Text

Mungu Anaweza

1 views 1 day ago

Zekaria 8:6 SUV

“BWANA wa majeshi asema hivi, Ingawa hili ni neno lililo gumu mbele ya macho ya mabaki ya watu hawa katika siku hizo, je! Liwe neno gumu mbele ya macho yangu? Asema BWANA wa majeshi.”

"kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu." Luka 1:37 SUV

"Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA?" Mwanzo 18:14a SUV

"Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza;" Yeremia 32:17 SUV

Ni kweli neno hilo ni gumu mbele zako na mbele ya macho ya kila mtu!

Ni kweli ni gumu hata mbele ya madaktari bingwa!

Ni Kweli kabisa ukiangalia unaona giza hauoni kama kuna mpenyo

Ni Kweli kabisa hauna kumbukumbu ya mtu aliyewahi kupatwa na jambo kama hilo na akavuka salama!

HATA MUNGU HAJAPINGA JUU YA UHALISIA (FACT) HUO MBELE YA MACHO YETU, LAKINI UHALISIA WA JAMBO HAUAMUI HATMA YA JAMBO, BADO KUNA KWELI (TRUTH) YA NENO LA MUNGU!

NA HILI NDIO SWALI MUNGU ANAKUULIZA LEO:- 

BWANA wa majeshi asema hivi, Ingawa hili ni neno lililo gumu mbele ya macho ya mabaki ya watu hawa katika siku hizo, JE! LIWE NENO GUMU MBELE YA MACHO YANGU? Asema BWANA wa majeshi.

Kwenye Neno hilo, Mungu hajapinga uhalisia (Fact) lakini ameonyesha uhalisia sio mwisho wa jambo bali kuna kweli (Truth) ya NENO LA MUNGU inayoweza kugeuza uhalisia wa aina yoyote ile!

Kutoona mwisho au kuona giza mbele haimaanishi umefikia ukingoni INAMAANISHA UMEFIKIA MWANZO WA UTENDAJI WA MUNGU BILA MSAADA WA MWANADAMU!

Israel walipoona bahari walidhani wamefikia mwisho lakini kumbe ndio ilikuwa mwanzo wao wa KUONA MKONO WA MUNGU UKIWAVUSHA NA KUWAPIGANIA KWA NAMNA AMBAVYO HAWAJAWAHI KUONA!

Najua KWELI (TRUTH) Hii inaweza kuwa ngumu kuielewa, lakini wakati mwingine HAUHITAJI KUELEWA ITAFANYIKAJE, UNAHITAJI TU KUAMINI (KU-TRUST) BILA MASWALI!

Uzuri ni kwamba UNAYEMUAMINI NI EXPERT WA KUTENGENEZA NJIA! 

Anaweza kufanya njia kwenye maji kwa KUYAPASUA MAJI ISRAEL WAPITE LAKINI PIA ANAWEZA KUFANYA NJIA KWENYE HAYO HAYO MAJI KWA KUMUAMURU PETRO NJOO na AKATEMBEA JUU YA MAJI!

Hata kama ulitegemea APASUE MAJI UPITE KAMA ISRAEL LAKINI HUKUONA YAMEPASUKA, HAINA MAANA HIYO NDIO NJIA PEKEE! AMINI TU NA UTAONA ATAKAVYOKUSHANGAZA; KAMA MAJI HAYAJAPASUKA, BASI UTATEMBEA JUU YAKE, KWA VYOVYOTE VILE KUVUKA NI LAZIMA.

He is a wonderful JESUS! He is a way maker!HE CAN DO WHAT NO MAN CAN DO!

Anaweza kufanya ambacho hakuna binadamu yeyote anaweza kufanya!

Anaweza kubadilisha kila hali iliyoshindikana! 

"Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara. Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi." Warumi 4:19-21 SUV

Hata kama umefika mahali unaona kama MUNGU AMESAHAU ALICHOKUAHIDI!

Nakuhakikishia, MUNGU AWEZA KUFANYA YALE ALIYOAHIDI KAMA ALIVYOFANYA KWA IBRAHIM!!

Hali ya mwili wake na wa mke wake ilikuwa IMEKUFA (FACT) lakini ilikuweko AHADI YA MUNGU (TRUTH) ambayo ilikuwa inawafuatilia!

MUNGU ALIMUULIZA SARAH, "Je kuna neno gumu la kumshinda Mungu?"

Kuna maswali mengine unajiuliza na unaona kama hayana majibu, lakini jibu lake ni kwamba, "LIMERUHUSIWA HILO ILI MUNGU ATUKUZWE" 

“Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.”YN. 11:4 SUV

Ni kama vile Yesu amechelewa kujibu, ni kama vile angekujibu jana angekuwa ndio amejibu kwa wakati maana angekuepusha na aibu hiyo kubwa; angekuepusha na maumivu hayo ya moyo! 

“Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne.Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.” Yohana 11:17, 21 SUV

YESU HUWA HACHELEWI (JESUS IS NEVER TOO LATE)! 

Acha maswali mengi, AMUA KUAMINI (KU-TRUST)! Sio lazima upate majibu ya maswali yote! Kuna majibu mengine huwezi kuyapata leo ila utayapata AKISHAKUVUSHA!

Kama alifanya kwa familia ya Martha, Mariam na Lazaro, ATAFANYA NA KWAKO PIA!

Kama alifanya kwa Ibrahim na Sarah, ATAFANYA NA KWAKO NA KWANGU PIA!

Shetani anataka uangalie mahali pasipo sahihi, uangalie tatizo na ukubwa wake ili usiuone ukuu wa Mungu!

MWAMBIE SHETANI ACHA KUNIDANGANYA, MUNGU WANGU NI MWAMINIFU ATAFANYA TENA, MUNGU WANGU NI MKUU KULIKO HILI TATIZO, HAJAWAHI KUSEMA UONGO, WALA HATAANZIA KWANGU KUSEMA UONGO! 

HE DID IT AND HE CAN DO IT AGAIN!

Moyo wangu tulia, moyo wangu acha kunisumbua, moyo wangu MTUMAINI BWANA!!

MUNGU ANAWEZA, MUNGU BADO ANAWEZA, MUNGU ANAWEZA TENA!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!