Text

Neno la Kukuvusha (Kukuokoa) Kutoka Kwenye Hali Unayopitia Sasa Haliko Mbali Nawe

2 views 1 day ago

Warumi 10:8

Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.

Jambo hili Mungu ameliweka ndani yangu kwa nguvu sana, ninajua ni Neno la wakati. 

Andiko nililonukuu, limesema wazi kwenye kipengele cha kwanza kwamba "Lile neno li karibu nawe"  na kwenye kipengele cha mwisho kwamba "ni lile neno la imani tulihubirilo" 

Na katikati yake kuna maneno yafuatayo "katika kinywa chako, na katika moyo wako" 

Kwa sasa sitaongelea maneno hayo ya katikati bali nitaongelea kipengele cha kwanza na cha mwisho... 

Anaposema "lile Neno", ukisoma mistari kadhaa inayofuata (Warumi 10:9-10) utagundua anaongelea NENO LA WOKOVU au kwa lugha rahisi NENO AMBALO LINAWEZA KUSABABISHA WOKOVU.

Sasa ukiunganisha kipengele cha kwanza na cha mwisho kwenye andiko hilo utagundua kuwa ni sahihi kabisa kusema andiko hili linasema "Neno la imani lililohubiriwa ambalo LINAWEZA KUSABABISHA WOKOVU (KUKUOKOA) LIKO KARIBU NAWE (HALIKO MBALI) " 

Hilo neno WOKOVU lina maana zifuatazo:-

- Ustawi 

- Mafanikio 

- Ukombozi, 

- Uhifadhi au Kuhifadhiwa 

- Usalama (Kimwili, Kimaadili na kiroho), 

- Uzima MKAMILIFU 

- Afya                                                          

- Wokovu wa baadaye, 

- Jumla ya faida na baraka ambazo Wakristo, waliokombolewa kutoka katika maovu yote ya kidunia, watafurahia baada ya kurudi kwa Kristo kutoka mbinguni katika ufalme uliokamilika na wa milele wa Mungu.

Kwa Hiyo, tukirudi kwenye kuliangalia kwa undani andiko letu la msingi huku tukizingatia nilichofundisha juu pamoja na tafsiri ya WOKOVU tunagundua maana ya andiko letu la msingi nililo nukuu ni hii;

"Neno linaloweza kusababisha wokovu (kuokoka kwetu), linaloweza kusababisha maisha yetu kustawi, mafanikio, ukombozi kutoka kwenye kila aina ya kifungo, kuhifadhiwa kwetu, usalama (ulinzi) wetu wa kimwili, kiroho na kimaadili, uzima na afya zetu, uhakika wa mbingu baada ya kurudi kwa Yesu au baada ya maisha haya nk.; liko karibu nasi."

HILO NENO LINALOWEZA KUFANYA HAYA YOTE

--LIKO KARIBU (HALIKO MBALI) NA WEWE 

--LIMESHAHUBIRIWA AU LINAUBIRIWA (UNAYO NAFASI YA KULISIKIA) MARA KWA MARA

--NI NENO LA IMANI

Warumi 10:8 a&c "... Lile neno li karibu nawe,.... yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo."

Neno la Mungu ni kweli, hata hili Neno ni kweli kabisa. 

Ninachomaanisha ni nini? Kila NENO AMBALO LINAWEZA KUSABABISHA jibu unalohitaji, kwa namna moja ama nyingine HALIKO MBALI NAWE, LIKO KARIBU NAWE. 

Wakati Roho Mtakatifu ananifundisha tafakari hii, alinikumbusha baadhi ya mafundisho ambayo mimi nimewahi kufundisha na haya yote yapo na wengi wanaosoma ujumbe huu nimewahi kuwatumia, NA YAKO KARIBU NA WAO. 

