Shika Sana Ulicho Nacho, Asije Mtu Akaitwaa Taji yako - Sehemu ya II
Yesu aliposema "Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, ASIJE MTU akaitwaa taji yako. UFU. 3:11"
Kwenye sehemu ya pili ya TAFAKARI hii, nataka tuangalie zaidi kipengele ASIJE MTU akaitwaa taji yako
Kimsingi alichokuwa anasema hapo ni kwamba, UWE MWANGALIFU UNAVYOHUSIANA NA WATU! Maana ni MTU (Sio shetani) NDIO anaweza kuitwaa taji yako!
Kila uhusiano ambao ukiufuatilia unagundua tangu umeuanza TAJI YAKO imeanza kuliwa au imetwaliwa basi huo sio uhusiano sahihi!
MAANA YAKE NINI?
1) Kila uhusiano na MTU ambao unakusababisha uishi maisha ya DHAMBI, ujue huyo ndio MTU anayezungumziwa hapo, anaiharibu taji yako!
“Taji ya kichwa chetu imeanguka; Ole wetu! Kwa kuwa tumetenda dhambi.” Maombolezo 5:16
Kwa hiyo kila anayekusababishia kutenda dhambi au anayekusababisha uishi maisha ya dhambi sio mtu sahihi kuhusiana naye, maana ataimega taji yako!
2) Kila uhusiano na MTU ambao tangu umeuanza umegundua HESHIMA YAKO IMESHUKA, ujue MTU huyo ameitwaa au ameimega taji yako!
“Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;” Zaburi 8:5 SUV
Kwenye maandiko hayo, TAJI ni HESHIMA na UTUKUFU maishani mwa mtu! Kwa hiyo ukiona mtu yeyote TANGU UMEANZA KUHUSIANA NAYE Heshima yako Inashuka (mbele za watu, mbele ya jamii, kanisa, kazini nk), ujue wazi HUYO NDIO ANAZUNGUMZIWA!
3) Kila uhusiano na MTU ambao tangu umeuanza umegundua UWEZO WAKO WA KUJIZUIA umepungua au umeisha basi ujue MTU HUYO anakuzuilia au anaitwaa taji yako!
“Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.” 1 Wakorintho 9:25 SUV
Kwa andiko hilo utagundua, Maisha ya kujizuia hupelekea kushinda na kuvikwa TAJI! Kwa hiyo kila mtu ambaye anakusababisha ushindwe kujizuia, HUYO ANAIMEGA TAJI YAKO
4) Kila uhusiano na MTU ambao tangu umeuanza umegundua umeathiri uwezo wako wa KUSTAHIMILI MAJARIBU, ujue MTU huyo anakuzuilia taji yako
“Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.” Yakobo 1:12 SUV
Tukistahimili majaribu tutavikwa taji, kwa hiyo kama kuna MTU AMBAYE ANAATHIRI USTAHIMILIVU WETU tunapohusiana naye maana yake ANAATHIRI NA TAJI LETU!
5) Kila uhusiano na MTU ambao tangu umeuanza umegundua FURAHA YAKO imeshuka au imeondoka basi ujue MTU HUYO anaitwaa taji yako!
“Basi, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, hivyo simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.” Wafilipi 4:1 SUV
KWAHIYO, TUWE MAKINI SANA SANA TUNAPOHUSIANA NA WATU!
Kama umegundua kuna mtu wa aina moja wapo nimeitaja hapo juu, ambaye una uhusiano naye; BASI CHUKUA TAHADHARI!
AU KAMA AMESHAITWAA TAJI YAKO, fanya maamuzi sahihi, VUNJA HUO UHUSIANO NA UMRUDIE MUNGU!!
#UponyajiWaKiMunguKwaWoteWenyeMwili
Umebarikiwa
~Na. Mwl. Francis M. Langula
(+255754711247)
Mwl. Francis Langula
Author