Pumziko la Milele Mbinguni [Rest In Peace (Rip)] Sio Kwa Watu Wote.
Ufunuo 14:13
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Neno hili Roho Mtakatifu ameliweka ndani yangu tangu alfajiri ya leo; ninaamini kuna mambo mazuri ya kukumbushana kuhusu hatma ya kila mmoja.
Kwenda Mbinguni imekuwa ndoto ya kila mtu bila kujali UMRI, DINI, TABIA, KABILA, RANGI, TAIFA NK.
Kila binadamu anayeishi, ndani yake ANGEPENDA AINGIE MBINGUNI, au ana ndoto za kwenda huko, japo wengi ni kama ndoto za wendawazimu sababu aina ya maisha na maamuzi yake haviendani kabisa na ndoto zake.
Andiko hilo nililonukuhu linaanza na kusema, "Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika,..."
"NIKASIKIA SAUTI KUTOKA MBINGUNI", A voice FROM HEAVEN...
Sauti kutoka HUKO AMBAKO TUNA NDOTO ZA KUFIKA... Sauti kujibu shauku ya mioyo yetu... Sauti kujibu ndoto zetu...
Sauti hii, sio kutoka duniani, ni kutokea huko MBINGUNI TUNAKOTAKA KWENDA AU TUNAKOKIRI KWAMBA TUNAENDA.
Sauti hii sio KUTOKA KWA MKUU WA DINI FULANI, AU KUTOKA KWA DINI FULANI, ni KUTOKA MBINGUNI AMBAKO KILA DINI INASEMA YENYEWE NDIO INASAIDIA KUWAPELEKA WATU WAKE HUKO...
Sauti hii ni kwa kila MTU ANAYESEMA DINI YAKE NDIO ITAMPEKEKA MBINGUNI...
SAUTI YA Roho wa Mungu, KUTOKA MBINGUNI, ANAJIBU SWALI NDANI YA KILA MOYO WA MTU MWENYE NDOTO ZA KUINGIA MBINGUNI.
Kwa msisitizo na UMUHIMU WA ANACHOTAKA KUSEMA, ANASEMA "ANDIKA". Yaani weka katika KUMBUKUMBU HIKI NINACHOTAKA KUKUAMBIA, USIKIPOTEZE.
Maandishi hayapotei, maandishi ni commitment.
Roho wa Mungu anasema, HAYA NINAYOENDA KUKUAMBIA, NIKO TAYARI KUJIKOMITI, NIKO TAYARI YANIFUNGE... YAANDIKE... HAYA NI YA UHAKIKA, SI MANENO MATUPU, NINATAKA YADUMU NA KUELEWEKA KIZAZI HATA KIZAZI...
Kwa sababu haya maneno yamesisitizwa kuandikwa, maana yake NI KWA AJILI YETU SISI TULIO HAI, SIO KWA AJILI YA WALIOKUFA TAYARI.
Kisha anasema HUU NDIO UJUMBE UTOKAO MBINGUNI KWA WANADAMU WOTE WALIO HAI WANAOTAKA KWENDA MBINGUNI
"Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao."
UFU. 14:13
Waambie WANADAMU HUKO DUNIANI, Wenye heri SIO WOTE WANAOKUFA, WANAOPUMZIKA (REST IN PEACE) SIO WOTE WANAOKUFA, BALI NI WALE WANOKUFA KATIKA BWANA TU, NI WALE WANAOKUFA KATIKA KRISTO PEKEE, WANAOKUFA WAKIWA WAMEMFANYA YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAO.
Wasiokufa KATIKA BWANA, hawana heri, HAWAPUMZIKI, HAPA NDIO RIP inakuwa useless.
Ujumbe huu sio kwa waliokufa, waliokufa hauwahusu, kuna kitu kingine kinawahusu waliokufa, ujumbe huu ni kwetu sisi tulio hai.
Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
EBR. 9:27
KUMKATAA YESU UKIWA HAI, NI KUYAWEKA MAISHA YAKO KWENYE HATARI (RISK) YA HALI YA JUU KULIKO HATARI NYINGINE YOYOTE ILE.
