Text

Roho Mtakatifu Anatutamani Kiasi Cha Kutuonea Wivu

1 views 1 day ago

Yakobo 4:5

“Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?”

Neno hili linaweka wazi jambo la ajabu sana, kwamba Roho Mtakatifu anayekaa ndani yetu, ANATUTAMANI KIASI CHA KUONA WIVU.

Anatutamani hatupati, anatamani ushirika na sisi lakini hatuna muda naye kiasi ambacho ANAONEA WIVU VITU AU WATU WANAOTUNYANG'ANYA MUDA NAYE.

Hilo neno KUTAMANI linamaana KUWA NA SHAUKU KUBWA NA SISI, KUMFUKUZIA (persue) MTU kwa sababu UNAMPENDA, KUTAMANI KUWA NA MTU KWA KIWANGO CHA JUU.

Neno lililotumika hapa mtu akiwa na tamaa ya aina hii kwa mtu ndio inaitwa TAMAA MBAYA (LUST). Kwa hiyo linaonyesha SHAUKU KUU (STRONG DESIRE) ALIYONAYO ROHO MTAKATIFU KWA AJILI YETU.

Shauku hii inasababishwa na sehemu ya kwanza ya andiko hilo inayosema "Huyo Roho akaaye ndani yetu", kingereza inasema "He DWELLS in us."

Yaani AMEFANYA MAKAO NDANI YETU, ANAISHI NDANI YETU, YAANI SISI NI MAKAO YAKE, NDANI YETU NDIO MAHALI PAKE SAHIHI NA HALALI PA KUISHI, NA ANAISHI HUMU NDANI YETU KWA AJILI YETU.

Jaribu kufikiria UNAFUNGA SAFARI KUHAMA UNAKOISHI KWA SABABU UMENUNUA MAHALI FULANI PA KUISHI NA MMEINGIA MAKUBALIANO KUISHI HAYO MAKAO MAPYA PAMOJA NA MTU, NA UNAENDA PALE KWA AJILI YAKE NA SIO KWA AJILI INGINE, UNAENDA ILI MUWE PAMOJA, MLE PAMOJA, MSHIRIKI MAONGEZI NA KILA KITU PAMOJA, NA SIO HILO TU, UNAO UWEZO WOTE WA KUMSAIDIA UNAYEENDA KUISHI NAYE MAKAO MAPYA KAMA AKIKUPATIA NAFASI, HALAFU UKIHAMIA HUKO, UNAKARIBISHWA VIZURI LAKINI BAADA YA HAPO SIKU ZINAKATIKA MUHUSIKA YUKO BUSY NA MAMBO MENGINE, BUSY NA KAZI, TV, NA MENGINE MENGI, HANA MUDA KABISA NA WEWE, NA MBAYA ZAIDI KUNA MAMBO UNAONA WAZI ANAHANGAIKA NAYO AMBAYO UNAO UWEZO WOTE KUMSAIDIA NA NDIO HAYO YAMEKULETA KUISHI NAYE, NA UNAJARIBU KUONYESHA ISHARA ZOTE NA HATA KUZUNGUMZA LAKINI HAKUELEWI.... NA HAYO MAKAO MAPYA NDIO MAKAO YAKO YA KUDUMU NA HUYO MTU.... INAFIKA POINT, UNATAMANI ULE USHIRIKA KIASI CHA KUONA WIVU, KUONEA WIVU KILA ANACHOKIFANYA.

Ndicho hili Neno linachotueleza, ndio HALI YA ROHO MTAKATIFU NDANI YETU.

Roho Mtakatifu ndani Yetu hana agenda yake binafsi, YUKO KWA AJILI YETU. Ameacha makao mbinguni, amenunuliwa makao mapya ambayo ni MIILI YETU, na ANAISHI RASMI NDANI YETU, NA AMEKUJA NA KILA UWEZO WA KI-MUNGU KUTUSAIDIA.

Yeye ni MSAIDIZI, MFARIJI, MWOMBEZI, MSHAURI, MLINZI, WAKILI, MUNGU, NK na yuko ndani yetu kwa kazi hiyo; Lakini, tuko busy tukitafuta WASHAURI wakati tunayemshauri ndani yetu anatusubiri, tuko busy kutafuta wa KUTUOMBEA wakati tunaye MUOMBEZI MKUU ndani yetu, tunatafuta FARAJA wakati tunaye MFARIJI MKUU NDANI YETU....