Nitataja BAADHI YA MAFUNDISHO NLIYOWAHI KUFUNDISHA:-

  1. MAPENZI YA MUNGU KUPONYA 
  2. MILANGO AMBAYO MAPEPO YANAWEZA KUTUMIA KUMUINGIA MTU
  3. MOYO MGUMU
  4. NGUVU YA KUKUMBUKA
  5. NAMNA YA KUTOA MIILI YETU KAMA DHABIHU 
  6. ROHO MTAKATIFU 
  7. USIOGOPE AMINI TU 
  8. NGUVU ITENDAYO KAZI NDANI YETU
  9. MTAZAMO SAHIHI KUSHINDA KILA AINA YA CHANGAMOTO 
  10. MSALABANI - YESU ALICHUKUA DHAMBI, HATIA, AIBU NA KUKATALIWA KWETU 
  11. MAFUTA YA ROHO MTAKATIFU KWA AJILI YA KAZI/BIASHARA 
  12. AMINI BILA KUONA
  13. SHIKA SANA ULICHONACHO
  14. MAFANIKIO - NAMNA YA KUFANIKIWA KWA MISINGI YA NENO LA MUNGU 
  15. HOMA IKAMUACHA - UPONYAJI 
  16. KANUNI ZA FEDHA KIBIBLIA 
  17. KIONGOZI MZURI WA KIROHO NI MFUASI MZURI
  18. NINAISHI KUDHIHIRISHA ISHARA NA AJABU ZA MUNGU 
  19. NAMNA SAHIHI YA KUMTOLEA MUNGU ILI KUTULETEA MATOKEO 
  20. MTAKENI BWANA NA NGUVU ZAKE 
  21. JIFUNZE KUJITOFAUTISHA SABABU UMETOFAUTISHWA 
  22. ROHO MTAKATIFU NA UPONYAJI WA KILA NAFSI ILIYOJERUHIWA 
  23. MUNGU ANAKUTAKA KWENYE CHUMBA CHA MAOMBI 
  24. NGUVU YA IMANI INAYOENDESHA MAISHA 
  25. ROHO MTAKATIFU NA MOTO WA MADHABAHU 
  26. ROHO SABA ZA MUNGU 
  27. SAUTI YA MUNGU KATIKA WAZO LA KAWAIDA
  28. NAMNA YA KUTAMBUA KUSUDI LA KUISHI 
  29. MAANA NA NGUVU YA IMANI
  30. SHIKA SANA ULICHO NACHO 
  31. UTOSHELEVU WETU UKO NDANI YA MUNGU PEKEE

Hayo ni baadhi ya mafundisho ya sauti (audio) ni sawa kabisa na alichosema Paulo, "Lile neno li karibu nawe".... "ni lile neno la imani tulihubirilo" 

Ukifuatilia hayo mafundisho yote, utagundua NI NENO LA WOKOVU, na YANAGUSA KARIBU KILA ENEO LA MAISHA, na yote hayo YAPO YANAWEZA KUPATIKANA MUDA WOWOTE (HATA SASA) LAKINI PIA WENGI WANAONIFUATILIA WANAYO HATA KWENYE SIMU zao (YAKO karibu na wao) na wakati huo huo unaweza kukuta mtu ana JAMBO linamsumbua na KUMBE LINA JIBU KABISA KWENYE MAFUNDISHO ALIYONAYO KARIBU... 

Sasa nimezungumzia MAFUNDISHO NILIYOFUNDISHA MIMI KAMA MFANO TU... 

 

Ukweli ni kwamba, UKIFUATILIA:- 

--VITABU ULIVYO NAVYO AU ULIVYO WAHI KUNUNUA NA HAUJAVISOMA, 

--MASOMO (NOTES) ULIYOWAHI KUANDIKA UKIWA UNAFUNDISHWA KANISANI KWAKO NA HAUJAYAPITIA WALA KUYAFANYIA KAZI, 

--MAAGIZO AMBAYO ROHO MTAKATIFU ALIKUPATIA UYAFANYIE KAZI NA UKAISHIA NJIANI

--MAELEKEZO AMBAYO ULIYAPATA ULIPOKUWA UKISOMA NENO

--MAHUBIRI AMBAYO UMEWAHI KUFUNDISHWA KANISANI, KWENYE SEMINA, MAKONGAMANO NK

Utagundua, ndani ya hayo yote ukiwa makini, KUNA WOKOVU UNAOHITAJI KWENYE KILA ENEO LA MAISHA YAKO. KUNA MAJIBU YA MAMBO AMBAYO YAMEKUKWAMISHA... 

