Text

MWANANGU NIPE MOYO WAKO (NAFASI YA MOYO NA MUDA) - SEHEMU YA 3

1 views 1 day ago

Mithali 23:26
Mwanangu, nipe moyo wako; 
Macho yako yapendezwe na njia zangu.

Ndani yangu nasikia Neno linasema "Mwanangu nipe moyo wako" 
Mungu anakusihi, mpatie moyo wako, mrejeshee tena moyo wako. 
Kuna watu tulikuwa tumempatia Mungu mioyo yetu lakini badae tukamnyang'anya na kuwapatia watu au vitu vingine. 
Hakuna mtu anapaswa kupewa nafasi ya kwanza kwenye mioyo yetu, MUNGU NDIO ANAPASWA KUPEWA NAFASI YA KWANZA MIOYONI MWETU. 
MOYO WAKO ULIKUWA KWA MUNGU LAKINI SASA HAUKO KWA MUNGU. 
MAISHA YAKO NA ROHO YAKO NI SHAHIDI KWAMBA YEYE HANA TENA ILE NAFASI ALIYOKUWA NAYO MOYONI MWAKO NA HIYO INAONEKANA WAZI KWENYE MUDA NA RATIBA YAKO. 
Zamani, yeye Mungu ndio alikuwa KIPIMO cha kila unachoamua na kukifanya, KAMA HAKIMPENDEZI NA KUMTUKUZA MUNGU, hata kama kinafurahisha, ULIKIACHA KWA GHARAMA YOYOTE ILE. 
MTU YEYOTE AMBAYE UMEMPA MOYO WAKO:-
--UTALIPA GHARAMA KUMPENDEZA
--KUNA MAMBO UTAJIZUIA KWA AJILI YAKE. 
--UTAMFIKIRIA YEYE KABLA YA KITU/WATU WENGINE
--ATAPATA NAFASI KWENYE RATIBA NA MUDA WAKO
Mungu anatusihi, TUMPATIE NAFASI YAKE ILIYOPOTEA KWENYE MAISHA YETU, TUANZE KUISHI TENA KWA AJILI YAKE NA SIO KWA NAFSI ZETU. 
Malaki 1:6 Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi?
Kama kweli bado tunasema Mungu ni baba yetu, IKO WAPI HESHIMA YAKE KWENYE MAISHA YETU? MAISHA TUNAYOISHI YANAMUHESHIMU MUNGU AU YANAMUAIBISHA? IKO WAPI NAFASI YAKE KWENYE MUDA NA RATIBA ZETU? IKO WAPI NAFASI YAKE KWENYE TABIA ZETU? 
Kwenye andiko hilo anasema, Mwana humuheshimu Baba yake. Hakuna uwana bila heshima kwa Baba. Lakini pia anasema, Mtumishi humcha Bwana wake, kwa hiyo HAKUNA UTUMISHI BILA KUMCHA BWANA.
Utumishi wa kweli na wenye faida HAUKO KWENYE KUFANYA KAZI YA MUNGU (KUHUBIRI, KUIMBA, KUTOA, KUJITOA NK) BALI UNAANZIA KWANZA KWENYE KUMCHA MUNGU (KUWA NA UHUSIANO MZURI NA MUNGU, MIOYO YETU KUWA SALAMA KWAKE KWANZA) NDIPO KAZI TUNAZOMFANYIA ZITAKUWA NA MAANA. 
Kuna watu bado wanaenda kanisani, wanaimba, wanafanya kazi za kanisa, wanahubiri, wanajitoa kwa nguvu zao lakini MIOYO YAO HAWAMCHI MUNGU TENA, MIOYO YAO HAWAJAMPATIA MUNGU, MIOYO YAO WAMEWAPA WATU AU VITU. HIYO HI HATARI. LEO MUNGU ANASEMA, MWANANGU NIPE TENA MOYO WAKO. 
Mathayo 15:8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.
Ishara ya nje kwamba umepoteza nafasi kwenye moyo wa mtu, ni kupoteza nafasi kwenye muda wake na ratiba zake.
Hata kama bado anakuambia kwa maneno, upo kwenye moyo wangu bado, lakini kama HAUKO KWENYE RATIBA ZAKE, ujue KUNA NAFASI IMEPOTEA AU IMEANZA KUPOTEA KWENYE MOYO WAKE. 
