Text

Mwenyewe Aliutwaa Udhaifu Wetu (Kama Aliutwaa Mimi Sina)

1 views 1 day ago

Mathayo 8:16-17 SUV
"Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu."

so that He fulfilled what was spoken by the prophet Isaiah: “He Himself took our infirmities [upon Himself] and carried away our diseases .” MATTHEW 8:17 AMP

Neno la Mungu linasema "Mwenyewe (yaani Yesu) aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu."

Tafsiri ya kiingereza inasema "He Himself took our infirmities [upon Himself] and carried away our diseases."

Neno halisemi "ATAUTWAA (BAADAYE TUKIAMINI) UDHAIFU NA KUYACHUKUA MAGONJWA" linasema "ALIUTWAA UDHAIFU NA KUYACHUKUA MAGONJWA (YAANI ALISHACHUKUA HAYO ZAMANI)".

Kwa hiyo, tukiongea kwa mifano, kama ugonjwa na udhaifu ni KITU CHA KUSHIKIKA MIKONONI MWANGU, maana yake ni kwamba, YESU ALIKICHUKUA HICHO KITU TOKA MIKONONI MWANGU, ANACHO YEYE.

Kwa hiyo, KAMA ANACHO YEYE MIMI SINA.

HAWEZI KUWA NACHO YEYE NA MIMI NINACHO KWA WAKATI HUO HUO. KWA HIYO NI MAWILI, EITHER NINACHO MIMI AU ANACHO YEYE, HAIWEZEKANI SOTE TUWE NACHO.

NA NENO LA MUNGU LINASEMA ANACHO YEYE, KWA HIYO MIMI SINA.

Yaani, "Mwenyewe (yaani Yesu) aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu."

If He took, I don't have...

Neno la Mungu linasema katika Warumi 3:4 "Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo;"

Kila kitu ni kinachoniambia kinyume na Neno hili  "Mwenyewe (yaani Yesu) aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu" ni uongo, na kila mtu anayeniambia kinyume na Neno la Mungu "Mwenyewe (yaani Yesu) aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu", ni mwongo; na Kila taarifa inayosema au itakayosema eti "Mwili wangu una ugonjwa au udhaifu", hiyo ni taarifa ya uongo sitaiamini.

If He took, means He took! Mungu anasema alichomaanisha na anamaanisha alichokisema, Mungu huwa hatanii au haropoki!

Nimegundua hata mwili wangu unaweza kunidanganya kwamba una ugonjwa kumbe alishauchukua Yesu zamani,maumivu yanaweza kunidanganya, hisia zangu zinaweza kunidanganya....

Nimeelewa alichosema Yesu kwamba aliutwaa udhaifu wangu, na ninajua alimaanisha wala si utani, "NA NIMEAMUA KUMUAMINI YEYE BILA KUJALI CHOCHOTE", bila kujali hata kama anayesoma meseji hii anaweza akaniona kama kichaa.

"Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona." 2 Wakorintho 5:7 SUV

Kila atakayefikia hatua hii ya kumuamini Mungu na kuliamini Neno lake, HAWEZI KUBAKI NA UGONJWA WOWOTE kwa majina yake; Iwe kansa, vidonda vya tumbo, UKIMWI, magonjwa ya figo, malaria, na mwingine wowote.

Kuanzia sasa hivi usijione mgonjwa, ona ugonjwa huo alishauchukua Yesu maana hiyo ndio kweli.

Kama ameutwaa, na umeshawishika ndani yako hauna wewe anao Yesu, ishi na uongee kama asiye nao, kwa sababu hauna, anao Yesu!

Jione kama anavyokuona Yesu!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!