Neno Limebeba Uzima na Afya ya Miili Yetu
Yohana 1:4-5
“Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.”
ISA 58:8 “Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara;”
MAMBO YA KUJIFUNZA:
Ndani ya NENO la Mungu umo uzima, huo uzima ndani ya neno ni NURU YA WATU, NURU hiyo inasababisa AFYA ITOKEE.
- Kumbe magonjwa mengine au kutokuwa na afya kwingine kunasababishwa na kukosa NENO LA MUNGU LA KUTOSHA KWENYE MAISHA YAKO.
- Kwa sababu UKO UZIMA NDANI YA NENO, kwa hiyo unapoongeza kasi yako ya kulijua Neno la Mungu unaongeza uzima ndani yako.
- JIEWEKEE UTARATIBU MAALUMU NA ENDELEVU WA KUSOMA NA KUJIFUNZA NENO LA MUNGU KILA SIKU BILA KUACHA; UTASHANGAA KIWANGO CHA UFAHAMU [NURU] WAKO KWENYE ENEO LA AFYA KINAONGEZEKA NA KIWANGO CHA KUTEMBEA KATIKA AFYA KITAONGEZEKA PIA.
- Kama unalisoma na kujifunza NENO na bado kuna maeneo ya AFYA YAKO yana changamoto, chukua hatua ya pili, fuatilia kwa makusudi kila NENO LINALOZUNGUMZIA UPONYAJI/AFYA, JIFUNZE KWA MAKINI HALAFU NG'ANG'ANIA HAKI YAKO YA KUWA MZIMA SAWA NA HILO NENO.
- Magonjwa sio fungu letu, yakija lazima yaondoke. MIILI YETU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU, NA SIO HEKALU LA MAGONJWA.
NA NDIO MAANA KATIKA NENO, MUNGU AMEWEKA UZIMA NDANI YAKE; KILA ANAYESOMA NA KUJUFUNZA ATAFURAHIA UZIMA ULIO NDANI YAKE.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author