Text

Neema ya Mungu

1 views 1 day ago

Tito 2:11-12 SUV

“Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;”

MAMBO YA KUJIFUNZA:

--Neema ya Mungu ni uwezesho wa Ki-Mungu kwenye maisha ya mtu.

--Neema ni kibali [Favor] cha Mungu kwenye maisha ya mtu.

--Neema ni kupokea usichostahili bila gharama yoyote!

Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa

--Neema ya wokovu imefunuliwa kwa kila mtu, yaani uwezesho wa Ki-Mungu kukuokoa au Kibali cha Mungu kuokoa kimefunuliwa kwa wanadamu wote!

Mtu akiikubali Neema inamuokoa!

Nayo [Neema] yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa

--Neema haiishii kukuokoa tu bali INAKUFUNDISHA PIA!

NEEMA INAKUFUNDISHA KUKATAA!

--Mtu mwenye neema ya Mungu ana uwezo wa kusema HAPANA kwa dhambi. 

Grace says NO to sin!

--NEEMA inakuwezesha kuishi maisha ya KIASI, HAKI NA UTAUWA katika ULIMWENGU HUU HUU WA SASA!

--Kuna watu wanasema ulimwengu huu huwezi kushinda dhambi, hawajaijua nguvu ya Neema, Neema inaweza kukupa uwezo wa kushinda katika ulimwengu huu wa sasa

--Kuna watu wanaishi maisha ya dhambi kwa kisingizio kuwa tunaishi kwa neema, huko ni kutoifahamu Neema ya Mungu

--Kama unafikiri huwezi kuishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi basi hujaijua nguvu ya Neema.

Tatizo ni kwamba, INGAWA NEEMA IMEFUNULIWA KWA WATU WOTE, lakini itawasaidia WATAKAOIPOKEA NA KUKUBALI KUKUA KATIKA NEEMA!

“Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.” 2 Petro 3:18 SUV

Lakini pia tuwe na HODARI KATIKA NEEMA

“Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.” 2 Timotheo 2:1 SUV

KAMA UNAKAA UNASUBIRI MAMBO YAENDE au YAJIENDESHE YENYEWE SAHAU UWEZESHO WA NEEMA, neema inawasaidia walio hodari katika hiyo!

Kama umepokea Neema tayari, fanya mambo yatokee usiyasubiri, fanya kitu... Fanya sehemu yako na unapoishia Mungu ataachilia uwezesho wake!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!