KILA ALIYE NA NAFASI KWENYE MOYO WA MTU, ANAYO NAFASI KWENYE RATIBA YA MTU, HATA KAMA HIYO RATIBA NI NGUMU KWA KIWANGO GANI. 
Vivyo hivyo, ishara ya nje kwamba Mungu amepoteza nafasi kwenye moyo wako, ni nafasi tunayompatia kwenye MUDA NA RATIBA ZETU, na sio kwa MANENO YAKO MATAMU tunayosema kwamba Mungu wewe ni namba moja kwangu. 
HATUWEZI KUUONA MOYO WAKO LAKINI TUNAZIJUA au TUNAWEZA KUZIONA RATIBA ZAKO. 
Kwa ujumbe huu Mungu anakuuliza, NAFASI YANGU IKO WAPI KWA MOYO WAKO? MBONA UMENINYANG'ANYA MOYO WAKO? MBONA HUNIPI MUDA WAKO? MBONA SIKO KWENYE RATIBA ZAKO? MBONA MIMI SIO KIPAUMBELE CHAKO TENA? 
Namuomba Mungu akusikizishe sauti hii ya Neno lake ninayoisikia ndani yangu ikisema, "MWANANGU NIPE MOYO WAKO" na sauti hii isiondoke moyoni mwako mpaka UMPATIE MUNGU TENA MOYO WAKO, UMPATIE TENA NAFASI YAKE KWENYE MAISHA YAKO, UMPATIE TENA HESHIMA YAKE.
Kama anasema "Mwanangu, nipe moyo wako;
Macho yako yapendezwe na njia zangu" maana yake ni kwamba:-
--Unao uwezo juu ya moyo wako (You have control of your heart) 
Moyo wako ni wako na wewe mwenyewe unao uwezo juu yake kuamua uuelekeze kwa nani au wapi, au kwa lugha nyingine maisha yako ni yako na unaweza kuamua yamuelekee Mungu au la. 
--Unawajibika kwa popote ambako moyo wako uko. 
Kama kuna mtu au vitu vimeuondoa moyo wako kwa Mungu, usitafute kujitetea, jiwajibishe kwa sababu ni wewe ulimpatia hiyo nafasi, usitafute vijisababu, beba wajibu na chukua hatua. 
Kuna watu, mioyo yao iliondoka kwa MUNGU baada ya kuwa wamekutana na watu au mtu fulani na wakaanza kuhusiana nao kwa namna isiyo sahihi na hao watu wakaitoa mioyo yao kwa Mungu, lakini ukweli ni kwamba ni wewe ndiye ulitoa hiyo nafasi. 
Kuna watu, kazi, biashara, vitu au shuguli fulani ndio iliwasababisha mioyo yao ikatoka kwa Mungu, yaani kazi/biashara/vitu vimemfanya akose kabisa nafasi kwa Mungu na badala ya kubeba wajibu amekuwa na visingizio vingi vya kazi nyingi, mambo mengi badala ya kubeba wajibu na kurekebisha. 
--Unao uwezo na uhuru wa kumpatia au kumnyima Mungu moyo wako. 
Anaposema nipe moyo wako, anakupatia uhuru wa kutumia UTASHI WAKO KUFANYA MAAMUZI. Kuna watu huwa wanasema, kama ni mapenzi ya Mungu basi Mungu atanifanya nifanye hivi. Ukweli ni kwamba Mungu huwa hafanyi kazi hivyo, Mungu siku zote anafanya kazi na UTASHI WETU. MUNGU HUWA HAENDI ZAIDI YA UTASHI NA UTAYARI WAKO. 
Kwa andiko hilo ni wazi kabisa, Mungu yuko tayari kwa mioyo yetu, ni wazi anaitamani mioyo yetu, ni wazi tunayo nafasi kwake inayotusubiri lakini ni wazi pia kuwa AMETUPATIA UHURU WA KUAMUA NA KUCHAGUA. 
