Roho Ndiyo Itiayo Uzima, Mwili Haufai Kitu
Yohana 6:63 SUV
"Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima."
Hivi karibuni nilihudhuria msiba mmoja na nilichokiona kilinifanya maneno haya "Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu" yaimbe ndani yangu, na hata baada ya kutoka msibani, Neno hili limekuwa ndani yangu na Roho Mtakatifu akanisaidia kuona vitu vya muhimu sana kwenye neno hili.
Haya ndio nimekuwa nikitafakari:-
-- Mtu anapokufa, lazima mara moja mwili wake unatakiwa unyooshwe na kurekebishwa viungo vyake vinginevyo utakakamaa na haitawezekana kumuweka sawa!
Kwa hiyo, tukiongea kwa ujumla, roho ndani ya mwili ndio husababisha mwili usikakamae na kuwa kama jiwe
--Mtu anapokufa, mara moja mwili wake unatakiwa uchomwe sindano za kumzuia asiharibike, akichelewa mwili utaharibika na kuanza kuoza kwa kasi kubwa sana ndani ya masaa machache tu!
Kwa hiyo, tunaweza kusema, roho ndani ya mwili ndio huzuia mwili kuoza
-- Mtu anapokufa Mapigo ya moyo husimama kufanya kazi, ubongo huacha kufanya kazi, damu huacha kuzunguka nk.
-- Mtu anapokufa, hata kama viungo vyote huonekana ni vizima, dakika hiyo hiyo huacha kufanya kazi.
Kwa hiyo, tunaweza kusema, roho ndani ya mwili ndio husababisha viungo hivyo kufanya kazi
-- Mtu anapokufa, dakika hiyo hiyo mwili unaanza mchakato wa kuwa mavumbi, na baada ya siku si nyingi, ukitafuta mkono, mguu, na sehemu zingine za mwili hautaziona maana tayari zitakuwa zimegeuka kuwa MAVUMBI!
KWA HIYO, KINACHOFANYA HUO MWILI UONEKANE NA KUFANYA KAZI SIO MWILI WENYEWE, BALI NI ROHO! Ndio maana roho ikitoka tu, mwili na hivyo viungo huwa udongo.
Kwa hiyo uzima wa mwili haupo kwenye mwili kama ambavyo tumekuwa tunafikiri hata kama kuna kitu katika mwili kimekufa si hakifanyi kazi, kwa kuwa chanzo cha uzima wa mwili sio mwili bali ni roho basi roho yaweza kuhuisha kilichokufa!
Uwezo wangu wa kuinua mkono hauko kwenye mkono wenyewe...
Uzima wa figo zangu hauko kwenye figo zangu...
Uzima wa mguu wangu hauko kwenye mguu wangu...
Uzima wa mwili wangu uko kwenye roho yangu, ndio maana hata kama kila kitu cha mwili kiko sawa sawa, roho ikitoka ndani ya mwili, vyote vinaacha kufanya kazi.
Hii inanifanya kufikiri (naweza kuwa sahihi au la, lakini inaleta maana kufikiri hivyo), kwamba kila kiungo cha kimwili kina kiungo chake cha kiroho ambacho kinakifanya kiungo hicho cha kimwili kuwa hai au kufanya kazi sawasawa! Ndio maana siku roho ikiondoka na viungo vyake vyote vya kiroho, mwili na viungo vyake vyote huacha kufanya kazi au kwa lugha nyingine hufa!
Kwa hiyo, kama roho iko ndani ya mwili, na kuna kitu kwenye mwili wangu hakifanyi kazi, Uzima wa roho yangu [kama roho yangu ni hai] unaweza kabisa kusababisha uzima wa mwili wangu.
Ndio maana Neno likasema, ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA, MWILI [PASIPO ROHO] HAUFAI KITU! Maana yake, UZIMA WA MWILI WANGU UNATEGEMEA UZIMA WA ROHO YANGU!
Sasa hii haimaanishi kila roho iliyo ndani ya mwili hiyo Roho ni hai na ina uwezo wa kuhuisha mwili... nitaelezea hili zaidi hapo chini.