Sasa turudi kwenye ANDIKO LETU LA MSINGI

Warumi 10:8 Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.

Kipengele cha katikati ya andiko hilo kinasema "katika kinywa chako, na katika moyo wako" 

Ili kuelewa kipengele hiki, ni muhimu angalia mistari inayofuata.

Na hapa ndio tutaweza kuona KWANINI HILI NENO LA WOKOVU LILILO KARIBU NASI HALITULETEI MATOKEO PAMOJA NA KWAMBA LI KARIBU NASI. 

Warumi 10:9-10 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Wokovu (kwa maana niliyotoa hapo juu) sio matokeo ya NENO LA WOKOVU KUWA KARIBU NAWE, BALI NI MATOKEO YA LILE NENO KUZALISHA IMANI MOYONI KISHA IMANI MOYONI KUGEUZA UKIRI WAKO, NA MWISHO KUSABABISHA UTENDAJI WAKO KUWA SAWA NA UNACHOAMINI NA UNACHOKIRI... 

Wokovu (kwa maana niliyoitoa) sio matokeo ya kuwa na mafundisho mengi kwenye simu au laptop yako, sio matokeo ya kuwa na vitabu vingi kwenye maktaba yako, sio matokeo ya kuwa na notebook zilizojaa MASOMO, BALI NI MATOKEO YA KUSOMA NA KUSIKILIZA HILO NENO LA WOKOVU KARIBU NAWE (Sababu imani huanzia kwenye kusikia), MPAKA HILO NENO LIZALISHE IMANI NDANI (SIO KUONGEZA ORODHA YA MASOMO ULIYOSIKILIZA). Ndio maana linaitwa NENO LA IMANI.

KISHA IMANI IGEUZE LUGHA YAKO JUU YA JAMBO HILO

(YAANI UANZE KUONGEA LUGHA YA IMANI/WOKOVU JUU YA HILO) 

KISHA UANZE KUTENDA SAWA SAWA NA UNACHOKIAMINI 

Haya yakiwa mahali pake, NINAKUHAKIKISHIA, LAZIMA UTAANZA KUONA WOKOVU NA NGUVU YA NENO LA MUNGU KWENYE KILA ENEO LA MAISHA. 

Watu wengi wanayo masuluhisho karibu nao lakini tatizo ni kwamba WAMEKUWA WAVIVU KUSIKIA, WAVIVU KUSOMA, WAVIVU KUJIFUNZA... 

-- Hata ujumbe huu wengine wameshindwa kuusoma wote sababu ya huo huo UVIVU... 

Waebrania 5:11 Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia.

Mahali pengine Neno hili la wokovu huitwa NENO LA UNABII LILILO IMARA ZAIDI

2 Petro 1:19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.

Ukifanikiwa KULIANGALIA NENO HILO KAMA TAA ING'AAYO, LITAKUTOA KWENYE KILA GIZA LA MAISHA

Lakini, angalia sehemu ya mwisho ya andiko hilo inasema "na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu

Maana yake HILI NENO LITAZALISHA MATOKEO IKIWA TU LITAINGIA MOYONI MWA MTU NA KUFUATA KANUNI NILIZOELEZA JUU.

Warumi 10:8Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo

Nenda kwenye kila NENO (Mafundisho, masomo, vitabu nk) karibu nawe, hakikisha unafanya kila unachopaswa kufanya Neno liingie moyoni mwako mpaka ligeuze ukiri wako, uanze kutenda kwa imani, Nakuhakikishia UTAONA NAMNA AMBAVYO LINAKUVUSHA.

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

#Umebarikiwa

~Na Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!