Maandiko yanasema katika Kumbukumbu la Torati 30:19b "... nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
Anataka tuchague baraka na uzima, lakini hatulazimishi isipokuwa anatusihi.
Anataka mioyo yetu, lakini anatuambia SISI TUFANYE MAAMUZI KUMKABIDHI MIOYO YETU. 
--Kama unaweza kumpa Mungu unaweza kumpa mtu mwingine pia au kuvipatia vitu vingine moyo wako. 
Neno la Mungu linasema katika Mithali 31:3 "Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme." 
Kwa hiyo, sisi tunao uwezo wa kumpatia Mungu nafasi ya kwanza au kuwapatia watu nafasi hiyo. 
Kuna watu tunawapa nafasi kwenye maisha yetu, na tangu tumewapatia hizo nafasi, wamechukua na nguvu zetu za kiroho za kuhusiana na Mungu. 
Hilo andiko linazungumzia wazi kabisa kuhusu maswala ya MAHUSIANO NA WATU WASIO SAHIHI. 
Kuna watu tumewapa nafasi maishani mwetu, WAMETUNYONYA NGUVU ZETU ZA KIROHO NA PIA WAMEHARIBU NA MIOYO YETU MBELE ZA MUNGU. 
Hatuna tena nguvu za kiroho (kukaa uweponi mwa Mungu, kuomba, kumtafuta Mungu, kufunga nk) lakini pia WAMEHARIBU MIOYO YETU. HATA WEWE NI SHAHIDI, KWAMBA WEWE SIO YULE AMBAYE UNAJIFAHAMU (You are the witness of yourself that you are not the one you used to be), MOYO WAKO UMEHARIBIKA, NA KUNA MTU AU WATU ULIWAPA NAFASI KUUHARIBU MOYO WAKO. 
SAUTI HII ISIKIKE NDANI YAKO NA MOYONI MWAKO IKILIA NA KUSEMA, "MWANANGU NIPE TENA MOYO WAKO" 
2 Wakorintho 5:20 Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.
Mungu anakusihi kupitia ujumbe huu kwamba, upatanishwe tena na yeye, umpatie tena nafasi yake, umpatie tena MOYO WAKO. 
--Ukimpa Mungu moyo wako, itageuza mtazamo wako.
Utaanza kupendezwa na njia za Mungu, ni wazi kwamba ukiona NJIA ZA DUNIA (TAMAA ZA MAMBO YA KIDUNIA NA MAMBO YASIYOMPENDEZA MUNGU) NDIO ZINAKUFURAHISHA ZAIDI UJUE MOYO WAKO HAUKO KWA MUNGU. 
Hata kama njia za dunia zinasisimua lakini hazitakufurahisha moyo wako kama moyo wako uko kwa Mungu, hautajifurahisha katika dhambi, UTAKUWA TAYARI KULIPA GHARAMA KUTOKA KWENYE NJIA ZISIZO SAHIHI. 
Mithali 23:26 Mwanangu, nipe moyo wako; 
Macho yako yapendezwe na njia zangu.

Kwa ujumbe huu Mungu anakusihi ufanye maamuzi sasa, amua kumpatia Mungu nafasi yake tena. 
Amua kumpatia HESHIMA YAKE KWENYE MAISHA YAKO. 
Amua kumrudisha tena na kumpa kipaumbele kwenye RATIBA ZAKO. 
Amua kumpatia kipaumbele KWENYE MAAMUZI YAKO. 
Amua KUMPATIA TENA KIPAUMBELE KWENYE MUDA WAKO. 
Itikia wito huu mkuu, "MWANANGU NIPE MOYO WAKO, MACHO YAKO YAANZE KUPENDEZWA NA NJIA ZANGU TENA."
 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

#Umebarikiwa
~Na Mwl. Francis Langula 

+255754711247

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!