Text

Nguvu ya Imani (The Power Of Faith)

1 views 1 day ago

Warumi 4:19-22

"Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara. Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.”

MAMBO YA KUJIFUNZA:

Warumi 4:19 “Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.”

--Imani ya Ibrahim, haikumfanya asione uhalisia wa hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, na uhalisia wa hali ya kufa ya tumbo la mke wake Sara.

--Alikuwa anaona kabisa kuwa, kwa hali ya asili ya mwili wake, hawezi kupata mtoto na kwa hali ya asili ya mke wake Sara hawezi kabisa kuchukua mimba... kwa hiyo imani yake haikumfumba macho asione uhalisia huo.

Warumi 4:20 "Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;"

--Lakini IMANI haikuishia kwenye uhalisia wa hali ya kufa kwa mwili wa Ibrahim na Sara; IMANI ilienda zaidi ya hapo...

--Hali halisi ya UGONJWA haiwezi kuiwekea mipaka IMANI.

--IMANI HAIWEKEWI MIPAKA NA UGONJWA AU HALI HALISI YA TATIZO

--IMANI HAIWEKEWI MIPAKA NA TAARIFA ZA MADAKTARI... SIO KWAMBA IMANI HAIONI HIYO REPORT, SIO KWAMBA HAIJUI TAARIFA INASEMA NINI; LAKINI KUNA CHA ZAIDI YA HAPO INAONA... TAATIFA SIO MPAKA WA IMANI...

Neno la Mungu linasema "Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu"

Pamoja na hali ya mwili wake na mke wake, IMANI ilimfanya KUONA AHADI YA MUNGU iliyo juu ya UHALISIA WA MIILI YAO.

Ni kweli UHALISIA UNASEMA HIVYO, LAKINI IKO AHADI YA MUNGU ILIYO JUU YA KILA HALI UNAYOIONA KUSHINDIKANA... IKO AHADI YA MUNGU JUU YA HIYO TAARIFA ULIYOPOKEA... USIISHIE HAPO TU.

UKIINUA MACHO ZAIDI KIDOGO UTAONA ZAIDI YA HIYO TAARIFA.... UKIINUA MACHO YAKO UTASIKIA NENO NDANI YA MOYO WAKO LINAKUAMBIA, HII SIO FINAL REPORT, KUNA AHADI YA MUNGU ILIYO JUU YA TAARIFA HIYO... HATA KAMA HAUSIKII MOYONI MWAKO, BASI POKEA NENO HILI LINALOBEBA AHADI YA MUNGU JUU YA TAARIFA HIYO AU JUU YA UGONJWA HUO AMBAO UNAONEKANA KAMA UMESHINDIKANA.

“Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.” 2 Petro 1:19 SUV

Kwenye hiyo changamoto (GIZA) liangalie NENO LA UNABII (NENO LA AHADI) kuhusiana na changamoto hiyo, litakupeleka mpaka kwenye pambazuko (JIBU) lako

Warumi 4:21-22 "huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.”

Ibrahim alijua kwa hakika kuwa Mungu anaweza kufanya yale aliyoahidi, na hicho kikahesabiwa kuwa ni haki kwake.

Imani ni kuwa na uhakika, au imani ni kujua kwa uhakika... ukishajua kwa uhakika kwamba KILE ALICHOAHIDI MUNGU anaweza akakutendea; unahesabiwa kuwa na haki ya kukipokea hicho.

Mungu anastahili kuaminiwa kwa alichoahidi kwa sababu Neno la Mungu linasema

“... mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.” Warumi 4:17 SUV

Mungu anaweza kuhuisha [kufufua] hata kilichokufa, anayataja yale yasiyokuwepo kana kwamba yamekuwako na yanatokea...

Kwa hiyo, hata kama hilo jambo linaonekana ni kama limekufa, Mungu anaweza kulifufua; hata kama linaonekana ni kama halipo, Mungu anaweza kulifanya liumbike.

--Uzuri wa IMANI INA UWEZO WA KUHUISHA AU KUFUFUA VILIVYOKUFA LAKINI PIA INA UWEZO WA KUUMBA VISIVYOKUWEPO

--Kwa kutumia IMANI, UKIMUAMINI, MUNGU ANAWEZA KUFUFUA KILICHOKUFA AU KINACHOKUFA KWENYE AFYA YAKO lakini pia anaweza KUUMBA KISICHOKUWEPO.

--Unaweza kuthubutu kuondoa macho yako kwenye uhalisia wa hali yako na kuyainua kuitazama ahadi yake ukaona akishugulika na hali hiyo?

KWA YALE ALIYOKWISHA FANYA KWENYE NENO LAKE NA KWENYE MAISHA YA WATU NA HATA KWENYE MAISHA YAKO, MUNGU ANASTAHILI KUAMINIWA KWA HALI HIYO UNAYOIPITIA; Mruhusu aingilie kati kwa IMANI YAKO KWAKE!

--Unaweza ukaamua kuondoa maswali yote na KUAMUA KUMUAMINI TU!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!