Text

Nguvu ya Ufufuo Ndani yangu

1 views 1 day ago

Warumi 8:11

Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu....

 

Roho wa UFUFUO yuko ndani yangu, na yuko na uweza wake wa KUFUFUA.

Ndani yangu kuna nguvu ya UFUFUO.

Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.

Yoh. 7:38

Mito ya Maji yaliyo hai ni ROHO Mtakatifu...

Hiyo mito ya maji yaliyo hai IKO NDANI YANGU, kazi yake ni kuhakikisha ndani yangu kuna uhai... Kila kiungo cha mwili wangu kina uzima na uhai... Kuhakikisha uhai unaingia kwa kila kiungo, kila organ, kila seli, kila tissue ndani yangu.

Lakini pia hiyo mito ya maji INAWEZA KUTOKA au KUTIRIRIKA TOKA NDANI YANGU NA KUWAENDEA WENGINE...

Kila mtu ambaye ninamuwekea mikono, ninaruhusu MITO YA MAJI YALIYO HAI KUTIRIRIKA KUMUENDEA, kwa hiyo kama kuna ugonjwa au mauti ndani yake lazima uhai uingie...

Kwa hiyo kwa mikono yangu ninaruhusu MITO YA MAJI YALIYO HAI au NGUVU YA UFUFUO kutoka ndani yangu na kusababisha UZIMA NA UFUFUO kwa kile ninachoweka mikono juu yake.

Lakini pia UZIMA NA UHAI HUU NA NGUVU HII YA UFUFUO ILIYO NDANI YANGU, ninaweza kuiruhusu kuwaendea wengine na KUWATIA uzima/kuwafufua au kuviendea vitu (biashara, maisha, ndoa na hali mbalimbali) na kuvifufua kwa njia ya KUTAMKA UZIMA KWENYE HIVYO VITU. Ndio maana Yesu akasema, maneno ninayowaambia ni Roho tena ni Uzima...

Kwa hiyo, naweza kuruhusu Nguvu hii kutoka ndani yangu na KUFUFUA kwa njia moja wapo au zote mbili, moja ikiwa ni ya KUWEKEA MIKONO na ya pili kwa njia ya KUTAMKA UZIMA juu ya kila kitu changu ninachotaka kiwe na uzima.

Kila aliye na Roho Mtakatifu ndani yake, ANAYO NGUVU YA UFUFUO NA UZIMA. Tatizo letu la msingi ni KUTOKUTAMBUA TUMEBEBA NINI NDANI YETU.

Ndani yetu tunatembea na ALIYEMFUFUA YESU lakini tunashindwa kumruhusu KUFUFUA MAMBO YETU YALIYOKUFA... Tunashindwa kumruhusu KUFUFUA AFYA ZINAZOSUMBUA.

Shetani ametudanganya kwamba NGUVU YA KUTUSAIDIA NA KUFUFUA INATOKEA MBINGUNI, kwa hiyo tunaisubiri kutoka mbinguni na wakati TUNAYE ROHO MTAKATIFU NDANI YETU NA YUKO NA NGUVU YOTE TUNAYOHITAJI.

Kama kuna kitu Shetani amefanikiwa kutudanganya watu wa Mungu, ni kutudanganya kuwa HATUNA NGUVU ZA MUNGU ZA KUTOSHA KUTATUA CHANGAMOTO TUNAYOPITIA, kwa hiyo muda wote tunasubiri Mungu aachilie nguvu ya ziada kutusaidia, wakati Neno linatuhakikishia kwamba, Roho Mtakatifu ndani yetu ana nguvu yote tunayohitaji.

Anza kwa kuamini unayo kila nguvu unayohitaji halafu chukua hatua kwa IMANI utashangaa unaona matokeo.

Kama una uhakika una Roho Mtakatifu ndani yako, amini unayo kila nguvu inayohitajika kushughulikia hali hiyo ya kufakufa na ruhusu nguvu ya Mungu ya UFUFUO kufanya kazi kwa kuwekea mikono na kwa kuendelea kutamka uzima mpaka udhihirisho.

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)
 

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!