Text

Neno la Mungu Katika Maombi na Utendaji wa Malaika

1 views 1 day ago

ZABURI103:20 (SUV)

"Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake."

Siku zote wako malaika walio hodari tayari tayari kwa ajili ya kulitenda Neno la Mungu.

Wako tayari kusikiliza sauti ya Neno la Mungu. 

Angalia kwa umakini, malaika hawalitendi andiko bali NENO, wanasikiliza SAUTI YA NENO!

MTENDAO NENO LAKE:

Unaposoma biblia unasoma maandiko, Roho Mtakatifu anapokupatia ufunuo wa kuutumia kwa wakati huu, andiko linageuka kuwa NENO, au Roho Mtakatifu anapokukumbusha andiko ambalo anataka ulitumie KATIKA changamoto fulani, maana yake ni kwamba andiko hilo limevikwa uhai au pumzi ya Mungu na ni NENO sasa!

Neno ni andiko lililovuviwa au lenye pumzi ya Mungu!

Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;” 2 Timotheo 3:16 SUV

Pumzi ya Mungu kwenye andiko ndio inalifanya andiko lililoandikwa miaka zaidi ya 1000 iliyopita kuwa hai leo (NENO) na kufanya kazi leo!

Na hilo NENO sasa ndio MALAIKA wako tayari kulitenda! 

SAUTI YA NENO LAKE:

SAUTI YA NENO ni AGIZO au MAAGIZO (orders) yanayobebwa na hilo NENO!

Sasa hayo maagizo ndio MALAIKA WAKO TAYARI KUYASIKILIZA NA KUYATEKELEZA!

Kwa hiyo, malaika wanasikiliza NENO NA KUTENDA AU KUTEKELEZA MAAGIZO (SAUTI) YAKE!

Mwl. Mwakasege alisema hivi, "Mungu akikupatia NENO, usiombe tu sawa na NENO hilo, tafuta kujua sauti ya Mungu pia kwenye NENO hilo"

Kwa hiyo ni WAJIBU WANGU NA WAKO kulisikia NENO ANALOLIACHILIA ROHO MTAKATIFU, KUJUA SAUTI au AGIZO YA HILO NENO, Yaani hilo Neno linataka lifanye nini kwenye hiyo changamoto na ndipo ulitumie kwenye maombi KUWAAGIZA MALAIKA KUFANYA UTEKELEZAJI!

Malaika ni roho watumikao, na ni NENO la Mungu na SAUTI YA MUNGU ndio huwatuma!

“Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?” Waebrania 1:14 SUV

MAOMBI NA NENO NA SAUTI YA NENO:

Kama KWENYE MAOMBI YAKO HAKUNA NENO WALA SAUTI AU MAAGIZO YA NENO, MALAIKA HAWATAKUWA NA JAMBO LA KUTEKELEZA maana wao wanalitii NENO na kusikiliza SAUTI AU MAAGIZO YA NENO PEKEE!

NDIO MAANA MUOMBAJI YEYOTE MWENYE MATOKEO MAZURI NI YULE ANAYETAFUTA KWANZA KWA ROHO MTAKATIFU NENO SAHIHI JUU YA JAMBO ANALOTAKA KULIOMBEA KABLA YA KUANZA KUOMBA!

Kabla ya kuanza kuomba, hakikisha Roho Mtakatifu anakupatia NENO SAHIHI la kusimamia, UKILIPATA NENO HILO, HAKIKISHA UNAJUA SAUTI YA MUNGU ndani ya hilo NENO KUHUSIANA NA JAMBO UNALOOMBEA; na ndipo uanze kuomba na KUWAAGIZA MALAIKA KUTEKELEZA MAAGIZO YA SAUTI YA MUNGU!

Kila Neno ambalo Mungu anakupatia, lina sauti nyuma yake kuhusiana na kile ambacho kwacho Mungu amekupatia andiko hilo!

Tunapoomba sawa na Neno La Mungu, tunawasikizisha sauti ya Neno Malaika na wanatenda sawa na Neno La Mungu tulilolitamka au kuliomba.

"Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake." Zaburi 103:20 (SUV)

Neno la Mungu linasema, hawa Malaika wako hodari sana kulitenda NENO na MAAGIZO YAKE!

Tuanze kuwatumia ipasavyo sawa na tafakari hii, tutaanza kuona matokeo ya maombi yetu!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!