Wenye heri ni wale wanaokufa katika Kristo, ni wale waliomfanya YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAO.
Sasa hapa "Kufa katika Bwana na kumfanya Yesu Bwana" ninapaswa kuelezea pia, maana zama hizi tunazoishi KILA ANAYEHUDHURIA KANISANI ANAJIITA AMEOKOKA na MAMPA BWANA YESU MAISHA YAKE.
Kiasi kwamba wengi ukiwauliza kama wameokoka wanasema ndio, na ukiishia hapo utatoka na takwimu zisizo sahihi.
Kuna wengi wana sema YESU NI BWANA KWAO, lakini maisha yao HAYAMDHIHIRISHI YESU KUWA BWANA KWAO.
Kuna wengi wanasema YESU NI BWANA KWAO NA BADO WANA MICHEPUKO, WANATOKA NJE YA NDOA ZAO.
Wengine wanasema YESU NI BWANA KWAKO NA WANAFANYA NGONO/MAPENZI NJE NA KABLA YA NDOA.
Wengine wanasema YESU NI BWANA KWAO, NA ANA BOYFRIEND AU GIRLFRIEND, nikiwa na maana WANAISHI NA WAPENZI KINYUME NA NENO LA MUNGU.
TUAMBIANE UKWELI, HAKUNAGA WOKOVU WA AINA HIYO. SIKU ZA LEO TUMEUFANYA WOKOVU RAHISI MNO.
TUMEIFANYA KAZI YA YESU MSALABANI RAHISI KUPITA KIASI.
YESU KUWA BWANA KWAKO MAANA YAKE NI KUISHI KWA AJILI YAKE, KUKUBALI KUWA MTUMWA WAKE...
Kuishi kwa kufuata ANACHOTAKA YEYE, NI KUAMUA KUYAKA
Hubby, [01.06.21 20:34]
NA MAISHA YAKO KWA AJILI YAKE.
HAIWEZEKANI MBINGU HIYO HIYO MOJA WAINGIE WENYE MICHEPUKO, WAZINZI, WANAOISHI BILA KUJIZUIA, WANAOJIRAHISI KWA DHAMBI ETI KWA KISINGIZIO CHA NEEMA, HALAFU NA WATAKATIFU, WALIOJIKANA KWA AJILI YA YESU.
Ni lazima KUFANYA MAAMUZI YA KUMFANYA YESU BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO KWELI.
Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
UFU. 21:27
Yesu ANAMPOKEA MTU YEYOTE BILA KUJALI DHAMBI YAKE, LAKINI HATAMUACHA NA DHAMBI ZAKE, ATAMSAFISHA NA KUANZA KUMSAIDIA KUKUA KIROHO NA KUISHINDA DHAMBI.
Sio sahihi KUKAA KATIKA WOKOVU MIAKA TU IKIKATIKA LAKINI HAKUNA BADILIKO LOLOTE LA KITABIA.
Neema HUTUPOKEA TUKILVYO LAKINI HAITUACHI TULIVYO, HUTUSAIDIA KUBADILIKA.
Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
TIT. 2:11 - 12
Ukweli ni kwamba mtu yeyote ambaye KIFO KITAMKUTA WAKATI YESU SIO BWANA KWAKE(Bila kujali ana dini gani), HUYO MTU KIFO CHAKE SIO HERI BALI NI BALAA, na wala haendi kupumzika (hata akiandikiwa RIP) bali ndio mwanzo wa mateso ya milele.
Wenye heri ni wale WALIOMAANISHA sasa hivi wakiwa hai, KUMFANYA YESU KUWA BWANA WA MAISHA YAO MPAKA MWISHO.
HAO NDIO WATA RIP hata wasipoandikiwa RIP.
Ni bora KUFANYA MAAMUZI LEO, IT'S TOO RISK TO LIVE WITHOUT JESUS.
Na wale ambao tulikuwa tuko nusu nusu, NI HERI LEO TUAMUE KUISHI KWA YESU.
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Ufunuo 14:13
*#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili*
*#Umebarikiwa*
~Na. Mwl. Francis M. Langula
WhatsApp:+255754711247
Mwl. Francis Langula
Author