Text

Ongeza Kiwango Chako Cha Maombi, Utaongeza Kiwango Chako Cha Utawala Kwa Njia ya Matamko yako (Neno Lako)

1 views 1 day ago

1 Wafalme 17:1 SUV

“Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.”

“Naye Eliya akamwambia Ahabu, Haya! Inuka, ule, unywe; kwani pana sauti ya mvua tele. Basi Ahabu akainuka ili ale na kunywa. Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini. Akamwambia mtumishi wake, Kwea sasa, utazame upande wa bahari. Akakwea, akatazama, na kusema, Hakuna kitu. Naye akanena, Enenda tena mara saba. Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie.” 1 Wafalme 18:41-44 SUV

MAMBO YA KUJIFUNZA:

Eliya alitoa tamko mbele ya mfalme kwamba "hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu" ambalo lilisababisha mvua kutonyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu!

Kwenye tamko la kwanza hatuoni maelezo mengi kuhusu kilichofanyika nyuma ya tamko hilo, lakini tunaona mbingu zikitii tamko hilo na kuacha kutoa mvua sawa sawa kabisa na neno la Eliya!

Sasa ni rahisi sana kufikiri kilichofunga ile mvua ni TAMKO TUPU LA ELIYA! Lakini ukifuatilia utagundua kwamba, kilichofunga mvua ni nguvu iliyokuwa nyuma ya tamko lile!

Nina uhakika kwa jinsi swala hili la mvua lilivyotesa watu lazima kuna watu wengi tu walitamka kupinga kile Eliya alichokitamka kwa hiyo lingekuwa ni tamko tupu lingetanguka tu lazima!

Ukifuatilia maandiko utagundua, KILICHOIFUNGA MVUA NI NGUVU YA MAOMBI YA ELIYA YALIYOKUWA NYUMA YA TAMKO LA ELIYA!

Kwa hiyo nguvu ya tamko ilishikiliwa na maombi!

Kwa hiyo, kumiliki anga kwa Eliya hakukua kwenye kutamka tu, bali kulikuwa kwenye maisha yake ya maombi au bidii yake ya maombi!

Kwa hiyo anga halikufungwa na kufunguliwa kwa tamko (ingawa alisema kwa neno langu) bali kwa maombi!

Ni kwa maombi tunamiliki na kutawala katika ulimwengu wa roho, halafu kwa matamko yetu tunakithibitisha kile tunachokimiliki tayari!

“Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.” Yakobo 5:17-18 SUV

Kwenye kitabu cha Yakobo imeeleza zaidi siri ya Eliya!

Ninashangaa Yakobo haongelei kabisa kuhusu alichosema Eliya, anaongelea tu kilichokuwa nyuma ya Eliya!

Kabla ya kutamka mvua kutonyesha ALIOMBA KWA BIDII na baada ya kutamka mvua kunyesha ALIOMBA KWA BIDII!

Kwa hiyo kabla au nyuma ya tamko KULIKUWA NA MAOMBI YA BIDII!

Sasa ukiangalia baada ya kuiruhusu mvua, aliomba kwa bidii na ilimgharimu kwenda mlimani na kukaa huko mpaka mtumishi wake alipoona wingu kama mkono!

Kwa hiyo NGUVU YA MATAMKO YA ELIYA ILIKUWA KATIKA MAOMBI YAKE!

Watu wengi tumekuwa hatuna matokeo kwenye ukiri wetu kwa sababu hatuna maisha STRONG ya maombi!

KILA MUOMBAJI ANAONGEZA NGUVU YA MANENO YAKE! Hasa akiwa anaomba na kujaza Neno la Mungu ndani yake

Nimekuja kugundua NGUVU HAIKO KWENYE MANENO MAZURI TUNAYOONGEA, WALA HAIKO KWENYE SAUTI KUBWA TUNAYOTUMIA WAKATI WA KUONGEA AU KUAMURU AU KUKEMEA!

NGUVU HAIKO KWENYE JINSI YA KUPANGILIA MANENO UNAPOHUBIRI AU UNAPOFUNDISHA!

NGUVU HAIKO KWENYE MA-VOCAL AU KUBANA NA KUACHIA SAUTI KWA WALE WAIMBAJI!

NGUVU IKO KWENYE MAISHA YAKO YA MAOMBI NA NENO LA MUNGU!

HIVYO VYOTE NILIVYOTAJA HAPO JUU VIKIFANYIKA BILA NYUMA YAKE KUWA NA MAOMBI NA NENO LA MUNGU, VITAISHIA KUBURUDISHA TU LAKINI HAVIWEZI KULETA MABADILIKO (KUZUIA MVUA AU KULETA MVUA)!

Usiridhike na sifa za umehubiri vizuri, au umefundisha vizuri au umeimba vizuri; siku zote tamani kile unachofanya kilete BADILIKO kwa jamii au watu!

Neno moja tu la Yesu "NJOO" liliyafanya maji ya bahari kuwa sakafu ambayo Petro alitembea juu yake!

Naamini hii haikuwa njoo tupu bali ilikuwa inasindikizwa na nguvu ya MAISHA YA MAOMBI  YA YESU MILIMANI!

Maombi yana uwezo wa kugeuza hata asili ya vitu au kanuni mbali mbali za maisha; kanuni hairuhusu mtu kutembea juu ya maji, lakini NJOO iliyotamkwa na MWENYE MAISHA YA MAOMBI ililazimisha kanuni hiyo kushindwa kufanya kazi!

Maombi yana uwezo wa kugeuza hata MAJIRA; MAJIRA YA MVUA YALIBIDI YAGEUKE ILI KUTII TAMKO LILILOTAMKWA NA MTU MWENYE MAISHA YA MAOMBI!

Kwa kadiri UNAVYOKAA MUDA MREFU KWENYE MAOMBI NA NENO, KWA KADIRI HIYO HIYO UNAONGEZA NGUVU NYUMA YA MATAMKO YAKO dhidi ya magonjwa na mambo mbali mbali ya maisha!

Tulichopishana sisi na Eliya, kwa swala hili, Neno la Mungu linasema, ni BIDII KATIKA KUOMBA

ONGEZA KIWANGO CHAKO CHA MAOMBI, [NA NENO] UTAONGEZA KIWANGO CHAKO CHA KUTAWALA KWA JIA YA MATAMKO YAKO!

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!