SASA TURUDI TENA KWENYE NENO LETU
"Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima." Yohana 6:63 SUV
Ukifuatilia maandiko, utagundua, baada ya anguko la Adam, roho ya mwanadamu ilikufa yaani uhusiano wake na Mungu ulikata, na hicho ndicho Yesu alikuja kurejesha!
Baada ya anguko la Adam, roho ya mwanadamu ilibakiziwa nguvu ya kuufanya tu mwili uwe hai, roho hiyo inapokuwa ndani ya huo mwili; lakini haikuwa na nguvu tena ya kuuhuisha mwili au viungo mbali mbali vya mwili vinapopata hitilafu hasa zisizotibika!
KABLA YA ANGUKO ROHO YA ADAMU ILIKUWA NA UWEZO WA KUHUISHA MWILI (YAANI KUHAKIKISHA MWILI HAUUMWI WALA SELI ZAKE HAZIFI), LAKINI UWEZO HUO ULIKWISHA BAADA YA ANGUKO
Yesu alikuja KUHUISHA ROHO ZETU, NA KUZIPA UWEZO WA KUUHUISHA NA MWILI PIA!
ROHO ZETU ZINAHUISHWA KWA KULIPOKEA NENO LA MUNGU LILILOVUVIWA, ZINAPOHUISHWA KWA MARA YA KWANZA NDIO TUNAITA KUOKOKA, KUZALIWA UPYA KWA NENO! LAKINI PIA KILA TUNAPOHUDUMIWA NA NENO LA MUNGU, TUNAPOKEA NGUVU YA UZIMA AMBAO UNAWEZA KWENDA MPAKA KWENYE MIILI YETU NA KUHUISHA KILA KILICHOKUFA.
Ndio maana Yesu akasema, "Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima."
Kwa hiyo, ukilipokea Neno la Mungu la uponyaji na kuliamini, haijalishi mwili wako una hali gani, NENO LINAWEZA KUHUISHA MWILI WAKO NA KUKUPONYA KABISA!
NDIO MAANA SEHEMU YA PILI YA ANDIKO HILO YESU AKASEMA "MANENO HAYO NILIYOWAAMBIA NI ROHO TENA NI UZIMA"
Kwa hiyo, hata kama ugonjwa umeshindikana kwa madaktari, KWA PUMZI ILIYOKO KWENYE NENO LA MUNGU, MWILI UNAWEZA KUHUISHWA NA HUO UGONJWA KUPONA KABISA!
Roho wa Mungu ndio hulipa uhai Neno kutuhuisha na kuhuisha miili yetu.
"Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu." Warumii 8:11 SUV
Sasa si rahisi sana kuelezea kila kitu kwa undani lakini ninaamini Mungu atatusaidia kupata mwanga kwa maelezo haya mafupi!
LAKINI PIA KWA TAFAKARI HII, TUNAPASWA KUHAKIKISHA TUNAUPA KIPAUMBELE UZIMA WA ROHO ZETU!
Neno la Mungu linasema, Roho itendayo dhambi ndio itakayokufa, na kifo cha roho ndio kinamfanya mwanadamu aende JEHANAMU MILELE NA MILELE!
KILA MTU AMBAYE HAJAMPA YESU MAISHA YAKE, ROHO YAKE IMEKUFA!
Kama roho ni mfu, MWILI HAUFAI KITU, KUJIPAMBA NA KILA KIZURI KWENYE MWILI NI UBATILI TU, HAKINA MAANA. KWA HIYO HAKIKISHA ROHO YAKO INA UZIMA KWA KULIKUBALI NENO LA YESU LA WOKOVU NA KUOKOKA!
"Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi[roho] yake?" Marko 8:36 SUV
Kwa kila unalolifanya duniani au katika mwili, hakikisha halidhuru UHAI WA ROHO YAKO - UHUSIANO WAKO NA MUNGU KWA YESU KRISTO, maana huo ni muhimu kuliko yote.
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author