Text

Nguvu ya Neno la Mungu Maishani Mwetu

1 views 1 day ago

Waebrania 4:12-13 SUV

“Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.”

NENO LA MUNGU:

  1. Liko hai
  2. Lina Nguvu
  3. Lina ukali kuliko upanga 
  4. Lachoma - hata kuzigawanya Nafsi na Roho, na Viungo na mafuta yaliyomo ndani
  5. Li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo
  6. Vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake

UNAPOJILISHA NENO LA MUNGU:

  1. Unajilisha uhai - Kufufua kila kilichokufa maishani mwako, ikiwemo kufufua afya inayokufa au kulegea. Unasababisha maisha hai ya kiroho
  2. Unajiongezea nguvu - unaji energize kiroho na kiimani pia
  3. Unajinoa kuwa silaha kali dhidi ya adui shetani na jeshi lake
  4. Unajilisha uwezo wa kutofautisha sauti ya NAFSI yako na sauti ya ROHO yako, Sauti ya Mungu inakuwa clear zaidi kwako - Maana Mungu huzungumza na roho zetu.
  5. Unajiongezea uwezo wa kulitambua kila wazo kama latokana na Mungu au la, aidha ni wazo lako ndani yako, au ni mtu amekuletea wazo/idea, mara moja utagundua kama wazo hilo limebeba kusudi la mwovu au la Mungu
  6. Unajiongezea uwezo wa kuyatambua mambo yaliyofichika, maana vitu vyote vitakuwa utupu na kufunuliwa machoni pa Neno lililo ndani yako.

TUONGEZE BIDII KUSOMA NENO LA MUNGU.

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!