Ndani ya Mungu Pekee Ndio Tunaweza Kuishi
Matendo ya Mitume 17:28
“Kwa maana ndani yake Yeye [MUNGU] tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.”
Mambo ya kujifunza:
Kwa maandiko hayo ina maana, NJE YA MUNGU HUWEZI KUISHI, HUWEZI KWENDA KATIKA KUSUDI LA MUNGU NA HAUNA UHAI NDANI YAKO
KUISHI MAISHA DUNIANI KIKAMILIFU KUNAWEZEKANA TU UKIWA NDANI YA MUNGU. VINGINEVYO UTAKUWA UNASOGEZA SIKU LAKINI HAUISHI KIKAMILIFU MAANA NENO LA MUNGU LINASEMA katika
Marko 8:36 "Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?"
Nje ya Mungu hata kama unaweza ukaona unaishi na umefanikiwa kwa viwango vya dunia hii, bado haina faida kwa sababu UTAPATA HASARA YA NAFSI YAKO.
“Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” Yohana 15:5 SUV
Pasipo Mungu/Yesu sisi hatuwezi kufanya neno lolote; kwa hiyo kama kuna jambo AU NENO unalifanya nje ya YESU, linahesabiwa kuwa si lolote mbele za Mungu kwa sababu pamoja na hilo NAFSI YAKO ILIYO YA THAMANI KULIKO VYOTE itapotea.
Kwa hiyo ni vizuri KULIFANYA JAMBO LA KWANZA, KWANZA ili kile unachokifanya baadaye kiwe na thamani mbele za MUNGU; NA JAMBO LA KWANZA NI KUMPA MUNGU NAFASI YAKE KWANZA, ILI KUISHI KWETU, KWENDA KWETU NA UHAI WETU UWE NA FAIDA.
TUNAISHIJE, TUNAENDAJE NA TUNAKUWAJE NA UHAI WETU NDANI YAKE MUNGU?:
1) KWA KUMPOKEA YESU KAMA MWOKOZI WA MAISHA YETU [KUOKOKA]
1 Yohana 4:15 SUV
“Kila akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu.”
2) KWA KULIISHI NENO LA MUNGU
1 Yohana 3:24 (SUV)
“Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.”
3) KWA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU
1 Yohana 4:13 (SUV)
“Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake.”
4) KWA KUKAA KATIKA UPENDO NA WANAOTUZUNGUKA
1 Yohana 2:10
“Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.”
Yohana 1:4 SUV
“Ndani yake [Mungu] ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.”
5) KWA KUISHI MAISHA YA USHINDI DHIDI YA DHAMBI
1 Yohana 3:6 SUV
“Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.”
HABARI NJEMA YA UFALME NDIO HII NIMESHAKUTANGAZIA, KAZI KWAKO KUJIINGIZA KWA NGUVU.
Luka 16:16 (SUV) Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author