Text

Roho ya Uzinzi na Mauti Huambatana!

2 views 1 day ago

1 Wakorintho 6:18 SUV

“Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.”

MAMBO YA KUJIFUNZA:

Neno la Mungu linasema, yeye afanyaye zinaa au aziniye hu     fanya dhambi juu ya mwili wake mwenyewe!

Tafsiri nyingine inasema kwamba yeye aziniye HU     FANYA DHAMBI KINYUME NA MWILI WAKE, na tafsiri nyingene inasema HUFANYA DHAMBI NDANI YA MWILI WAKE!

Yaani HUPIGANA NA MWILI WAKE AU ANAFANYA UADUI NA MWILI WAKE AU HUIINGIZA DHAMBI NDANI YA MWILI yaani huruhusu dhambi kuingia na kukaa ndani ya MWILI WAKE!

“Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.” Mithali 6:32-33 SUV

“But whoever commits adultery with a woman lacks heart and understanding (moral principle and prudence); he who does it is destroying his own life. Wounds and disgrace will he get, and his reproach will not be wiped away.” Proverbs 6:32-33 AMPC

Kuna mambo manne au matano yametajwa hapa kwa kila mtu afanyaye uzinzi:-

1) Hana akili (lacks heart and understanding (moral principle and prudence))

- Amepungukiwa akili za moyoni na ufahamu (kanuni za maadili na busara)

- Maana yake ameamua kutokutumia akili yake ipasavyo, kwa hiyo Mungu hamtegemei mwenye akili za kiroho kufanya uzinzi!

2) Anafanya jambo la kumuangamiza (destroying his own life)

- Anajiangamiza maisha yake mwenyewe, ni sawa kabisa na mtu anayejiwekea sumu kwenye chakula au aliyetega bomu ndani ya nyumba yake!

3) Atapata jeraha (la Moyo)

- Moyo wake hautabaki salama kwanza na hali ya hukumu ndani; lakini pia kwa sababu ya udanganyifu maana udanganyifu hujeruhi moyo!

4) Anajivunjia Heshima Yake

- Kila mtu anayeruhusiwa access kwenye mwili wako kinyume na utaratibu wa Neno la Mungu maana yake unaruhusu HESHIMA YAKO KUSHUKA KWA MTU HUYO

- Lakini pia haiishii hapo, HESHIMA NI UTU     KUFU, haiwezekana UTUKUFU WA MUNGU UBAKI KWA MTU ASIYETUNZA MWILI WAKE!

5) Anajifedhehesha (reproach will not be wiped away)

- Hujisababishia mashitaka, shutuma na lawama za adui!

UZINZI SIO TENDO TU BALI NI ROHO:

“Matendo yao hayatawaacha kumgeukia Mungu wao; maana roho ya uzinzi imo ndani yao, wala hawamjui BWANA.” Hosea 5:4 SUV

ROHO YA UZINZI HUAMBATANA NA ROHO YA MAUTI:-

“Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu;” Mithali 5:3-5 SUV

MIT. 7:5, 7, 21-23, 27 SUV "Wapate kukulinda na malaya, Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake. Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili, Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda. Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu; Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake. Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.”

Maandiko hayo yameweka mambo magumu zaidi!

Kila NJIA YA UZINZI INA UCHUNGU, MAUTI NA KUZIMU NDANI YAKE ingawa m     wanzoni yaweza kuonekana njia hiyo INADONDOZA ASALI

Imemfananisha anayefuata njia ya uzinzi ni sawa kabisa na ng'ombe aendaye KUCHINJWA! Au mtu mpumbavu anayejipelekeka KUFUNGWA PINGU na kuruhusu MSHALE UMCHOME au NDEGE AKIMBILIAYE MTEGONI asijue      ni KWA HASARA YA NAFSI YAKE!

ROHO YA UZINZI NA MAUTI ZILIVYOFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO KATIKA BIBLIA:-

“Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake. Hata ikawa asubuhi, Daudi akamwandikia Yoabu waraka, akaupeleka kwa mkono wa Uria. Akaandika katika waraka huo, kusema, Mwekeni Uria mbele ya watu penye vita vikali, kisha ondokeni, mmwache, ili apigwe akafe.” 2 SAM. 11:4, 14-15 SUV

Baada ya Daudi kulala na mke wa Uria, kwa sababu roho ya uzinzi huambatana na roho ya mauti, ndipo roho ya kuua ikamuingia akaamua kumuua Uria bila hata kuona anafanya dhambi!

“Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu. Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, ndipo mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, iweni na ujasiri.” 2 SAM. 13:11, 14, 28 SUV

Roho ya uzinzi iliyokuwa ndani ya Amnoni hata akambaka Tamari iliambatana na mauti yake Amnoni! Ingawa ilikaa miaka miwili na Amnoni mwenyewe akasahau, lakini maadamu ilikuwa haijatubiwa, ile mauti ilikuwa inamtafutia nafasi tu!

Ukitaka kujua kweli jinsi gani roho ya uzinzi huambatana na roho ya mauti, fuatilia ni watoto wangapi wamebaki yatima kwa sababu tu ya wazazi wao kufa kwa magonjwa ya zinaa

Angalia ni mauaji mangapi yameshatokea sababu ya wivu wa mapenzi na mafumanizi.

Angalia ni watoto wangapi wameuawa kabla ya kuzaliwa (abortion) kwa sababu ya kufanya uzinzi na kubeba mimba kabla ya wakati!

Angalia ni watu wangapi magonjwa ya zinaa yamekatisha maisha yao!

Angalia ni ndoa ngapi zimekufa sababu ya uzinzi

Angalia familia ngapi zilikuwa nzuri na zimekufa sababu ya uzinzi.

MUNGU HAWEZI KUTUZUIA JAMBO LISILO NA MADHARA KWENYE MAISHA YETU! Kwa hiyo hata kama sijaona MADHARA YALIYOTAJWA ninapaswa KULITII NENO LA MUNGU TU MAANA NENO LA MUNGU NI KWELI!

Miili yetu ni chombo cha thamani sana MBELE ZA MUNGU na kwakweli hakuna      sababu yoyote yenye nguvu kutufanya tutoe miili y     etu kwa zinaa!

“maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu” 1 KOR. 6:20 SUV

Miili yetu ni mali ya Mungu kabisa! Yesu aliinunua miili yetu kwa gharama kubwa!

“Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.” 1 PET. 4:2 SUV

Ni vizuri kugeuka na Kumrudia Mungu kwa toba kabla MAUTI haijaingia!

Ni bora kuwa kama wale manabii na kumpigia mtumishi wa Mungu na kumwambia "MAUTI IMO SUFURIANI"

“Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu wa Mungu. Wala hawakuweza kula.” 2 FAL. 4:40 SUV

Kama unajua fika kwamba MAITI IMO SUFURIANI ni vizuri usiendelee kujikausha!

“Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.” 1 KOR. 6:18 SUV

 

#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili

Umebarikiwa

~Na. Mwl. Francis M. Langula

(+255754711247)

Comments (0)
Login to leave a comment.

No comments yet. Be the first to comment!