Text

Mungu Husababisha Mambo Yote Kufanya Kazi Kwa Pamoja Kukupatia Faida [Wema].

3 views 1 day ago

Warumi 8:28

“Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”

 

Kabla ya kuandika kile ninachokiona kwenye NENO hilo, ninaweka hapa tafsiri ya Kiswahili ANDIKO hilo kutoka katika AMPLIFIED BIBLE:

Romans 8:28

“And we know [with great confidence] that God [who is deeply concerned about us] causes all things to work together [as a plan] for good for those who love God, to those who are called according to His plan and purpose.”

 

Nasi twajua [tukiwa na ujasiri mkuu] kwamba MUNGU [ambaye anajihusisha sana na mambo yetu] husababisha vitu vyote kufanya kazi kwa pamoja [kama vilivyopangwa] kwa wema kwa ajili ya wale wampendao Mungu, kwa wale walioitwa kwa ajili ya kusudi na mpango Wake.

TUNAWEZA KUSEMA PIA:

Nasi tunajua, na tuna ujaisiri mkuu juu ya hilo, kwamba MUNGU, AMBAYE ANAJISHUGHULISHA SANA NA MAMBO YETU, husababisha vitu vyote [katika kila eneo la maisha yetu] vifanye kazi kwa pamoja [kama vilivyopanwa] kwa KUSUDI LA KUZALISHA JAMBO JEMA KWA AJILI YA WATU WANAOMPENDA MUNGU NA KWA AJILI YA WALE WALIOITWA KWA KUSUDI NA MPANGO WA MUNGU.

 

Naamini hata kama sijatafsiri zaidi, tayari umeshaona kile ninataka uone katika tafakari ya leo.

YAANI, TUNAJUA KWA UJASIRI WOTE, BILA MASHAKA YOYOTE, HATA KAMA KWA NJE TUNAONA VITU FULANI KAMA HAVIKO SAWA, LAKINI TUNAJUA KWA UJASIRI KWAMBA, MUNGU ANAYEJISHUGHULISHA SANA NA MAMBO YETU YOTE; YEYE ATASABABISA VITU VYOTE AU MAZINGIRA YOTE [HATA KAMA YANAONEKANA SIO MAZURI] YAFANYE KAZI KWA KUTEGEMEANA [IN HARMONY] KWA LENGO MOJA TU LA KUZALISHA WEMA KWA AJILI YA WATU WANAOMPENDA MUNGU.

 

Ni sawa na gari inayotembea. GARI KUTEMBEA NI MATOKEO YA VITU VYOTE KATIKA GARI (matairi, engine, bodi, usukani, nk) KUFANYA KAZI KWA PAMOJA/KUSHIRIKIANA KWA AJILI YA KUZALISHA MWENDO ambao ndio unatusababisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa urahisi.

 

Ukitenga kitu kimoja kimoja katika gari, unaweza usielewe kwamba hivi vitu vyote vikiwekwa pamoja vinaweza kusababisha GARI KUKUBEBA NA KUTEMBEA [wema].

Ukiona matairi peke yake utagundua huwezi kupanda tairi [so huwezi kuuona wema wa gari], ukiona injini peke yake, huwezi kupanda injini peke yake, ukiona vipande vya bodi peke yake huwezi kuona kama vinaweza kukubeba au huwezi kuona kama kuna jema lolote. LAKINI HIVYO VITU VYOTE VIKIFIKA MIKONONI MWA INJINIA WA TOYOTA ANAYETENGENEZA MAGARI, ATAVIUNGANISHA HIVYO VYOTE NA ATAVIFANYA VITU VYOTE KUFANYA KAZI KWA PAMOJA NA KUZALISHA GARI ZURI AMBALO LINAKUFAA.

 

Ndivyo ilivyo kwenye maisha, UKIANGALIA JAMBO MOJA MOJA LINALOTOKEA KATIKA MAISHA YAKO, UNAWEZA USIONE WEMA AMBAO UTAZALIWA. LAKINI YUKO MUNGU AMBAYE "husababisha vitu vyote kufanya kazi kwa pamoja [kama vilivyopangwa] kwa wema kwa ajili ya wale wampendao yeye"

Hiyo situation unaiona hivyo kwa sababu unaiangalia ikiwa imejitenga peke yake (isolated); kuna upande wa pili ambao inawezekana hauoni, hivyo vyote vikifika MIKONONI MWA MUUMBAJI/MFINYANZI atatoa kitu CHEMA KWA AJILI YAKO. KWA HIYO, USIOGOPE, MAANA NENO LA MUNGU LIMETUHAKIKISHIA KUWA "katika mambo yote [YAKIWEMO NA HAYO YA KWAKO] Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema"

 

Zaburi 37:37 “Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.”

Mwisho wa hilo unalopitia na unaona kama hakuna wema, mwisho wake ni AMANI, Mwisho wake utauona wema wa Mungu.

MAADAMU UNAMPENDA MUNGU, USIWE NA HOFU, KILA KINACHOENDELEA KWA AJILI YAKO, KILA VIKAO WANAVYOKAA KWA AJILI YAKO, KILA WANACHOFANYA KWA AJILI YAKO, MUNGU ATAKISABABISHA KUKUZALISHIA WEMA. 

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!