Text

Mungu Aweza Kukutolea Chakula Katika Hicho Unachodhani Kitakumaliza

1 views 1 day ago

Waamuzi 14:14

“Naye akawaambia, Katika huyo mwenye kula kikatoka chakula, Katika huyo mwenye nguvu ukatoka utamu.”

Ili tuweze kupata picha kamili, ninanuku     u hapa chini m     aandiko ya nyuma kidogo kabla ya hilo nililonuku     u juu.

Waamuzi 14:5 -9 “Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba akamngurumia. Roho ya BWANA ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya. Basi akatelemka na kuzungumza na huyo mwanamke; naye akampendeza Samsoni sana. Kisha baadaye akarudi ili kumtwaa, naye akageuka kando kuuangalia mzoga wa huyo simba; na tazama, nyuki wengi walikuwamo ndani ya mzoga wa simba, na asali. Akatwaa asali mikononi mwake akaenda mbele, huku akila alipokuwa akienenda, akawafikilia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba.”

Ukisoma Waamuzi 14:8-9 ambayo ipo kati ya mistari niliyonukuu hapo juu utaona,

- Mwanzoni Simba alionekana anaweza kumuangamiza Samson na wazazi wake, lakini Nguvu ya Mungu ikamsaidia Samson akamuua Simba wala hakuwadhuru. Nina uhakika Samson alijua habari ya simba imeishia hapo.

- Wakati anarudi akakuta mzoga wa simba umegeuka kuwa kama mzinga wa nyuki wenye asali.

- Mwanzo simba alikuwa hatari kwa maisha ya Samson na familia yake, Nguvu ya Mungu ikamsaidia kumuua; baadaye simba alionekana kama mzoga (hana madhara yoyote kwenye maisha yake lakini pia hafai kwa lolote), ndani ya mzoga walionekana nyuki wengi (ambao wanaweza kuuma na kusababisha madhara), lakini baada ya nyuki ilikuwemo asali iliyomfaa Samson na familia yake.

- Kuna vitu au changamoto kwenye maisha yetu tunaziona kama simba ambaye anataka kutudhuru, lakini habari njema ni kwamba nguvu ya Mungu inaweza kuingilia kati na kusababisha zisiwe na madhara; lakini Mungu haishii hapo, anaweza kusababisha muujiza wako utokee hapo hapo ambapo panaonekana kama vile pana changamoto!

- Kuna vitu tunaviona kama mizoga lakini Mungu anataka avitumie hivyo hivyo kututolea chakula.

- Kwa hiyo, Samson angeogopa simba na kumkimbia, sio tu angejikosesha asali yeye, bali angewakosesha na wengine pia asali.

MAHALI ULIPO KUNA HALI FULANI ZINAONEKANA KAMA SIMBA, lakini mwisho wake kitatoka chakula; ukizikimbia unakimbia CHAKULA CHAKO.

Waamuzi 14:14 “Naye akawaambia, Katika huyo mwenye kula kikatoka chakula, Katika huyo mwenye nguvu ukatoka utamu.”

- Katika kile ambacho kilionekana kama hakifai [mzoga] kilitoka kinachofaa [asali]

- Katika kile ambacho kilionekana kama kinatisha na kinaweza kusababisha madhara [Simba] kilitoka kinachofaa [Chakula/asali]

- Katika kile kilichoonekana kama kinaweza kumla/kummeza samson, kilitoka chakula cha Samson.

- Katika hiyo kazi/biashara/huduma nk inaonekana kama hakuna cha kufaa, lakini maadam uko na mkono wa MUNGU, hapo hapo kitatoka chakula chako na familia yako.

- Kuna hali za maisha zinaonekana kama ni simba kutushambulia, au kama ni mizoga hazina faida kwetu, lakini kutokea humo humo Mungu atatutendea mema.

- Katika kila jambo unalopitia, bila kujali liko katika hali gani, Mungu anaweza kugeuza na kukutolea chakula hapo hapo.

Warumi 8:28 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”

Romans 8:28 AMP “And we know [with great confidence] that God [who is deeply concerned about us] causes all things to work together [as a plan] for good for those who love God, to those who are called according to His plan and purpose.”

- Katika kila jambo unalopitia, wema wa Mungu kwa ajili yako unaweza ukatokea humo.

- Katika mambo yote, Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao

Tafsiri hiyo ya andiko hilo la Rum 8:28 kwa tafsiri ya AMPLIFIED linasema kuwa:-

Na tunajua [kwa ujasiri mkubwa] kwamba Mungu [ambaye anajishughulisha sana nasi] husababisha vitu vyote kufanya kazi kwa pamoja [Kama ilivyopangwa] kwa ajili ya mema kwa wanaompenda Mungu, Hao walioitwa kwa kusudi na mpango wa wake.

- Kwa kila unacho kipitia, maadam mkono wa Mungu uko nawe, Mungu mwenyewe hufanya kazi kukupatia wema wake kupitia changamoto hiyo.

KWA HIYO SITAOGOPA SIMBA NINAOWAONA, MAANA NDANI YAO KITATOKA CHAKULA CHANGU NA FAMILIA YANGU.

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!