Sasa anapoendelea kuiona hali hiyo, NDANI YAKE INAIBUKA SHAUKU YA HALI YA JUU SANA, ANAANZA KUTUTAMANI KIASI CHA KUONA WIVU.

Mbaya zaidi ni kwamba, wengine kati yetu, TUMEWAHI KUWA NA UHUSIANO MZURI SANA NA ROHO MTAKATIFU.

Tumewahi kuwa hatufanyi kitu bila kuwa na uhakika Roho Mtakatifu ameridhia, tumekuwa tukiongea naye, tukimruhusu aombe pamoja na sisi, na alitufikisha mbali, tuliweza kuwa na ushirika naye masaa mengi, kuwa naye katika mikesha, mifungo mirefu bila hata kukumbuka chakula.

Kuwa naye kwenye UWEPO WAKE mpaka tunasahau kila kitu, tunasahau SIMU, TV, NK.

Tulikuwa tunaishi kwa ajili yake, hutukuweza kufanya jambo kama tunahisi litamuhuzunisha... Tulikuwa tunaishi maisha ya Nidhamu na kujitunza na utakatifu tukiutambua uwepo wake kila mahali.

Alikuwa ndiye rafiki wa karibu, LAKINI KWA SABABU MOJA AU NYINGINE, ULE UHUSIANO UKAANZA KUPOTEA, WENGINE WAKAMKASIRIKIA TU SABABU KUNA MAMBO HAYAKWENDA KAMA WALIVYOTARAJIA, AU KUNA CHANGAMOTO WALIKUTANA NAZO MFULULIZO WAKAJIKUTA WANAPOA NA KUUPOTEZA USHIRIKA HUU WA THAMANI.

Mahusiano yakaenda yanapotea mpaka sasa yamefika mahali ni kama yamekufa, yamepotea kabisa au yamekuwa baridi kabisa.

Ukweli ni kwamba Roho Mtakatifu bado yuko ndani Yetu, hajaondoka lakini tumepoteza ushirika naye.

Akikumbuka siku zilizopita tulivyohusiana, ANATUTAMANI KIASI CHA KUTUONEA WIVU. Anazimiss zile siku tulikuwa tunakaa kwenye uwepo wake masaa, zile zama za kujilinda na kujitunza kwa ajili yake, zile zama za mifungo mirefu na kusoma Neno, zile zama za fellowship naye....

He misses us, He misses the precious moments we used to have together.

ANATUTAMANI KIASI CHA KUTUONEA WIVU.

USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU NDIO JAMBO LA KWANZA LA MUHIMU KWENYE MAISHA YA WOKOVU. HII NI MUHIMU KULIKO HATA KUMTUMIKIA MUNGU, NI MUHIMU KULIKO KUHUBIRI.

Roho Mtakatifu anatuhitaji sisi kuliko vipawa vyetu, kuliko pesa zetu, kuliko kingine chochote.

Ushirika wetu na Roho Mtakatifu ndio utazalisha MATOKEO YENYE TIJA KWA KILA TUNACHOFANYA, VINGINEVYO INAWEZEKANA KILA TUNACHOMFANYIA MUNGU KIKATEKETEA KWA MOTO.

“Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?” Yakobo 4:5

Maneno haya YAPIGE KELELE NDANI YETU, TUJITATHIMINI MAHUSIANO YETU NA ROHO MTAKATIFU KWA UPYA NA TUANZE TENA KUUTHAMINI USHIRIKA HUU WA MUHIMU.

Anatusubiri kwake, ANATUONEA WIVU, ANATUTAMANI SANA, YUKO NDANI YETU KWA AJILI YETU NA SIO KWA AJILI YA KITU KINGINE.

AMEACHA MBINGU KUJA KUISHI NA SISI DUNIANI, NA MIILI YETU NI HEKALU LAKE, NDIO MAHALI PAKE PA KUISHI MPAKA WAKATI UTAKAPOFIKA TUNYAKULIWE PAMOJA NAYE MBINGUNI, HANA MPANGO WA KUTUACHA, SIKU ANARUDI MBINGUNI NDIO SIKU YA UNYAKUO, HE IS OUR ETERNAL PARTNER.

Anatutamani kiasi cha kutuonea wivu, turudi kwake anatungojea.

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!