NA MSAMAHA.
“Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.” Maombolezo 3:22-23 SUV
Ni kwa sababu ya huruma za Mungu HATUANGAMII, ni kwa sababu KWAKE KUNA MSAMAHA, ndio maana sisi HATUANGAMII.
Kiwango cha utakatifu na uadilifu wa Mungu kiko juu mno kiasi ambacho Mungu angeamua kuwa strict, bila kutusaidia kuvifikia viwango vyake kwa kutupatia Neema ya Yesu, Neno la lake na Damu ya Yesu, basi hakuna mtu angeishi, sote tungeangamia.
Ndio maana Neno linasema, Ni huruma (upendo, msamaha, wema na neema) za Bwana HATUANGAMII.
Na kwa kuonyesha u-serious wa jambo hili ili tusiangamie anasema, NI MPYA KILA SIKU ASUBUHI.
Yaani Mungu akagundua, TUKITUMIA REHEMA (MSAMAHA) YAKE ILIYOTUSAIDIA JANA KWA UOVU AU MAPUNGUFU YA LEO, inawezekana tukaangamia, AKAAMUA KILA SIKU AWE ANAZIACHILIA REHEMA (MSAMAHA) MPYA.
Kama vile tusivyotumia JUA NA MWEZI WA JANA LEO, KAMA TUSIVYOTUMIA HEWA YA JANA LEO, NDIVYO ILIVYO NA REHEMA (MSAMAHA) ZA MUNGU, TUNAZIHITAJI KILA SIKU.
Ndio maana DAMU YA YESU haina siku ya kuisha muda wake (Expire date).
Hii NI MOJA YA SIFA KUBWA YA MUNGU NA NDIO MOJA YA SABABU TUNAMUHESHIMU KWA KIWANGO CHA JUU.
Kwa sababu KWAKE KUNA MSAMAHA NDIO MAANA HAJAWAHI KUGHAIRI KUTOA JUA, KWAKE KUNA MSAMAHA NDIO MAANA HAJAWAHI KUGHAIRI KUTOA HEWA SAFI(OXYGEN) pamoja na maovu mengi yanayoendelea huku duniani.
Neno la Mungu linasema "Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe [au UHESHIMIWE ZAIDI]." Zaburi 130:4
Kwa Mungu kuna msamaha ILI TUMUHESHIMU, ndio maana anaheshimiwa.
Hii si heshima tu ya kawaida bali ni heshima ya kiwango cha juu sana (reverence).
Tukiichukua kanuni hii, itafanya kazi na kwetu pia.
Tukiwa na misamaha mingi, kiasi kwamba kila asubuhi tunaandaa misamaha ya kutosha kwa wale waliotukosea na watakaotukosea siku hiyi, hii itatuongezewa HESHIMA (Thamani) mbele za Mungu na pia mbele za watu; Heshima yetu itakua.
Bahati mbaya ni mwamba, SHETANI AMEIGEUZA KWELI HII KWENYE FIKIRA ZA WATU. Watu wengi wanafikiri, WAKIWA WEPESI KUSAMEHE, BASI WANAJISHUSHIA HESHIMA ZAO.
Wanadhani wakisamehe haraka, watadharauriwa, wataonekana ni wadhaifu, wataonekana ni wanyonge kwenye mahusiano, lakini HUO NI UONGO WA SHETANI, Ili kuwaweka watu wengi kwenye VIFUNGO VYA KUTOKUSAMEHE.
Kutokusamehe, kwa mfano wa Yesu wa Mathayo 18, husababisha mtu kuwekwa kwa watesaji.
“Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.” Mathayo 18:34
Kutokusame hukufanya mfungwa au mtumwa kwa lile kosa na kwa watu, kusamehe hukufanya kuwa huru.
Wepesi kusamehe huongeza HESHIMA YAKO. Kwa upande wa pili, UGUMU WA KUSAMEHE HUKUSHUSHIA HESHIMA YAKO.
Amua kusamehe HARAKA, itakuongezea HESHIMA YAKO kwa huyo unayemsamehe na mbele za Mungu.
Kama Msamaha na Rehema za Mungu kwetu ndio zinatufanya TUMUHESHIMU na KUMUHOFU; Basi msamaha na Rehema zetu kwa watu zitatuongezea Heshima pia.
“Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe.” Zaburi 130:4
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author